Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah Itakomesha Ugaidi

 (مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا)

"… aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote." [TMQ Al Maidah 5: 32]

Septemba 11, 2020 inaashiria kumbukumbu ya miaka 19 ya shambulio la 9/11, ambalo linachukuliwa kuwa tukio baya zaidi lililotokea kwenye ardhi ya Amerika.

Siku hiyo ya kutisha, mashambulizi manne makubwa yalitokea kwenye Jumba la Twin Towers la Kituo cha Biashara cha Ulimwengu, Pentagon na ndege nyingine iliyorushwa kuelekea Washington DC ilianguka katika uwanja huko Pennsylvania ambayo yaligharimu maisha ya watu karibu 3000 na kujeruhi zaidi ya watu 6000. Shambulizi la 9/11 lilitumika kama uhalalisha wa 'Vita dhidi ya Ugaidi' vya Amerika na likawa ni muktadha wa Waislamu ulimwenguni kupewa kibandiko cha Magaidi, Wenye Misimamo Mikali, Wenye Siasa Kali na kila uchao orodha hii inakua.

Shambulizi la 9/11 lilidaiwa kuwa la wanamgambo 19 wa Al Qaeda, wengi wao walikuwa raia wa Saudia. Kufuatia mashambulizi ya 9/11, kwa jina la kulinda raia wa Amerika, Amerika ilivamia Afghanistan mnamo 2001. Pia ilivamia Iraq mnamo 2003 ingawa hakuna hata mmoja wa wanamgambo hao wanaodaiwa alikuwa anatoka Iraq.

Kilichoanza kama 'Vita dhidi ya Ugaidi' hakikuwa tu ni vita dhidi ya ugaidi au vita dhidi ya wanamgambo wachache bali ilikuwa ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ilithibitishwa baadaye wakati wa Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Syria wakati wa wanachama wa chama cha Republican walimtaka Obama kuviita 'Vita dhidi ya Ugaidi' kama 'Vita dhidi ya Uislamu'. Chuki dhidi ya Waislamu iliendelea kuenezwa kupitia vyombo vya habari, chaneli za habari, majarida na hata sinema za Hollywood zilionyesha Waislamu kama magaidi. Kitendo chochote cha vurugu kinachodaiwa kwa Waislamu kitaitwa kama 'Ugaidi' lakini kitendo chochote cha vurugu kinachodaiwa kwa wengine kitaitwa kama 'ubwana wa wazungu' au kutokana na matatizo ya kisaikolojia. "Kukomesha Ugaidi" pia ni karata kuu inayotumiwa na viongozi wakati wa kampeni za uchaguzi. Ulimwengu una ubaguzi wa rai jumla kama "Waislamu wote sio Magaidi lakini Magaidi wote ni Waislamu".

Wakati Amerika inapojifanya kama mkombozi kutokana na Ugaidi, hebu tuchunguze hatua za Amerika. Amerika ilidai shambulizi la 9/11 liliua watu 3000 na kujeruhi zaidi ya 6000. Ili kulipiza kisasi, Amerika ilitangaza 'Vita dhidi ya Ugaidi' juu ya Afghanistan na Iraq. Kulingana na ripoti ya Lancet mnamo 2006, kati ya 2003-2006, zaidi ya watu 650,000 walipoteza maisha yao nchini Iraq kwa sababu ya 'Vita dhidi ya Ugaidi', ambapo zaidi ya watu 200,000 walikuwa ni raia wa kawaida. Hii ilizidi hata utawala dhalimu wa Saddam wa miaka 30 ambao uliua watu 200,000 kikatili. Unafiki wa Amerika unafichuliwa zaidi kupitia vipaumbele vyao vya nyumbani kuhusu kuokoa maisha.

Ugaidi umeua zaidi ya watu 3300 nchini Amerika wakati wa 1995 - 2014. Kwa kulinganisha, idadi ya vifo vilivyosababishwa na Saratani, matumizi ya kupita kiasi ya dawa aina ya Opioid, uhalifu wa Bunduki unasimama kwa viwango vya kutisha vya 600,000 (2018), 70,000 (2017), takriban 15,000 kwa mwaka. Wakati Amerika ilitumia dolari bilioni 6 kwa mwaka kupambana na saratani, ilitumia dolari bilioni 186 kwa mwaka kupambana na ugaidi. Bila ya kutaja kiwango duni cha pesa inachotumia kupambana na uhalifu wa bunduki au matumizi ya kupita kiasi ya dawa aina ya Opioid. Vile vita vya Amerika vinavyoitwa 'Vita dhidi ya Ugaidi' viliharibu maisha na mali za Waislamu wa nchi nyingi na vikawafilisi watu wa Amerika. Watu pekee ambao walionekana kufaidika ni 'Warasilimali Wapigiaji Debe Vita' wa kitengo cha ulinzi cha Amerika. Dharau ya Amerika kwa maisha na mali ya watu imefunuliwa kwa maneno ya Condoleezza Rice, (Waziri wa zamani wa Kigeni wa Amerika) ambapo alitoa maoni yake mnamo 2006 kwamba "Iraq isiyokuwa na utulivu ilikuwa bora kuliko Iraq thabiti iliyokuwa chini ya mikono ya watu wenye siasa kali", akihalalisha Uvamizi wa Amerika nchini Iraq mnamo 2003. Kauli yake ilikuwa sawa na ya Madeleine Albright (Waziri wa zamani wa Kigeni wa Amerika na balozi wa Amerika katika UN) mnamo 1996, "Gharama hiyo inastahiki", kuhalalisha vikwazo vilivyoongozwa na Amerika juu ya Iraq kuanzia 1991 vilivyoua watoto zaidi ya 500,000 kwa sababu ya utapiamlo. Hadi leo, 'Vita dhidi ya Ugaidi' bado havijamalizika na milioni chache wakiwa wamekufa na mamilioni wengi wakikosa makao. Madai ya Amerika kama 'Demokrasia Kubwa zaidi ulimwenguni' yanamaamisha tu kifo, uharibifu na deni.

Je! Magaidi halisi hapa ni kina nani? Je! Amerika inajali maisha ya wanadamu? Kwa nini wanajenga chuki nyingi sana dhidi ya Waislamu? Kwa nini wanaua maisha ya wengi wasio na hatia kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu na raia wao wenyewe? Kwa nini wanaharibu mataifa yote kama Afghanistan, Iraq, Syria, Yemen

Kwa kutumia neno "Ugaidi", makumi na maelfu ya Waislamu wameuawa vitani, chuki dhidi ya Waislamu imeenea, hofu kwa maneno kama Shariah, Jihad, Dola ya Kiisilamu yameasisiwa na sheria za kupambana na ugaidi zinazochochea hofu kati ya Waislamu hata kujadili kuhusu ukamilifu wa Uislamu. Cha kukasirisha zaidi hapa ni kwamba Amerika imefanya uharibifu huu kwa jina la kupambana na Ugaidi. Kinyume chake, kuingilia kwao mambo ya watu na uvamizi imekuwa sababu ya kutokuwa na utulivu ulimwenguni! Paul Bremmer, ambaye aliandika katiba ya Iraq na ambaye pia aliitwa na wakosoaji kama "Baba wa ISIL". Gereza la Amerika nchini Iraq liliitwa na wakosoaji kama Chuo Kikuu cha Jihad.

 (وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُون)

"Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji." [TMQ Al-Baqarah 2:11]

Licha ya ukatili wa wazi wa Amerika, ulimwengu umeufungia macho na yale yanayoitwa kuwa ni mataifa yenye nguvu kamwe hayasimami dhidi yake. Hii ikiwa ni pamoja na watawala kutoka katika nchi za Kiislamu ambao wanashirikiana na Amerika katika dhulma zote dhidi ya Waislamu na kuusaliti Ummah wetu.

Dola ya Khilafah ijayo itakomesha Ugaidi huu wa Amerika. Nyoyo na akili za Watawala, Ummah, Wanajeshi zitajazwa na Iman na UchaMungu, ambao wataweka haki na kuregesha amani.

(يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ)

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [TMQ As-Saff 61:8]

Imeandika kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ayeesha bint Mohammed

Maregeo:

https://www.statista.com/statistics/202871/number-of-fatalities-by-terrorist-attacks-worldwide/
https://seer.cancer.gov/statfacts/html/common.html
https://www.start.umd.edu/pubs/START_AmericanTerrorismDeaths_FactSheet_Nov2017.pdf
https://www.drugabuse.gov/drug-topics/trends-statistics/overdose-death-rates
https://www.americanprogress.org/issues/guns-crime/news/2019/11/20/477218/gun-violence-america-state-state-analysis/
https://www.defensenews.com/pentagon/2018/05/16/heres-how-much-the-us-has-spent-fighting-terrorism-since-911/
https://www.cancerhealth.com/article/trumps-2020-budget-plan-slashes-national-cancer-institute
https://youtu.be/L7xfS3LXSOk
https://youtu.be/-EghwCDNyiY

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 26 Septemba 2020 14:26

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu