Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dori ya Kuisimamisha Dola ya Khilafah katika Mzozo wa Sasa wa Kimataifa juu ya Nani Ataitawala Dunia

(Imetafsiriwa)

Mizozo ya kimataifa imekuwepo muda wote wa historia ya mwanadamu na imeendelea kuwa mibaya zaidi katika muda wa sasa. Kila muda ukisonga, dunia hii ya kisasa inashuhudia mizozo ya kutisha zaidi katika historia ya mwanadamu, ikiuwa mamilioni ya watu katika hali ya kikatili kutokana na maendeleo ya silaha za kisasa, kutokana na vikwazo vikali vya kiuchumi vinavyowekwa na mataifa makubwa kwa mataifa dhaifu, na kutokana na kuanguka kwa viwango vya kimaadili kwa viongozi wa dunia.

Mienendo ya mzozo wa kimataifa chini ya mfumo wa dunia wa dola za kitaifa

Mizozo ya kimataifa kijumla hujulikana kuwa ni mizozo baina ya dola tofauti tofauti za kitaifa. Inaweza kugawika katika aina nyingi tafauti kwa kutegemea msingi wa sababu ya mzozo. Mtazamo makini wa hali ya sasa ya muundo wa dola za kitaifa unaonyesha kuwa kuna aina zifuatazo za mizozo:

Aina   

Sifa muhimu                                                       

Mfano

Kabila

Mzozo baina ya makabila mawili au zaidi yanayopambana

Rohingya

Dini

Kukosekana uvumilivu wa dini nyengine dhidi ya wafuasi wa dini nyengine

 Ghasia za (India) mwaka 2022

Mfumo

Msuguano baina ya makundi mawili yenye mifumo tafauti. Pia, imani ya kuwa jaribio la mtu fulani kubeba fikra ya kubadilisha hali ni tisho kwa mfumo uliopo.

 Uingereza dhidi ya Uthmaniya, Vita baridi, Uyghur-China

Mipaka

Misimamo inayozozana juu ya eneo la ardhi.

 Mzozo wa Kashmir, Kurdi-Uturuki, India-China, Yemen.

Serikali

Misimamo inayozozana baina ya serikali mbili katika taifa la kidemokrasia. Hii huibuka wakati serikali kuu sio sawa na serikali ya jimbo.                                                              

 Inapatikana katika kila nchi ya kidemokrasia. wanaRepublican dhidi ya wanaDemokrasia.

Uchumi

Kupigania rasilimali, au kutumia ala za kiuchumi kudhibiti uwezo wa taifa jengine.

 US na China, vikwazo vya EU dhidi ya Urusi.

Chimbuko la Mizozo

Kwenye kiini cha jambo hili kuna maradhi yaliojikita ya utaifa. Ni muhimu kwa hiyo, kufahamu uhusiano baina ya utaifa na mizozo, na kisha kufikia hitimisho kuhusu namna ya kushughulikia machafuko haya. Waheshimiwa miongoni mwa wenye fikra za utaifa na usekula wanaelewa wazi juu ya suala la kuwa utaifa ni fungamano ovu. Hebu tuangalie namna hawa waheshimiwa miongoni mwa umma wanavyouona utaifa katika muktadha wa India kama mfano: 

Ndio, hii ni mantiki ya Taifa. Haitosikiza sauti ya ukweli na wema. Itaendelea na ngoma yake ya mzunguko wa ufisadi, ikiunganisha chuma kimoja kwa chengine, na mashine moja kwa nyengine; ikikanyaga chini kwa kishindo maua yote ya kupendeza ya imani ya wazi na maadili bora ya maisha ya mwanadamu.” – Rabindranath, mtunzi wa wimbo wa Taifa la India

“Uzalendo hauwezi kuwa ni makaazi yetu ya mwisho ya kiroho. Sitonunua glasi kwa thamani ya almasi na sitoruhusu uzalendo kuushinda ubinadamu muda wote nitakaoishi.” – Rabindranath

“Muda wowote panapotokea mvutano wa kimaslahi baina ya nchi na wale wasioguswa, kwa uoni wangu, maslahi ya wasioguswa yanachukua nafasi dhidi ya maslahi ya nchi”. – Ambedkar, Baba wa katiba ya kisekula ya India.

“Mtu hutakiwa afe kwa ajili ya familia, familia hutakiwa ife kwa ajili ya kijiji, kijiji hutakiwa kife kwa ajili ya wilaya, wilaya hutakiwa ife kwa ajili ya jimbo, na jimbo hutakiwa life kwa ajili ya nchi, hata nchi pia hutakiwa ife, kama ni lazima, kwa manufaa ya dunia.” – Gandhi

Kama alivyoeleza Colin Flint, mtunzi wa “Introduction to Geopolitics”, - Dola ya kitaifa itakuwa nchi huru yenye kundi moja la watu wanaounda historia ya pamoja. Utaifa unasawazisha hisia ya pamoja ya kujifunga na taifa maalum na kuitumia kuhalalisha matendo ya kisiasa. Utaifa ni imani ya kuwa kila taifa lina haki ya kudhibiti eneo la mipaka. Kimsingi, kama kundi la watu wana hisia ya pamoja ya utaifa, hutengeneza “nchi.” Fikra ya utaifa inaamini kuwa kundi mara linapojitafsiri kuwa ni nchi huwa na “haki ya kimaumbile” ya ulazima kwa eneo ya kuishi na kulitawala. Kwa maana nyengine, utaifa ni imani kuwa nchi iwe na dola yake yenyewe … Watu wengi hutumia utaifa kuhalalisha migogoro, kwa kuwa kila nchi hupigana kwa ajili ya haki ya eneo lake kwa kuishi na kutawala … Jiografia ya kisiasa ya utaifa imepelekea mamilioni ya vifo kwa sababu ya watu kupigana kusimamisha dola kwa ajili ya taifa lao … Marekani imeendelea kutumia utaifa kama uhalali wa kuhifadhi eneo lao la sasa inalolishikilia …”

Wote hao wanajua kuhusu uovu wa utaifa lakini wamekuwa watu wa kidiplomasia zaidi wakati wanapouzungumzia katika mawanda huru. Wanauchukulia kama ni uovu wa lazima na kuidanganya dunia kuuchukua utaifa kwa moyo safi, kwa sababu tu ya kuweka mpango wa dola ya kitaifa uende sambamba na mabwana wa Kizungu. Muundo huu wa dola ya kitaifa umezaa hamu ya kudhibiti ubwana miongoni mwa wakubwa na hakuna gharama iliyo na ukubwa wa kutosha kuwazuia. Kiwango cha migogoro chini ya muundo wa dola ya kitaifa, katika upande wa maangamizi, ni makubwa mno, viwango vya vifo havifikiriki, na viwango vya maadili ya vita ni vya chini mno. Takwimu zinaeleza juu ya hayo:

- Mashambulizi ya Marekani kwenye miji ya Hiroshima-Nagasaki – Mabomu mawili yameua baina ya watu 129,000 na 226,000 – zaidi wakiwa ni raia wakiwemo watoto wachanga, Watoto wadogo, na wanawake.

- Mzozo wa Rohingya – Wazazi wa ki-Rohingya wapatao 43,000 wameripotiwa kupotea, wanadhaniwa kufariki. Kati yao, watoto 28,000 wamepoteza angalau mzazi mmoja. Watoto 7,700 wameripotiwa kupoteza wazazi wote wawili.

- Mzozo wa Uyghur – Baina ya mwaka 2015 na 2018, ukuaji wa watu hasa katika maeneo ya Uyghur ya Kashgar na Hotan ulishuka kwa kiwango cha kushangaza cha asilimia 84. Mnamo 2014, zaidi kidogo ya vifaa 200,000 vya Intra-Uterine (IUD) viliingizwa jimboni Xinjiang. Idadi hiyo iliongezeka kufikia takriban IUD 330,000 hadi 2018 – ongezeko la zaidi ya asilimia 60. Idadi hii mpya iliyo ndogo hata kwa jamii ya kisekula na kikomunisti.

- Syria dhidi ya Bashar al-Assad – Makadirio ya kiwango cha vifo ni baina ya 470,000 – 610,000. Shirika la ‘Human Rights Watch’ (HRW) linakisia kuwa angalau mashambulizi 85 ya kemikali yalitokea baina ya Agosti 21, 2013 na Feb 25, 2018, na serikali ya Syria ilikuwa muhusika wa mengi ya mashambulizi hayo. HRW imesema idadi halisi ya mashambulizi inakadiriwa kuwa kubwa zaidi ya 85. Kwa mujibu wa uchunguzi wa taasisi ya ‘Global Public Policy Institute’, angalau mashambulizi 336 yalifanyika.

- Vita vya Yemen: Inakisiwa vifo 377,000 vilitokea hadi mwishoni mwa 2021, ikihusisha wale waliouliwa kwa sababu za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Asilimia 70 ya waliouliwa ni watoto walio chini ya miaka mitano.

Waislamu na wasiokuwa Waislamu wameathirika ikiwa ni matokeo ya mizozo hii. Hata hivyo, maafa katika ulimwengu wa Kiislamu yamekuwa makubwa zaidi kwa sababu ya kutumika ardhi za Waislamu kama uwanja wa kupiganisha mapambano na mataifa makubwa yanayoshindana, na hamu yao ya kusimamisha changamoto mpya, kama ya Khilafah, kujitokeza tena. Kutokana na uoni wa kijumla, wagomvi watatu wanashiriki katika mizozo mingi ya kimataifa ya miongo michache iliyopita, ima moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja – Marekani, Urusi na China.

Uwezo wa nguvu baina ya Marekani, China na Urusi

Mfumo wa dunia wa Marekani uliofuatia kipindi cha vita baridi umeanza kufichua baadhi ya alama za dosari. Mataifa ya dunia hivi sasa yapo huru zaidi kuchagua washirika wao, bila pingamizi kubwa kutoka Marekani. Hata vibaraka bora zaidi wa Marekani kama familia ya Saudi hivi sasa ipo huru zaidi kuchagua washirika wake. India inaagiza mafuta kwa utulivu kutoka Urusi, licha ya wito wa viongozi wa Ukraine wa vikwazo kwa India, watunga sheria wa Marekani wameamua kutoiwekea vikwazo India, hali inayofichua nafasi yao hafifu ya kupatana katika siasa za kimataifa. Marekani pia ilibidi kukabiliana na aibu katika ngazi ya kimataifa kwa sababu ya kuipoteza Afghanistan kutoka kwa wapiganaji wachache wa msituni. Washirika wa Marekani wamesita kuiamini kama walivyokuwa mwanzoni na wanatafuta mabwana mbadala au washirika. Licha ya kuwa Marekani inamiliki mfumo wa sasa wa dunia kwa ubwana wake wa sarafu yake ya dolari, ikidhibiti kiasi cha kambi 750 katika nchi angalau 80 duniani kote, na ikiwa na matumizi ya kijeshi yasio na mfano yalio sawa na matumizi jumla ya nchi 10 zinazoifuatia.

Vitisho kutoka Urusi na China kwa Marekani, kiongozi wa sasa wa dunia, ni vya aina tafauti kabisa.

Urusi imekuwa ni taifa mchokozi wa kivita ikiwa na uchumi dhaifu kulinganisha na Marekani. Hata hivyo, kulituliza taifa linalopenda shari kijeshi lenye kigingi cha nyuklia inatoa kitisho kikubwa, hata kama taifa ni dhaifu na dogo kama Korea Kaskazini. Urusi zaidi ipo kama jitu kubwa linalotaka kuhifadhi nyumba yake kutokana na mfumo wa dunia ambao haiwezi kuutawala kwa sababu ya rai jumla hasi dhidi yake katika medani ya kimataifa.

China kwa upande wake, sio taifa chokozi kama Urusi.

Hatua zake ni zenye kupimika zaidi, ambazo zinaonekana wazi kutokana na namna walivyoweza kushikilia maeneo zaidi ya India na kushikilia udhibiti wake kwa Tibet na Hong Kong, na kuwa na ushawishi muhimu kwa Taiwan. China, kinyume na Urusi, ipo kimkakati zaidi katika kutanua misuli yake na kutanua maeneo yake. Wakati Urusi inajulikana zaidi kwa vita, majaribio ya mauaji, na kufanya udukuzi kwenye kampeni za uchaguzi za nchi za kigeni, China inajulikana kwa uundaji, biashara, teknolojia na uwekezaji, ambapo inaifanya kuwa ni mgombea anayefaa kwa kuongoza dunia kwa kutokuwepo Marekani. Uwezo wa kijeshi wa China umekuwa ukiongezeka na kuendelea kukua katika Mashariki ya Asia ikiwa na upinzani hafifu. India ambayo ni kibaraka wa Marekani haijaweza kutoa upinzani wowote wa maana kwa China, na inaendelea kupoteza baadhi ya maeneo yake.

Kujumuika kwa Khilafah kwenye mchanganyiko wa mataifa yenye nguvu

Suala la mpinzani mpya kuwa anazaliwa tena na kutoa changamoto juu ya hali ya sasa imekuwa ni jinamizi kubwa zaidi la Marekani. Urusi na China ni kitisho kilicho karibu zaidi, lakini Khilafah inaitishia Marekani hata kabla ya uwepo wake. Haishangazi kwa nini imetumia dolari trilioni 8 kwa ajili ya vita vyake dhidi ya ugaidi, ili tu kumuweka shujaa usingizini. Basi itakuwaje shujaa huyu akiamka?

Khilafah itaziunganisha nchi za Waislamu 57 kuwa dola moja yenye mfumo mmoja.

Hata kama itaunganisha mataifa 3 tu ya Waislamu, nguvu yake itakuwa haisemeki. Na hii sio kutia chumvi maneno kwa sababu mbili. Kwanza, Marekani haikuweza kuishinda Taliban iliyo na vifaa duni vya kivita, basi kwa vipi kwenye nchi iliyo imara kiuchumi, na iliyo na ujuzi wa teknolojia. Pili, Urusi na nguvu zake zote bado haijaweza kuikalia Ukraine, basi vipi itaweza kuipa changamoto dola ambayo siku ya mwanzo ya kuzaliwa kwake inatarajiwa kuwa na nguvu (angalau) mara 3 zaidi ya nguvu za Ukraine, na huenda ikawa mara 30 zaidi ya nguvu zake kuliko Ukraine ndani ya miezi 6.

Jeshi la Ukraine lina takriban wapiganaji 200,000, na askari wa akiba takriban 250,000. Idadi ya vifaru vya Ukraine: 953. Idadi ya ndege za kivita: 312. Haina silaha za nyuklia.

Jeshi la Pakistan lina takriban askari 654,000 na wapiganaji wa akiba 550,000 na Walinzi wa Taifa 185,000, walio tayari kutumika eneo lolote muda wowote. Idadi ya vifaru: 3742. Idadi ya ndege za kivita: 970. Inakisiwa kuwa na vichwa vya makombora 165.

Kama jeshi la Ukraine limeweza kutoa upinzani na kuipa wakati mgumu Urusi kwa kiasi hicho kidogo, basi nini Pakistan itaweza kufanya kwa Urusi? Na kama Pakistan, Afghanistan na Iran zitaungana chini ya dola ya Khilafah, nani atakayeweza kuitawala? Na kama ulimwengu wote wa Kiislamu utaungana chini ya dola ya Khilafah, basi nani atakayesubutu hata kuwaangalia Waislamu.

Sera za Khilafah – Maeneo ya umuhimu

Mara baada ya ukubwa wa uchumi na jeshi la dola ya Khilafah kujulikana, itakuwa rahisi kufahamu namna ya mfumo mpya wa dunia utakavyotawaliwa na dola ya Khilafah. Hata hivyo, kutawala huku siko kule kunakotokana na ulafi wa kujichukulia rasilimali, bali ni kutawala kwa namna ambayo ni lazima kwa ubebaji da’wah ya Uislamu, kuwahifadhi Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kueneza amani, kuzuia umwagikaji damu ulioanza kutokana na uanzishwaji wa nadharia ya dola ya kitaifa. Mukhtasari wa vipaumbele vya dola ya Khilafah vimewekwa hapo chini:

1) Khilafah itaikomboa Ardhi Takatifu. Abu Umamah (ra) ameeleza kuwa Mtume (saw) amesema: «لا تزالُ طائفةٌ من أُمَّتِي منصورينَ لا يَضُرُّهُمْ من خَذَلَهُمْ حتى تقومَ الساعةُ» “Halitoacha kundi katika Ummah wangu kunusuriwa, hatowadhuru yule atakayeacha kuwasaidia, hadi kisimame Kiyama”. Maswahaba wakauliza: “Watakuwa wapi hao, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Mtume (saw) akasema: «ببيت المقدس وأكناف بيت المقدس» “Baytul Muqaddas na maeneo yanayozunguka”.

2) Dola ya Khilafah italenga kuweka vizuizi mara moja dhidi ya wachokozi. Abdallah ibn Omar (ra) amesema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akifanya tawaf kuizunguka Al Ka’ba huku akisema kuiambia: «ما أطيبك وأطيب ريحك، ما أعظمك وأعظم حُرْمَتك. والذي نفس محمَّد بيده، لحُرْمَة المؤمن أعظم عند الله حرْمَة منكِ، ماله ودمه، وأن نظنَّ به إلَّا خيرًا» ‘Ni mzuri ulioje! Na mwenye harufu nzuri ilioje! Una ukubwa ulioje na ukubwa wa utukufu ulioje! Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi mwake, utukufu wa muumini na mali yake na damu yake ni mkubwa zaidi ya utukufu wako!’”

Khilafah itaendeleza uundaji wa silaha zenye nguvu zaidi za kutia hofu maadui ikiwemo za maangamizi ya watu wengi (WMD) ili kuwafanya viongozi waliopo duniani kufikiria mara mbili juu ya kufanya vita na taifa ambalo watu wake kifo kwao ni chenye kupendwa zaidi ya starehe za dunia. Khilafah haitovumilia uchokozi wowote dhidi ya Waislamu katika ardhi zake yenyewe au kwenye ardhi za kigeni.

3) Khilafah itaweka mfumo mpya wa dunia, mfumo wa dunia wa Kiislamu. Khilafah itajisalimisha kwa sheria za Mwenyezi Mungu na itaendesha dunia kwa utaratibu wake wenyewe kwa manufaa ya Waislamu pamoja na wasiokuwa Waislamu. Sheria za kimataifa hazitoifunga Khilafah. Khilafah haitoruhusu mataifa ya kigeni kuingilia sera zake na mikataba ya UN. Bali Khilafah itatekeleza mipango yake yenyewe katika anga ya kimataifa.

4) Khilafah itatoa ulinzi kwa walio dhaifu. Raia wasiokuwa Waislamu katika nchi isiyo ya Kiislamu wakihitaji msaada, itawasaidia kama ilivyowasaidia Wakristo wa Uhispania. Haki ni ya wote na itafika kwenye ardhi isiyo ya Waislamu mara moja. Kimsingi hii ina maana kuwa dhulma yoyote ya kijamii, kisiasa au kiuchumi itashughulikiwa na Khilafah. Kama dola ya dunia ikiitaka msaada dola ya Khilafah dhidi ya mchokozi, Khilafah itatoa ulinzi chini ya mikataba ya kisharia, ambapo itaweza kupata washirika huko mbeleni.

Kwa sera kama hizo madhubuti na imara zilizowekwa, Khilafah italeta amani kwa Ulimwengu wa Kiislamu na pia kwa uwanja wote wa kimataifa. Bila Khilafah, dola za kitaifa ni kama mbwa waliopotea wakibwekeana wao kwa wao. Khilafah itawadhibiti na kuwafanya wawe na nidhamu. Baada ya mataifa haya duni kufundishwa nidhamu, hakutakuwa tena na mzozo wa kibinadamu kama ule wa Rohingya au Syria au Yemen. Na hakutakuwa tena na hali kama ya Hiroshima au Iraq au Afghanistan.

Bila ya Khilafah, Ummah umekuwa ukihangaika kwa zaidi ya miaka mia moja sasa. Waislamu wamekuwa wakiteswa, kuuliwa, kupigwa mabomu, kuzamishwa, kupigwa risasi, kuhamishwa kwa muda wote wanaoweza kukumbuka. Waislamu hivi sasa wameshasahau mahali salama walipowahi kuwa hapo kabla. Waislamu wanahitaji kujihisi wapo salama, angalau kwa kipindi hiki kifupi bila kuwa na wasiwasi wa kitakachotokea kesho kwa familia zao, bila kuwa na wasiwasi kuhusu mtoto gani atakayekwenda kuchukuliwa na jeshi la umbile la Kiyahudi kesho, mtoto gani atakayeuliwa na genge la Hindutva kesho, msichana gani atakayebakwa na jeshi la China kesho, mtoto gani atakufa kesho kwa bomu la kemikali, msichana gani atakayeuzwa katika makambi ya Rohingya nchini Bangladesh kesho. Mateso ya vijana na wasichana wa Ummah yakome, na itakuwa ni Khilafah inayosubiriwa kwa kipindi kirefu itakayokomesha maumivu na mateso haya. Na Ummah utajitahidi kuiregesha tena Khilafah bila kujali namna jitihada kubwa za mataifa makubwa hivi sasa za kujaribu kuukandamiza ulinganizi huu.

Haya ni majaaliwa yasiyo epukika ya mfumo wa dunia na mataifa makubwa hayawezi kufanya chochote juu ya hili. Ummah hautosahau abadan. Umehifadhi kila chembe ya mateso yaliyowakumba vijana wetu na wasichana wetu kutoka kwa mataifa haya makubwa yenye nguvu.

«ثم تكون خلافة على منهاج النبوة» “...Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” - Mtume Muhammad (saw)

Ama kwa Waislamu kupitia maumivu haya walio nayo, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ]

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliowajia wale waliopita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja nae wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu”. [2:214].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Hassan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu