Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mtoto asiye na Mfumo wa Kifamilia yuko Hatarini kama ulivyo Hatarini Ummah usio na Mfumo wake wa Kutawala

(Imetafsiriwa)

Hakika dunia iko katika machafuko na machafuko haya yanajitokeza katika kila ngazi ya jamii, mojawapo ni maisha ya familia na kuvunjika kwake. Kama mtaalamu anayefanya kazi na vijana katika nchi za Magharibi, kufeli kwa jamii kwa jumla kunadhihirika zaidi katika faragha ya chumba changu cha utoaji ushauri.

Uchunguzi umegundua kuwa jinsi watoto wanavyouona ulimwengu huandaliwa kwanza kabisa na kile wanachopitia nyumbani, na kwamba jinsi wazazi wanavyounda familia zao inacheza dori muhimu katika ustawi wa vijana kwa jinsi wazazi wanavyo amiliana wao kwa kwao.

(H. Benson, Marriage foundation) Cha kusikitisha ni kwamba, matokeo ya kuvunjika kwa familia na matokeo yake hasi yote huathiri watoto wote, wakiwemo wale wanaotoka katika familia za Kiislamu. Vijana wa Kiislamu wanakabiliwa na changamoto za afya ya akili, kama vile wasiwasi, matatizo ya hisia, matatizo ya kula, matatizo ya kujirekebisha, na mawazo ya kujiua (Basit & Hamid, 2010). Pia, unyanyapaa unaozunguka maradhi ya akili na matibabu yake ndani ya jamii ya Kiislamu umekita mizizi sana. Hii inachangiwa na ukosefu wa uaminifu wa kitamaduni kwa mfumo wa afya ya akili wa Kimagharibi ambao umeegemezwa katika mtazamo tofauti wa maisha.

Kiuhalisia, hii ina maanisha kwamba vijana wa Kiislamu wakati mwingine hutembelea huduma za afya ya akili bila familia zao kujua na kwamba vijana hawa wanasitasita kushirikisha familia zao kwani mara nyingi wanahisi kwamba matatizo yao yanahusiana na mfumo wa familia zao. Matokeo yake ni kwamba mara nyingi unaweza tu kuzungumza na kijana mwenyewe kwani wanakataa kutoa ruhusa ya kuhusisha mfumo wa (familia). Kwa hivyo, bila ya chaguo jengine unajaribu kuwasaidia vijana hawa kukuza fahamu bora zaidi kuhusu wao wenyewe na ulimwengu unaowazunguka, kuwafundisha tabia ya kuwasaidia katika vipindi vigumu na kuwapa mbinu za kuendelea na kile walichojifunza.

Cha kusikitisha ni kwamba, unajua kwamba saa yako moja kwa wiki ni vigumu kupima maingiliano yao ya kila siku na familia zao zenye matatizo, shule au mazingira ya kazi na jamii zinazofeli wanazoishi ndani yake pamoja na matatizo yake mengi ya kijamii, kiakhlaqi na kiuchumi yanayowaathiri. Vijana hawa wanaishi katika jamii zinazoweka thamani na hadhi zaidi kwa kile mtu anachopata, anachoonekana  nacho na anachomiliki badala ya kuwa na tabia nzuri na yenye kusaidia. Jamii hizi huweka malengo ya maisha yasiyo ya kiuhalisia, ambapo vijana hufundishwa kupata idhini isiyo ya kweli na isiyo na maana ya wengine huku wakijazwa vichwa vyao mara kwa mara kupitia mitandao ya kijamii na taswira zisizo na dosari za jinsi maisha “yanapaswa kuwa.”

Kama tabibu unatumaini na kuomba kwamba mteja wako, bila matatizo mengi, bado atafanya maamuzi sahihi, kuwa na mwalimu mkarimu na muelewa, kukutana na rafiki mzuri na mwaminifu, kujiunga na kikundi cha halaqa chenye usaidizi katika msikitini na muhimu zaidi kupata mwanafamilia msaidizi wanayeweza kumwamini na kumtegemea na kuwasaidia zaidi.

Je, ni jinsi gani maisha ya familia yanavyokuwa muhimu unapokabiliwa na aina hizi za matatizo na je jinsi ilivyo muhimu kuweza kuhusisha mifumo ya familia ya vijana hawa. Je, sio lazima kwa kijana mwenye matatizo aweze kutegemea mfumo wake wa usaidizi anapokabiliwa na masuala ya afya ya akili badala ya kuwaacha wajitetee wenyewe katika jamii ambayo tayari ni sumu?

Uhalisia huu kwa hakika umenikumbusha hali ya ummah kwa jumla, kwani unawezaje kumsaidia kijana bila kuhusisha mfumo wake (wa familia). Ni mfumo wenye vipengele vyake vyote tofauti; k.m. wazazi, ndugu, babu na nyanya, mashangazi na wajomba, wapwa na binamu ambao wangeweza kumpa kijana usalama, msaada, makaazi, usuhuba, ushauri (uimarishaji mzuri) na mawasiliano wanayohitaji sana vijana hawa. Wazazi wanahitaji kutahadharishwa kuhusu mahangaiko na matatizo ya watoto wao na kwa pamoja kujaribu kutafuta njia za kuwasaidia. Ndio, familia zetu nyingi zina tabia ngumu na wakati mwingine zenye sumu lakini familia zote zina changamoto kwani pia zina nguvu na familia zote zina maeneo yenye uwezo wa ukuaji.

Na bado mfumo wa usaidizi wa Ummah wetu, mfumo ambao hauruhusiwi kuhusika katika kutatua matatizo yetu, Khilafah (mfumo wa utawala wa Kiislamu) kwa hakika hauna dosari yoyote kwani umeteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wetu. Unatokana na mfumo mpana wa imani ambao unaweza kutatua matatizo yote ya binadamu kwa njia bora zaidi. Ni mfumo utakaohakikisha maelewano, ustawi, usalama na haki kwa wote. Mwenyezi Mungu (swt) ametoa masuluhisho ya hekima Yake isiyo na kikomo kwa matatizo yote ya maisha na njia ya kuyaleta masuluhisho haya maishani ni kwa kupitia kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume itakayotabikisha imani, maadili, kanuni, sheria na mifumo yote ya Uislamu juu ya ardhi zetu za Kiislamu.

Bila ya kuhusishwa mfumo huu, sisi ni mithili ya kijana, tunakabiliwa na matatizo mengi na kutokuwa na uwezo wa kuhusisha mfumo wetu wa Kiislamu kunatufanya kuwa watuhumiwa kwa matatizo yote yanayotuzunguka.

[فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 123-124]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu