Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

“Hatuwezi Kuishi bila Mfumo wa Sasa wa Ulimwengu”

(Imetafsiriwa)

Imani kwamba hatuwezi kuishi bila mfumo wa sasa wa ulimwengu labda ndio kikwazo kikubwa kwa usalama wa watu wa Palestina. Iwe kwa kujua, au kutojua, imani hii inaonekana kushikiliwa na watu kote ulimwenguni huku wakiendelea kujaribu kutumia njia za kidemokrasia kuwasaidia watu wa Palestina, licha ya ukweli kwamba wamewafelisha watu kote ulimwenguni.

Huu ni utambuzi ambao tunauelekea tunapokataa suluhisho la dola mbili. Lakini tunahitaji kuvuka hili kuelekea kufahamu kwamba hatuwezi tu kuishi bali kustawi, ikiwa tutakataa mfumo wa sasa wa ulimwengu na kusimamisha tena Uislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu.

‘Ikiwa tutakataa mfumo huu, dola zengine za kitaifa zitatutenga’

Hiki ni kikwazo ambacho kinarudiwa rudiwa na wafuasi wa mfumo huu - tunawezaje kubadilisha mfumo? Hatuwezi kuishi bila mfumo wa kimataifa na faida zote ambazo utandawazi unatupa.

Lakini hebu tufanye tathmini hili kwa muda. Tunapoangalia jinsi uchumi unavyofanya kazi, angazo lake liko kwenye jambo moja mahususi - kuhakikisha kuwa nchi kote ulimwenguni zinautegemea. Ikiwa tutakuza viwanda vyetu, lazima viwe ni viwanda vinavyoshajiisha biashara, kunufaisha mfumo wa kimataifa. Ikiwa tunataka kuimarisha sarafu yetu, ni lazima tutafute njia ya kuleta dolari zaidi nchini kupitia biashara hiyo hiyo, au kupitia kurekebisha sera zetu na mazingira ya ndani ili ziweze kufaa kwa uwekezaji wa kimataifa.

Lakini hii ina maanisha nini? Inamaanisha kuwa uchumi wetu unaweza kufanya kazi tu ikiwa sisi ni sehemu yake, na kwa hivyo tunategemea, ulimwengu wote. Inamaanisha rasilimali zetu zinamilikiwa na, au zinaweza kutumiwa na ulimwengu wote. Dunia ambayo inatunyonya ili iweze kuhakikisha kwamba mfuo wa sasa unaendelea kustawi.

Fikra za kujitosheleza wenyewe zinasifiwa kuwa zimepitwa na wakati, au haziwezekani kufikiwa. Lakini jambo hilo lisilowezekana lipo tu ikiwa tutaendelea kutii sheria na kanuni za mfumo wa kimataifa wa sasa. Na tunapofanya hivyo, tumekwama kwenye kitanzi ambacho kitatudhuru tu.

Kwa hiyo, kwa nini tusijitahidi kukata kitanzi hiki? Kwa sababu ulimwengu wote utatutenga? Kwa hiyo? Kitu pekee ambacho tutapoteza ni manufaa ya kimada yanayodhaniwa ya 'chaguo' katika bidhaa tunazotumia na bidhaa ambazo tunaweza kuzipata. Tutakachopata ni umiliki wetu pekee wa rasilimali zetu, ambao utaturuhusu kujiendeleza, kustawi na muhimu zaidi, kufanya maamuzi yetu ya sera. Maamuzi ya sera ambayo yataturuhusu kupeleka majeshi Palestina na kuikomboa kutokana na ukandamizaji wa umbile la Kiyahudi.

Ikiwa tunaogopa kutengwa, tunahitaji tu kukumbuka kuwa kutengwa kunapatikana tu ndani ya mfumo huu - mfumo ambao kwa kweli ulichora mistari katika ramani ya ulimwengu katika jaribio la kuhakikisha kuwa Waislamu wanatenganishwa kwa msingi wa migawanyiko iliyokuwepo kama matokeo ya ukoloni na sera zake za ‘gawanya utawale’.

Kwa hivyo, kwa wale ambao wana wasiwasi juu ya kutengwa - chukua muda kukaa chini na kutazama ramani na ufikirie ni nchi ngapi ambazo zimeshikamana na Uislamu, zamani na sasa, na kisha fikiria jinsi itakuwa wakati tumeungana kwa mara nyengine tena.

‘Hatuwezi kuungana, kuna migawanyiko mingi sana ndani ya Ummah’

Je, hali ya Palestina haijaonyesha kwamba sisi ni wamoja? Waislamu kote ulimwenguni wametoa wito wa kupinga ukatili unaofanywa huko Palestina, na kuweka wazi kwamba sisi ni Ummah mmoja. Tunakosa tu uongozi wa kufanya mawazo yetu, hisia zetu na kushikamana kwetu na Dini ya Mwenyezi Mungu kuwa uhalisia.

Ukosefu wa umoja upo tu kwa sababu tunaishi katika mfumo ambao umetugawanya katika dola za kitaifa na kututenganisha na mistari na mipaka iliyoundwa na mwanadamu.

“Hakuna 'Ulimwengu wa Kiislamu', kama vile hakuna 'Ulimwengu wa Kikristo'. Waislamu ni kundi la watu tofauti  tofauti wanaoishi katika muktadha tofauti tofauti wenye historia na mifumo tofauti ya kisiasa. Kigawanyo (Ulimwengu wa Kiislamu) kinapunguza na kulisha watu wenye ubaguzi wa rangi. Hakuna chochote katika historia ya hivi majuzi ambacho kimefichua ubatili wa aina hii kama vile mauaji ya halaiki huko Palestina. Serikali za nchi zenye Waislamu wengi hazina misimamo ya pamoja na wala kimsingi hazijakuwa watetezi wa sababu ya watu wa Palestina.” Nukuu ya Nida Kirmani, Profesa Mshiriki (Sosholojia) katika LUMS Pakistan.

Wazo hili ni sahihi tu tunapoishi katika ulimwengu unaotetea utaifa, tukiwa na serikali zinazotetea maadili haya kama njia ya kudumisha mamlaka yao ndani ya mfumo wa sasa. ‘Ulimwengu wa Kiislamu’ upo; uko katika fikra na hisia za Umma wa Kiislamu. Lakini nguvu zake hazitapatikana isipokuwa tuukatae mfumo wa Kibepari, na wazo lake kwamba sisi ni ‘watu wa aina mbalimbali wanaoishi katika mazingira tofauti tofauti yenye historia na mifumo mbalimbali ya kisiasa’. Wazo ambalo ni ufafanuzi kamili wa migawanyiko kulingana na kitambulisho cha utaifa. Kama Waislamu, tukiwa na dola ya Kiislamu inayotutawala, vitambulisho vyote hivi vya utaifa vitakuwa visivyo na maana kwani sheria za Mwenyezi Mungu zinatuunganisha, kwa mara nyingine tena.

“Hata tukikataa mfumo huu, hatutafanikiwa kamwe - Marekani na washirika wake wana nguvu sana”

Tunaogopa madhara ya kuukataa mfumo huu, na kuondoa uungaji mkono wetu kutoka kwa Marekani na washirika wake, bila kutambua jinsi wanavyotegemea katika ushirikiano wetu, na ni kiasi gani wana wasiwasi kuhusu kusimamishwa upya kwa Khilafah.

Walifanya kazi bila kuchoka kufahamu fikra zetu wakati wa Khilafah, ili waweze kuzivunja na kuzipotosha, waliposhiindwa kutushinda kwa njia ya vita. Basi wakatugawanya katika mataifa, na wakazusha mifarakano baina yetu, ili watushinde. Wanaogopa wakati ambapo tutavuka tofauti hizi na kukumbuka kwamba sisi ni Ummah mmoja, na kukataa kukubali serikali ya Kibepari ambayo inajaribu kutuambia vyenginevyo.

Wanachotegemea ni ushirikiano wa watawala wetu kuimarisha madaraka yao. Watawala ambao wameruhusu Marekani kuingia kwenye anga juu ya ardhi za Waislamu, kutumia kambi za kijeshi na kushawishi maamuzi yetu ya sera.

Marekani ina kambi 750 za Marekani katika baadhi ya nchi na makoloni 80 kote duniani. Kambi hizi zilipeanwa na watawala wetu wasaliti, na ni muhimu kwa Marekani kuzishikilia ardhi yetu.

“Mbali na kambi zinazoweza kuwa tisa za Marekani nchini Ufilipino, Marekani tayari ina, kwa hesabu ya Pentagon yenyewe, kambi 313 za kijeshi za Marekani katika Asia Mashariki pekee.”

“Jeshi la Marekani kwa sasa linatumia anga ya Pakistan kufika Afghanistan kama sehemu ya juhudi zinazoendelea za kukusanya taarifa za kijasusi ... Linaendesha operesheni zake za juu-juu kutoka kambi za Mashariki ya Kati, na kulazimisha droni kuruka kutoka kambi za mbali, kama zile za Qatar na Imarati, karibu na Iran na kupitia anga ya Pakistan kabla ya kufika Afghanistan.(Chanzo)

“Marekani inadumisha kambi mbili katika Asia ya Kati, moja katika Uzbekistan na Kyrgyzstan. Wanakodisha kambi hizo bila malipo, lakini lazima walipie gharama ya usalama wa kambi hizo, mafuta ya ndege, na gharama zengine (Uzbekistan inashikilia kuwa inadaiwa ada za kutua na gharama zengine na Marekani kwa gharama ya kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na matumizi makubwa ya ndege za usafiri). Serikali ya Uzbekistan pia inapokea takriban dolari milioni 150 za vifurushi vya misaada ya kila mwaka, pamoja na mafunzo ya kukabiliana na ugaidi, kijasusi na utekelezaji wa sheria kutoka kwa mashirika ya serikali ya Marekani. (Chanzo)

Lakini, chini ya Khilafah, Khalifa kamwe hatakubali hili.

Kwa hakika ni haramu kwake kufanya hivyo.

“Dola ambazo hatuna mikataba nazo, dola za kikoloni, kama vile Uingereza, Marekani na Ufaransa, na zile dola ambazo zina matamanio katika ardhi zetu, kama Urusi, zinachukuliwa kuwa uwezo wa kuwa za kivita. Tahadhari zote lazima zichukuliwe dhidi yao na hairuhusiwi kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia nazo. Raia wao wanaweza kuingia katika Dola tu na pasipoti, na visa maalum kwa kila mtu binafsi na kwa kila safari.

Ama dola ambazo kwa kivitendo ni dola za kivita, kama vile Israel, hali ya vita lazima ichukuliwe kama msingi wa mitazamo yote nazo. Lazima ziamiliwe kana kwamba kuna vita halisi kati yetu, iwe wakati wa kusitisha mapigano au vyenginevyo. Raia wote wa dola kama hizi wanazuiwa kuingia katika Dola.”

Katiba ya Dola ya Kiislamu (Ibara ya 184)

Katika hali hii, Marekani itakuwa na nguvu gani juu yetu? Hawatakuwa na ufikiaji wa ardhi zetu, rasilimali zetu, anga yetu. Wao ni taifa la kisiwani - kwa hivyo, wangewezaje kufikia ardhi za Kiislamu? Wangetudhibiti vipi? Kupitia dolari? Naam, tutakataa hilo - haina thamani halisi, hata hivyo. Na kukataa kwetu kutapunguza thamani yoyote inayoonekana kuwa nayo.

Tutakataa sheria zao, biashara zao, tutaondoa makampuni yao ya kimataifa. Kimsingi, kuondoa mamlaka yoyote na yote ambayo Marekani, na washirika wake, wanayo juu yetu. Kwa hivyo, ushawishi wao juu ya sera yetu - kiuchumi, kisiasa na kijeshi- utatoweka. Na kisha, wataweza kufanya nini? Fikiria kuhusu hili – fikiria sana kuhusu hili – na uangalie ramani kama unapofikiria.

Ikiwa tutazingatia bara la Asia - sehemu kubwa yake ni ardhi ya Waislamu, na migawanyiko ambayo ipo tu chini ya mfumo wa sasa. Pakistan, Bangladesh, Afghanistan, Iran, Iraq, Uzbekistan, Tajikistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Azerbaijan, Turkmenistan. Nchi hizi kisha zinaungana na zile za Mashariki ya Kati - Kuwait, Bahrain, Qatar, Oman, UAE, Saudi Arabia Jordan, Syria, Lebanon, Uturuki na Palestina. Ambayo kisha zinaungana na ardhi za Waislamu barani Afrika - ikiwa ni pamoja na Misri.

Lau tutasimamisha Khilafah katika mojawapo ya nchi hizi, itaenea hadi nyengine. Na hii itaifanya kuwa nguvu ya kuzingatiwa. Marekani, na washirika wake wengine wa Kibepari, wanajua hili. Na ndio maana wanadumisha uwepo katika nchi hizi, wakieneza vita na mizozo ili kuyumbisha eneo hilo na kutusukuma katika hali ambayo tunaamini kuwa kamwe hatutashinda.

Hadi tutakapokubali hili, na kuvuka hali ya sasa na kuingia katika hali bora zaidi, ndugu na dada zetu Waislamu huko Palestina wataendelea kuteseka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu