Jumapili, 05 Rajab 1446 | 2025/01/05
Saa hii ni: 16:15:22 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utaifa Ndio Msukumo wa Mgawanyiko wa Umwagikaji Damu katika Ardhi za Waislamu

Yaliyotokea Srebrenica kipindi cha vita vya Bosnia, yaliyopelekea kuibuka kwa msamiati wa kisiasa wa "Balkanization", lilikuwa ni doa jeusi katika historia ya siasa za kileo. Uharamishaji wa uongozi wa serikali za Kikomunisti-Ujamaa uliathiri siasa za ndani za Yugoslavia mwanzoni mwa miaka ya tisiini. Yugoslavia kisha iligawanywa kuwa nchi nyingi: Slovenia, Croatia, Bosnia and Herzegovina, Serbia, Montenegro, na Macedonia. Wapinzani wa serikali hii ya ujamaa waliita wimbi la uingizaji demokrasia kwani ilimaliza utawala wa serikali ya kikomunisti nchini Yugoslavia. Kwa bahati mbaya, wimbi hili pia lilichochea ari ya utaifa kwa msingi wa ukabila na dini. Matokeo yake, neno Balkanization sasa linajulikana vyema zaidi kuwa ni neno baya la siasa ya eneo ambalo ni sawa na kuvunjika kwa eneo moja. 

Waislamu walilazimika kulipia gharama kubwa mno ya ugawanyaji huu wa Balkan. Vita vya miaka 3 vya Bosnia, kuanzia 1992 hadi 1995, vilishuhudia mauwaji ya kimbari ya Waislamu (soma: vita vya halaiki) kutoka katika mamia ya miji na vijiji. Mbali na historia ndefu nyeusi ya vita vya Bosnia, makala haya yataangazia zaidi juu ya fahamu ya utaifa wa umwagikaji damu ambao ndio kichocheo kikuu cha kuzigawanya ardhi za Waislamu pamoja na sababu ya kupotea kwa maisha ya maelfu ya Waislamu nchini Bosnia. Ni fahamu hii ndio iliyomshajiisha kiongozi wa Serbia Slobodan Milosevic kumaliza kabila la Waislamu wa Bosnia, kwa sababu alitaka kuunda ruwaza yao ya kitaifa ya Serbia Kuu, kwa eneo la Serbia lililosafi kikabila pambizoni mwa Mto Drina.

Fikra hatari na yenye sumu ya utaifa iliyo milikiwa na Milosevic haiwezi kutenganishwa na mizizi ya kihistoria ya utaifa wenyewe. Mizizi yake iko katika ubwana wa Westphalian (mkoa wa Ujerumani), iliyo undwa na mataifa ya Kikristo ya Ulaya yaliyo kuwa yakipigana mnamo 1648 na kujitokeza fahamu ya dola ya kieneo. Kuendelea kwake kulikoma katika karne ya 19. Fikra ya utaifa hukadiria dola halali kuwa inahusiana na taifa, ambalo ni kabila maalum au mkusanyiko wa makabila au watu waliojifunga na mipaka fulani ya kijografia.

Utaifa, hivyo basi, hauna mizizi ya kihistoria katika hadhara ya Kiislamu. Tunapo angali kwa karibu muda wa kihistoria, utaifa ulikuwa ni uhalisia mpya ulio lazimishwa juu ya uchoraji ramani wa eneo la ulimwengu wa Kiislamu. Kwa mujibu wa mtafiti wa hadhara ya Kiislamu kutoka Indonesia, Prof. Ajid Thohir, utaifa ulizaliwa katika ardhi za Waislamu kama natija ya maslahi ya kibepari na ya kikoloni katika karne ya 18 hadi mwanzoni mwa karne ya 20. Kwa bahati mbaya, umekuuza kwa njia isiyo ya moja kwa moja hisia ya mfarakano wa kisiasa miongoni mwa Waislamu.

Kihakika, katika karne ya 8 hadi karne ya 18, Ummah wa Kiislamu mwanzoni ulikuwa ni watu walio na umoja wenye uongozi na kitovu cha serikali chini ya nidhamu moja ya Khilafah (dola kuu). Tangu kuzaliwa kwake pamoja na risala ya Muhammad (saw), Waislamu waliishi kama Ummah mmoja, sio tu wakiwa wameunganishwa na Aqeedah (itikadi) moja pekee bali pia chini ya mfumo mmoja wa maisha. Leo, wakiwa na idadi ya zaidi ya milioni 1, Waislamu wanaishi kwa mfarakano katika maeneo yao ya kitaifa, wakiendesha serikali zao zilizo gawanyika, wakitekeleza hukmu zao za kidini juu ya matatizo katika mazingira yao ya mgawanyiko. 

Tangu mwanzoni mwa karne ya 20, Waislamu wamepitia mchakato wa "Balkanization" kiulimwengu chini ya pazia la utaifa na mvutano wa kutaka uhuru wa kujitawala. Pamoja na uondoaji ukoloni ambapo ilizalisha nchi mpya nyingi kwa jina la uhuru kutoka katika ukoloni wa Kimagharibi, ulimwengu wa Kiislamu uligawanywa na kuwa dola za kitaifa zaidi ya hamsini. Lakini huo sio mwisho wa hadithi. Ummah wa Kiislamu ulitumbukia ndani ya mtego wa udhibiti mpya wa Kimagharibi. Nchi za Waislamu tangu wakati huo zimekuwa zinaishi katika mfumo wa dola za kitaifa za kisekula, zilizo gubikwa na udhibiti wa Urasilimali na kujazwa kwa miito ya demokrasia na haki za kibinadamu. 

Kinaya ni kuwa, hatma ya Waislamu iko mbali na maendeleo, hadhi na ufanisi. Takriban Waislamu 12.5 milioni wameuwawa katika vita vingi katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, kwa mujibu wa msomi Refik Turan, kinara wa Jumuiya ya Kihistoria ya Kituruki, aliye sema katika kongamano la 2018 jijini Istanbul, "Hili takriban linafafanua hasara katika Vita vya Dunia." Tarakimu hizi hazijumuishi Waislamu wanaoteswa hadi kufa na Mabudha nchini Myanmar na mikononi mwa Wachina wa Xinjiang. Zaidi ya hayo, mamilioni ya Waislamu wanaokufa kutokana na njaa, maradhi, uhamiaji, na majanga mengine yanayo sababishwa na wanadamu hawamo ndani ya orodha hiyo.

Mipaka ya dola za kitaifa pia imewafanya Waislamu wa Rohingya kutengwa na ndugu zao Waislamu wa Bangladesh, Malaysia, na Indonesia. Hili pia liliwatokea Waislamu wa Uyghur waliokuwa wakiteseka chini ya dhalimu wa Kichina na kutelekezwa na watawala wa Waislamu kutokana na kuyapa kipaumbele maslahi yao ya kiuchumi ya kitaifa. Hawa hawajumuishi maelfu ya wakimbizi Waislamu wasio na makaazi waliofurushwa kutoka Syria, Iraq, na Palestina. Hii ndio gharama kubwa ya kulipia ukosefu wa umoja na mgawanyiko wa Ummah huu.

Hakika, Uislamu unashutumu vikali na kuharamisha uasabaiyyah, ikiwemo utaifa, kutabanniwa kama kitambulisho cha Waislamu, badala ya fungamano la udugu wa Kiislamu (ukhuwah Islamiyah). Mwenyezi Mungu anasema:

 [إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]

“Hakika Waumini ni ndugu…” (Surah al-Hujurat [49]: 10). Uislamu unatufunza kuwa fungamano imara zaidi kwa Muislamu ni Itikadi ya Kiislamu inayojitokeza katika ukhuwah Islamiyah. Hivyo, fungamano hili ni lazima liwekwe juu ya kabila, jinsia, au rangi. Mtume sallallaahu ‘alayhi wa sallam amesema, 

«أَوْثَقُ عُرَى الْإِيمَانِ: الْمُوَالَاةُ فِي اللَّهِ، وَالْمُعَادَاةُ فِي اللَّهِ، وَالْحُبُّ فِي اللَّهِ، وَالْبُغْضُ فِي اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ»

“Fungamano imara zaidi ni imani: Utiifu ni kwa Mwenyezi Mungu, na uadui ni kwa ajili Mwenyezi Mungu, na mapenzi ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuchukia ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu.” [Imesimuliwa na Ahmad]

Pindi Wamagharibi walipojua siri hii ya nguvu ya Ummah wa Kiislamu, walitia juhudi zao kuivunja na kuimaliza, au angaa kuudhoofisha msingi wa al-Walaa’wal-Bara’ah (Utiifu na upingaji) katika mwili wa Waislamu. Walikuwa wametabanni fikra ya "utaifa" ili kupata lengo lao ovu. Kutokana na haya, uhalisia mbaya ambao Waislamu ni lazima wakabiliwe nao na kuupitia ni ukosefu wa fahamu ya al-Walaa’wal-Bara’ah katika nyoyo za vizazi mtawalia. Utiifu wao kwa Uislamu umekuwa ukififia kidogo kidogo, na hatimaye kumalizwa na fahamu potofu.

Matendo na mivutano yoyote inayo fanywa na Ummah wa Kiislamu hayakuwa tena kwa manufaa ya Uislamu, wala kwa ajili ya kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu (Tawheed) juu ya ardhi hii. Imani kuwa Uislamu ni rehma kwa viumbe wote imetingishwa. Wamekuwa hawako tayari kutabanni maadili na mafunzo ya Kiislamu ili kufanikiwa ulimwenguni na kuendeleza umma.

Zama za nyuma, Uislamu uliuonya Ummah wake kutotumbukia ndani ya aina hii ya ufahamu mpotofu, kwa sababu utaifa umeorodheshwa kama fahamu ya kijahiliya kwa mtazamo wa Uislamu. Katika mojawapo ya Hadith, Mtume (saw) amekemea vikali wanaopigia debe asabiyya kuwa ni watu wajinga:  

«وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً فَقُتِلَ فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ»

“Na yeyote anayepigana chini ya bendera ya upofu kwa ajili ya uasabiya au akalingania uasabiya au akanusuru kwa ajili ya uasabiya kisha akauwawa, kifo chake ni cha kijahiliya.”[Imesimuliwa na Muslim]

Uharamu huu mkali unafafanuliwa zaidi na Shaykh Muhammad Said Al-Qahthani kwa kusema: "Kuwa Utaifa ni aina ya shirk kwa sababu humhitaji mtu kupigana kwa ajili yake, na kulichukia kundi jengine linalokuwa adui yake – bila ya kujali kuwa ni Waislamu au la -, hivyo basi kwa njia isiyo ya moja kwa moja ameufanya kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu (swt)."

Muhammad Qutb hata ameiweka fikra ya utaifa sambamba na mifumo potofu mengineo kama ukomunisti, usekula, na demokrasia, ambayo ni kinyume na Aqeedah ya Kiislamu na huenda ikaharibu Uislamu wa mtu. Alifafanua kuwa fikra hii huwafunza wafuasi wake kutenganisha Uislamu na maisha yao. Rai yake haitofautiani sana na ya A'la al Maududi, mwanachuoni wa Kipakistan, katika mojawapo ya maandishi yake. Alipinga uoanishaji wa Uislamu na fikra ya utaifa. Hakumkubali yeyote anayejidai kuwa ni Muislamu mtaifa, kwa sababu Uislamu wala utaifa kamwe haviwezi kuwa sambamba.

Utaifa umewagawanya, kuwadhoofisha, na kuwafanya mayatima Waislamu kwa kupoteza mlinzi wao, na kuwafanya kuwa windo ambalo hatma yake iko katika rehma ya wawindaji wafujaji ambao wamekuwa wakiwanyakua mmoja mmoja kila usiku. Tafakari kuwa mnamo 1995 pekee, tulipoteza maisha ya Waislamu 8,000 nchini Bosnia, na katika kipindi hiki cha miaka hii 25 tumepoteza maisha ya zaidi ya Waislamu 12.5 milioni! Imeongezeka kwa mara 1500! Fauka ya hayo, hizi hazijumuishi takwimu za viwanja vyote vya umwagaji damu kote ulimwenguni. Hii ndio hali mbaya ya Ummah wa Kiislamu leo, kama natija ya kupoteza ngao yake, Khilafah ya Kiislamu, iliyo vunjwa mnamo 1924, takriban miaka tisiini iliyopita.

Uislamu umeuwajibisha Ummah wake kuishi chini ya uongozi mmoja wa kisiasa, Khilafah. Ni haramu kwao kufarakana chini ya zaidi ya uongozi mmoja wa kisiasa, achilia mbali kuishi kwa kudhulumiwa chini ya uongozi wa kiimla wa makafiri walio wengi. Rudisheni ngao ya Ummah, itakayo maliza udhibiti wa makafiri juu ya Waislamu pamoja na kulinda damu na heshima ya wanawake na watoto wa Kiislamu kote katika ulimwengu wa Waislamu! Uokozi pekee wa Ummah huu ni kurudi kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Mtume (saw) amesema,

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (kiongozi wa Waislamu) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na kujihami kwayo (kutokana na madhalimu na washambuliaji).” [Sahih Muslim]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#Srebrenica25YearsOn       #Srebrenitsa25Yıl      #SrebrenicaMiaka25Baadaye    سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 15 Julai 2020 15:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu