Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Umwagaji damu wa Hivi Punde huko Jenin, Palestina

(Imetafsiriwa)

Mkutano wa dharura ulifanywa na kamati ya Mamlaka ya Palestina inayoongozwa na Nabil Abu Rudeineh ambaye alilaani mauaji ya umbile vamizi la kimabavu na mauaji na uvamizi wake dhidi ya Jenin. Kamati hiyo ilitoa wito wa upinzani wa amani wa umma na kutangaza kusitishwa kwa juhudi zote za uratibu wa usalama kati ya umbile hilo vamizi na Mamlaka ya Palestina. Pia ilitoa wito wa mwelekeo wa haraka kwa Baraza la Usalama na ICC (Palestine TV, Januari 26, 2023)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atasafiri kuelekea Misri, 'Israel' na Ukingo wa Magharibi wikendi hii, Wizara ya Mambo ya Nje ilitangaza Alhamisi, huku Marekani ikieleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ghasia baada ya operesheni moja mbaya zaidi ya 'Israel' katika Ukingo wa Magharibi katika kipindi cha miongo miwili. Ziara ya Blinken huko ‘Israel’ imepangwa kwa wiki kadhaa lakini uvamizi wa Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Ukingo wa Magharibi mapema Alhamisi ambao Wapalestina wanasema iliua watu tisa, akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 61, kuna uwezekano mkubwa utatawala mazungumzo yake jijini Jerusalem na Ramallah. Jeshi la Israel pia lilimpiga risasi na kumuua Mpalestina mmoja mwenye umri wa miaka 22 baadaye siku hiyo. (Washington Post, Januari 26, 2023)

Thamani ya damu ya Wapalestina imekuwa nafuu... inamwagika kirahisi, inakiukwa kirahisi, inadharauliwa kirahisi, inapuuzwa kirahisi na kudunishwa. Watu 9 waliuawa akiwemo bikizee mmoja na 4 wakiwa katika hali mbaya na makumi ya wengine kujeruhiwa katika umwagaji damu leo katika kambi ya Jenin. Kuongeza idadi ya Mashahidi hadi 30 katika mwezi huu pekee. Jeshi la umbile la Kiyahudi lilifyatua mabomu ya machozi katika hospitali na kuvamia na kuteketeza moto nyumba kadhaa katika mauaji ya leo. Vifaru vya IDF vilisagasaga magari barabarani huku gari moja likiwa na mtu ndani!

Shabak wakiwa katika jopokazi lao la operesheni maalum walivamia kambi ya Jenin mchana kweupe walikuja Jenin wakiwa chini ya ulinzi wa "Jeshi la Ulinzi la Israel" walishambulia nyumba za Wapalestina na kuzichoma moto hadi kuwa jibu wakilenga watu maalum.

Mauaji bila ya uwajibikaji wa watawala wa Kiislamu na hata jumuiya ya kimataifa ambayo inaweka kichwa chake mchangani wakati Palestina inashambuliwa vikali.

Je, kuna umuhimu gani wa kulaani kwa Mamlaka ya Palestina na Wizara yake ya Afya?

Je, ni mwitiko gani unaotarajiwa kutoka kwa mahakama za kimataifa za jinai?!

Umma umeghadhabishwa, shule zimegoma kupinga ukatili huo, maduka na wizara kufungwa, maandamano makubwa yalitokea katika miji mikuu ya Palestina.

Lau ingekuwa ni juu ya watu wa Palestina, wangekabiliana na vikosi vya uvamizi vifua wazi wakiwa na ngao ya ushujaa pekee. Ni nani anayeufunga minyoror Ummah wetu kutokana na kulipiza kisasi hiki ikiwa si kwa ufuatiliaji wa kijasusi, macho na masikio ya tawala za kihalifu katili? Hakika wao si wa aina yetu licha ya majina na sura zao, ni katika wanafiki na wasaliti na vibaraka.

Kusisitizwa kukatishwa tamaa kutoka kwa tawala za Kiarabu na nchi zengine za Kiislamu ambazo zinamiliki njia muhimu za kutokomeza umbile hili la umwagaji damu linalokalia kimabavu, lakini wito huo ni wa kweli kutoka kwa watu wa Palestina, wito wa ukombozi lazima utimizwe na wale wenye ikhlasi miongoni mwa majeshi ya Waislamu. Na sio kutoka kwa mithili ya Waziri wa Marekani Blinken ambaye anakuja kuzima hali ya kuenea kwa mzozo katika Ukingo wa Magharibi akitoa wito kwa Mamlaka ya Palestina kuhakikisha utulivu juu ya Wapalestina. Licha ya machafuko na lugha ya kisiasa juhudi zote hizi ni kudumisha hali halisi iliyokuwepo hapo awali na kuhakikisha hali ya umma haivuki mipaka, jambo ambalo Amerika haiko tayari kukabiliana nayo kwa sasa. Mavuguvugu ya Wapalestina na makundi ya Jihad yanaweza kushindwa na shinikizo la umma kulipiza kisasi mauaji ya Jenin ikiwa PA na Wamarekani hawatazima hasira zao.

Hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote, dola ya Khilafah ni takwa la dharura la watu kukomesha mashambulizi ya wazi dhidi ya Umma wa Kiislamu na kuangamiza kabisa umbile saratani ndani ya Ardhi Iliyobarikiwa, na hivyo kuwaruhusu kina mama kumaliza maombolezi yao ya watoto wao kwa mauaji ya kikatili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah #TurudisheniKhilafah
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
أقيموا_الخلافة# كيف_تقام_الخلافة#
#YenidenHilafet #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu