Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah Itategemea Juu ya Kuonekana Mwezi Mwandamo kwa Kuanza na Kumalizika kwa Mfungo wa Ramadhan

(Imetafsiriwa)

Mnamo 3 April 2021, Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Pakistan, Fawad Chaudhry aliandika nukuu ya tweet “Mwezi wa Ramadhan utaonekana wazi jioni ya April 13 kwenye maeneo ya Lahore, Islamabad na Peshawar na katika miji mengine na funga itaanza April 14.”

Kwa nini Waziri wa Sayansi na Teknolojia amesema hivyo wakati nguzo ya Dini yetu, Saumu ya Ramadhan, inaamuliwa kwa kuonekana mwezi mwandamo na sio kutegemea mahesabu ya uwezekano wa kuonekana? Kwa nini Waziri amesema hivyo, wakati Mtume wetu Mpendwa (saw) amesema na kutuamuru,

إِنَّا أُمَّةٌ أُمِّيَّةٌ، لاَ نَكْتُبُ وَلاَ نَحْسُبُ الشَّهْرُ هَكَذَا وَهَكَذَا يَعْنِي مَرَّةً تِسْعَةً وَعِشْرِينَ، وَمَرَّةً ثَلاَثِينَ»

“Sisi ni watu tusiojua kusoma wala kuandika, hatuandiki wala hatuhesabu. Mwezi mara huwa hivi na mara huwa vile – yaani mara huwa ishirini na tisa na mara nyengine huwa thalathini.” (Bukhari). Hadithi hii tukufu, iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa Mtume wake (swt), inauzingatia mwezi mwandamo, ikiagiza kuwa zingatie kuonekana kwa mwezi na sio kwa uwezekano wa makisio ya kuonekana, ambayo ni makisio tu na yanaweza kuwa na makosa kwa namna nyingi, ikiwemo kuzibwa na mawingu na kufanya usionekane. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

 «صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ، وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ، فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلاَثِينَ»

“Fungeni kwa kuuona (mwezi wa Ramadhan), na fungueni kwa kuuona (mwezi wa Shawwal), na kama mawingu yametanda (hamuwezi kuuona), basi kamilisheni idadi ya siku thalathini za Sha’ban.” (Bukhari).

Ni lazima izingatiwe kuwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kila mwaka hufanya makosa juu ya mahesabu kwa Shaaban na hivyo kuwaongoza vibaya Waislamu wa Pakistan kuuangalia mwezi wa Ramadhan siku moja mbeleni. Ni lazima izingatiwa vile vile kuwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia inashabikia mgawanyiko wa utaifa na wa kimadhehebu kwa uelekezaji vibaya wa Siku ya Arafah, ambapo Waislamu hushuhudia Hijjah wazi wazi katika viwanja vya Arafah, lakini bado huongozwa vibaya juu ya kusherehekea Idi ya Kuchinja siku inayofuata.

Kwa nini taarifa kama hizi kutoka kwa wizara inayoelekeza vibaya ikiambatana na kampeni ya mitandaoni inayodhuru kwa siri ya kukebehi Wanachuoni wanaoheshimika, warithi wa Mitume (as), kudhoofisha Sunnah za Mtume (saw) na kuubeza Ummah kuwa ni wajinga kwa kushikilia Dini? Kwa hakika, tamko, «إِنَّا أُمَّةٌ أُمِّيَّةٌ» “Sisi ni watu tusiojua kusoma” halitutaki kuwa hivyo. Tulikuwa hatujasoma wakati huo kabla ya kuja Uislamu, kama Mwenyezi Mungu alivyosema,

(هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا)

“Yeye ndie aliyempeleka Mtume kwenye watu wasiojuwa kusoma.” [Al-Jumu’ah 62:2]. Neno ummi (kutojua kusoma na kuandika) linatokana na msingi mmoja na neno ummah. Linahusiana na yule asiyetafautishwa na watu wengine kwa kujua kusoma na kuandika. Linafanana na neno ‘ammi linalotumika kumuelezea mtu wa kawaida asiyetafautishwa nao kwa kuwa na elimu wasiokuwa nayo. Pia inasemwa kuwa katika lugha ya Kiarabu kuwa neno ummi linahusiana na neno umm (mama), kwa sababu hakujifunza zaidi ya mapajani mwa mama. Kwa hakika, Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa hivyo, wakati Watu wa Kitabu walikuwa na Vitabu vitakatifu vya kurejelea.

Maelezo yalikuwa kama Ummah ulivyokuwa kabla ya Uislamu na sio namna ulivyobakia. Imepokewa kuwa wakati Mtume (saw) alipomchagua mtu kuhudumia Zakah, Ibn al-Latabiyyah, alikuja kwake (saw), Yeye (saw) alikuwa akihesabu idadi jumla iliokusanywa. Alikuwa na waandishi kadhaa, kama Abu Bakar, Umar, Uthman, Ali na Zayd (ra) walioandika Wahyi, na walioandika mikataba na kuandika barua zake kwa watu ambao Mwenyezi Mungu (swt) amemleta kwao, kwa watawala juu ya ardhi kujisalimisha kwa mamlaka ya Dola ya Kiislamu. Yeye (saw) aliweka sharti la kikomboleo kwa mateka wa vita vya Badri kuwa ni kuwafundisha Waislamu kusoma. Kwa hakika, kama Ummah wa Kiislamu, Waislamu waliweka msingi wa sayansi na teknolojia ambayo Fawad Chaudhry hivi sasa anaitegemea, kama elimu ya trigonometria, aljebra na algorithmi, huku ukiongoza mataifa yote katika sayansi na teknolojia katika zama za Khilafah, katika baadhi ya nyakati ikiwa ni kwa karne kadhaa.

Na kwa wale wasiojiamini linapokuja suala la hadhara ya Wamagharibi hawazingatii Ukubwa wa Muumba wa mwezi na jua Mwenyezi Mungu (swt)? Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

 (هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ)

“Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu.” [Surah Yunus :5]? Wanadamu wangali kupotea na kukanyagwa katika kipindi fulani, lau kama haungepewa jua na mwezi na Mwenyezi Mungu (swt) kuamua tarehe na nyakati. Je, mizunguko ya dunia, mwezi na jua, pamoja na sura maalum za mwezi, sio alama za uwepo wa Al-Mudabbir, Mpangaji wa Mambo yote (swt)?

Basi Waislamu na wajifunge na maamrisho ya Mtume (saw) juu ya suala la uangaliaji wa mwezi. Na wachukue usaidizi kutokana na makisio yanayotarajiwa ya muonekano wa mwezi, lakini wasiyategemee. Na wafanye kazi juu ya kurejesha dola pekee ambayo ndio itahifadhi nguzo za Dini yao, Khilafah kwa Njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu