Sakata ya Imran Khan
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan alikamatwa kwa kasi na maafisa wa kutuliza ghasia alipokuwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi na uchochezi. Wafuasi wa Khan waliingia mabarabarani, wakiteketeza magari, kushambulia kambi za jeshi pamoja na nyumba za baadhi ya makamanda.