Mamlaka za Mahouthi Zaendelea na Ukamataji wao wa Kidhulma dhidi ya Wabebaji Dawah ya kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu katika Mashababu wa Hizb ut Tahrir
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 16 Shawwal 1444 H sawia na 6/5/2023 M, mamlaka za Mahouthi zilimkamata Mhandisi Shafiq Khamis, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, mbele ya nyumba yake katika mji mkuu, Sana'a, bila ya mashtaka yoyote isipokuwa uanachama wake na Hizb ut Tahrir, ambayo inafanya kazi ya kurudisha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu baada ya kutoweka kwake katika maisha ya Waislamu.