Jumanne, 18 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  13 Dhu al-Qi'dah 1447 Na: HTY- 1447 / 19
M.  Alhamisi, 30 Aprili 2026

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

Dada Lamya bint Bashar

(Imetafsiriwa)

[يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ * ارْجِعِي إِلَى رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً * فَادْخُلِي فِي عِبَادِي * وَادْخُلِي جَنَّتِي]

Ewe nafsi iliyo tua! * Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha * Basi ingia miongoni mwa waja wangu * Na ingia katika Pepo yangu.” [Al-Fajr:27–30]

Mnamo Jumatano tarehe 12 Dhu al-Qa‘dah 1447 H sawia na tarehe 28 Aprili 2026 M, dada mwema, mbebaji da’wah aliyefanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, mwanachama katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Yemen, Dada Lamya bint Bashar alifariki.

Mwenyezi Mungu amrehemu dada yetu mwema ambaye aliitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Aal-i ‘Imran:104].

Hivyo alifungua moyo wake na nyumba yake ili kuandaa halaqa za Hizb ut Tahrir zenye lengo la kuwaelimisha wabebaji Da‘wah kwa hukmu za Uislamu na fikra zake.

Na nyumba yake ilikuwa alama ambayo wale wenye hamu ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu waliongozwa, katika kuhudhuria vikao vya pamoja na kushiriki kikamilifu katika semina miongoni mwa wanawake. Ili nyumba ya dada yetu huyu mwema iwe mfano wa kuigwa na kutafuta baraka kutoka kwa nyumba ya swahaba Al-Arqam ibn Abi Al-Arqam, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ambaye alishuhudia kukusanyika kwa Waislamu wa kwanza kutoka kwa maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), akiwasomea yale yaliyofunuliwa kwake kutoka kwa Qur’an na kuondoa fikra za ujinga kutoka akilini mwao na kuweka mahali pao hukmu za Uislamu na fikra zake, akiunda kutoka kwao shakhsiya za Kiislamu zilizoongoza ulimwengu kwa Uislamu na kuwashinda Wafursi na Warumi.

Dada yetu mwema hakuzuiliwa na mateso ya maradhi kutokana na kubeba Da‘wah na kuharakisha kwenye amri ya Mwenyezi Mungu:

[وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ]

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu.” [Aal-i ‘Imran:133]. Na kauli ya Mtume wake (saw): «اغْتَنِمْ خَمْساً قبلَ خَمْسٍ: شبابَكَ قبلَ هَرَمِكَ، وصِحَّتَكَ قبلَ سَقَمِكَ، وغِناءكَ قبلَ فَقْرِكَ، وفَراغَكَ قبلَ شُغلِكَ، وحياتَكَ قبلَ موتِكَ» “Patiliza mambo tano kabla ya tano: ujana wako kabla ya uzee wako, afya yako kabla ya ugonjwa wako, utajiri wako kabla ya umaskini wako, wakati wako wa faragha kabla ya shughuli zako, na maisha yako kabla ya kifo chako.” (Imeripotiwa na Al-Hakim katika Al-Mustadrak kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili)

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amfunike dada yetu kwa Rehema Zake Kubwa, na amkubali miongoni mwa wale aliowaneemesha katika manabii, wakweli, mashahidi, na waadilifu—na ni maswahaba bora walioje hao. Na tunamuomba awape familia yake na jamaa zake uvumilivu na faraja. Na hatusemi chochote isipokuwa kile kinachomridhisha Mola wetu Aliyetukuka: [إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizbuttahrir.today
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu