Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuachana na Dolari: Je, Kupungua kwa Utegemezi wa Dolari Kunaathiri Utawala Wake?

(Imetafsiriwa)

Kuna mjadala unaokua kuhusu iwapo mabadiliko kuelekea kwenye matumizi ya sarafu nyenginezo tofauti na dolari katika mikataba fulani ya kibiashara itasababisha mchakato wa kuiondoa dolari, na ikiwa hii itasababisha kupunguzwa kwa utawala wa dolari katika mfumo wa sasa wa dunia.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu kukisia juu ya uwezekano wa kufa kwa dolari, na kwa mabadiliko ya mara kwa mara ndani ya uchumi, haitakuwa mara ya mwisho. Lakini ili kuelewa mjadala wa sasa, na kuuweka katika mtazamo, tunahitaji kuangalia uhalisia wa mfumo huu- vipengele vyake vya kisiasa pamoja na vya kiuchumi- na kuelewa jinsi Marekani imejikita ndani ya Mfumo wa Dunia wa Kibepari ambao nchi zote zimetoa utiifu wao kwake.

Kwa nini mjadala huu umeanza upya?

Habari za hivi punde zinaonyesha dola ambazo zimechukua hatua za kufanya miamala ya kibiashara kwa Yuan ya China, badala ya Dolari ya Marekani, na hivyo kupunguza utegemezi wao kwa dolari.

 - Benki kuu ya Iraq, msambazaji mkuu wa mafuta, ilitangaza kwamba itaruhusu biashara na China kufanywa kwa Yuan kwa mara ya kwanza.

- Benki Kuu ya Bangladesh ilitoa tangazo sawa na hilo mnamo Septemba.

- Wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai linalotawaliwa na China walikubali kuongeza biashara katika sarafu zao za ndani. Kando na China, kambi hiyo inajumuisha Urusi, India, Pakistan, Uzbekistan, Kazakhstan, Tajikistan na Kyrgyzstan.

- Mnamo Disemba, China na Saudi Arabia zilifanya miamala yao ya kwanza ya kibiashara kwa Yuan.

- Urusi imeamua kuhifadhi mapato yake yote ya ziada ya mafuta na gesi ya mwaka wa 2023 kwa Yuan huku ikizidi kutumia sarafu ya China kwa akiba yake ya fedha. (Chanzo: Al Jazeera)

- Brazili na China zilifikia makubaliano ya kufanya biashara kwa kutumia sarafu zao badala ya dolari ya Marekani. Wachina wanatimiza kiapo chao kuanzia Februari cha kufungua nyumba ya kupasisha bidhaa ili kusuluhisha biashara zinazotawaliwa na Yuan nchini Brazil, baada ya kutangaza majumba sawa na hilo ya kupasisha bidhaa nchini Pakistan, Kazakhstan na Laos. (Chanzo)

- China imekuwa ikiondoa bondi zake za Hazina ya Marekani, ambazo ni miongoni mwa zana ambazo nchi hutumia kuweka akiba ya dolari. Sasa inashikilia $870bn katika deni la Marekani, kiasi cha chini kabisa tangu 2010. Pia imekuwa ikijadiliana mikataba na nchi nyingine kufanya biashara kwa Yuan. (CFR)

- China pamoja na Urusi zinafanya miamala biashara ya mafuta kwa sarafu zao za ndani.

- EU imefanya mipango ya kufanya biashara ya mafuta ya Iran kwa euro.

- India imefanya makubaliano ya kulipia mafuta ya Iran kwa rupia.

Maamuzi haya yamechochewa na hali halisi mbalimbali za kisiasa: kuanzia uamuzi wa Marekani wa kuiwekea Urusi vikwazo vya kifedha, hadi kutaka kununua mafuta kutoka Iran na kuepuka mivutano ya kisiasa inayozunguka Makubaliano ya Nyuklia.

Kwa mtazamo wa kimkakati, juhudi za kupunguza utegemezi wao kwa dolari ni matokeo ya hofu kwamba Marekani inaweza kutumia nguvu ya dolari kulenga nchi nyingine, kama walivyofanya walipoiwekea vikwazo Urusi. Kwa kupunguza utegemezi wao kwa dolari, na kuhamisha biashara yao hadi sarafu nyingine kama yuan, mataifa yanaweza kudhoofisha nguvu laini ya dolari.

Kwa mtazamo wa kiuchumi, kupunguzwa kwa utegemezi wao kwa dolari kunaweza kuwaruhusu kudumisha uchumi wao na kupunguza athari ambazo sera za kiuchumi za Marekani zitakuwa nazo kwao.

Hili ni muhimu wakati nguvu ya dolari inapoongezeka, inaongeza mashinikizo ya mfumko wa bei kwa nchi zingine. Hilo linafanya kuwa vigumu kwa benki kuu kudhibiti mfumko wa bei. Maumivu huongezeka kadri nguvu ya dolari inavyosababisha mbano kwa kiasi cha biashara, masharti magumu ya ufadhili wa biashara na kuongezeka kwa deni kuu pamoja na kupanda kwa gharama za kulipa deni. Halafu kuna ukweli kwamba, dolari inapopata nguvu, inaburuza shughuli za kiuchumi duniani, na kushinikiza sarafu nyingine kudhoofika na kuchochea nguvu kubwa zaidi ya dolari. Matokeo haya yana uzito zaidi juu ya shughuli za kiuchumi, kuimarisha udhaifu wa sarafu, kuweka katika mwendo wa kujiimarisha kwa kitanzi cha adhabu. Tokeo moja hasi husababisha jengine. (Chanzo)

Kwa hivyo, kuchukua mkondo mwengine kunaweza kuwasaidia kukabiliana na athari za dolari, na hiyo itategemea mambo mengine mengi.

Lakini je, mseto huu unamaanisha kuwa Dolari itapoteza kabisa utawala wake?

Hapana, haitapoteza. Kwa sababu dolari ingali inatawala- kuongezeka kwa matumizi ya sarafu nyenginezo hakujasababisha dosari kubwa katika utawala wao.

“Cha kushangaza, kushuka kwa hisa ya dolari hakujaambatana na ongezeko la hisa za pauni ya Uingereza, yen na euro, sarafu nyingine za hifadhi za muda mrefu ... Badala yake, kuhama kwa dolari kumekuwa katika pande mbili: robo katika renminbi ya China, na robo tatu katika sarafu za nchi ndogo ambazo zimekuwa na dori ndogo kama sarafu za akiba.” (Chanzo)

“Inaweza kuanzisha mwanzo wa mfumo uliovunjika zaidi ambao unaweza hatimaye kufifisha uwezo wa Marekani wa kutumia vikwazo vya kifedha kama silaha ... “Kadiri nchi zinavyolazimisha kutafuta njia hizo mbadala, kwa ufanisi kile utakachofanya ni kuongeza manufaa ya kiuchumi na uzoefu katika maeneo hayo.” (WSJ)

Lakini huku benki kuu zikishikilia dolari kidogo kama akiba (ikilinganishwa na mwaka jana), IMF inabainisha kuwa dolari ingali inacheza "dori kubwa zaidi" katika masoko ya kimataifa kutokana na dori yake kuu katika biashara ya kimataifa, madeni ya kimataifa na ukopaji usio wa benki, ambao bado unazidi kwa mbali hisa ya Marekani ya biashara, utoaji wa dhamana, na ukopaji na ukopeshaji wa kimataifa. (Chanzo)

“Mambo ambayo yanachangia kutawala kwa dolari ni pamoja na thamani yake thabiti, ukubwa wa uchumi wa Marekani, na hali ya kisiasa ya kijiografia ya Marekani. Kwa kuongezea, hakuna nchi nyingine iliyo na soko la deni lake sawa na Marekani, ambayo jumla yake ni dolari trilioni 18. "Inasaidia zaidi kufikiria Hazina za Marekani kama rasilimali ya akiba inayoongoza ulimwenguni. Ni vigumu kushindana na dolari ikiwa huna soko linalofanana na soko la Hazina.” (CFR)

Licha ya kupungua kwa sehemu ya akiba ya fedha za kigeni, dolari bado inachangia zaidi ya sarafu nyingine zote kwa pamoja. Yuan inachangia 2.7% pekee ya akiba ya kimataifa ya fedha za kigeni. (WSJ)

Kuelewa kina cha hali ni muhimu

Ni kweli kwamba nchi zinajaribu kubadilisha; huu ni uhalisia usioepukika wa mfumo wa sasa ambapo nchi zinazozana kila mara huku zikijaribu kutekeleza maslahi yao ya kitaifa. Lakini ili kuelewa hali hiyo, hatuwezi kuangalia tu takwimu za kiuchumi, au hata katika matukio ya kisiasa ya mtu binafsi. Ili kupata ufahamu wa kina wa hali hiyo, tunahitaji kuelewa jinsi mfumo unavyofanya kazi na dori dolari inayocheza ndani yake.

Ikiwa hali hiyo itatathminiwa tu kama mchezo wa sifuri, na mataifa yenye ajenda tofauti yakishindana, inaonekana kana kwamba hatua ambazo China na mataifa mengine zinachukua zitapelekea utegemezi kutoka kwa Marekani na dolari. Lakini hali inapoeleweka kwa mtazamo wa kimfumo, pamoja na mataifa yanayofuata maslahi yao wenyewe ndani ya mipaka fulani, ili kuhakikisha kwamba mfumo wa Kibepari unaendelea kutawala, uchambuzi wa hali hiyo hubadilika kidogo; hasa tunapoangalia jinsi Marekani ilivyoingiza dolari kwenye mfumo unaochipuza kutokana na mfumo wa Kibepari.

Hadhi ya Kiutawala ya Dolari

Mnamo 1971, Rais Nixon alitoa dolari kutoka kwa dhahabu. Tangu wakati huo, bidhaa muhimu, maarufu zaidi mafuta, zinajumuishwa katika dolari zisizo na thamani ya dhati (fiat), badala ya kuungwa mkono na dhahabu au fedha. Marekani iliimarisha msimamo wa dolari, ilipopata makubaliano kutoka kwa nchi zinazozalisha mafuta kama Saudia, kuuza mafuta kwa dolari pekee na kuunda kile kinachojulikana kama 'dolari za petroli'. Kwa hiyo dunia nzima ilikubali dolari, kwani walihitaji dolari kununua mafuta.

Hii inaathiri biashara, huku mataifa yanayouza nje ya nchi yakishindana katika soko la kimataifa ili kukamata dolari zinazohitajika ili kuhudumia mtaji na madeni ya kigeni yanayotawaliwa na dolari, kulipia nishati inayoagizwa kutoka nje, malighafi na bidhaa kuu, kulipa ada za uvumbuzi na ada za teknolojia ya habari.

Na kwa kuziegemeza sarafu nyingine kwenye dolari, dolari hutenganisha thamani ya biashara ya kila sarafu kutoka kwa uhusiano wa moja kwa moja hadi tija ya uchumi unaotoa sarafu hiyo ili kuunganisha moja kwa moja na saizi ya akiba ya dolari inayoshikiliwa na benki kuu ya nchi inayotoa sarafu hiyo.

Matokeo yake, utawala wa dolari unaiwezesha Marekani kumiliki kwa njia isiyo ya moja kwa moja uchumi mzima wa dunia kwa kupata utajiri wake ili kujumuishwa katika dolari zisizo na thamani ya dhati (fiat) ambazo Marekani inaweza kuchapisha ipendavyo kwa gharama ndogo za fedha.

Dolari ni kipande kimoja tu cha Mfumo, ambapo Marekani ni Mtawala wa Kidunia

Katikati ya miaka ya 1900, wakati enzi ya kibeberu iliyotangulia ilipokuwa inamalizika wakati Vita vya Dunia vilisababisha maafa makubwa kote ulimwenguni, Marekani iliibuka kama mtawala mkuu na kuleta Utaratibu mpya wa Ulimwengu ambao ulifuata mfumo wa kibepari na kuhakikisha kwamba ulimwengu wote ulitoa utiifu wao kwa kwake.

Walianzisha hatua kadhaa ikiwemo kutaka kukarabati uchumi wa dunia kupitia kuruhusu utawala wa dolari, huku nchi nyingine zikiegemeza sarafu zao za ndani kwake na kushikilia dolari kwenye akiba zao ili kudumisha viwango vyao vya kubadilisha fedha. Dolari ilijikita sana katika mfumo huo, na soko la fedha la Marekani la kina na linalonyumbulika, kanuni za uwazi za usimamizi wa shirika na uthabiti wa dolari zilihakikisha kwamba sarafu hiyo imesalia kutawala. (Chanzo)

Lakini hii inakwenda mbali zaidi ya dolari kama sarafu inayotumika kati ya mataifa, na hapa ndipo nyanja za kisiasa na kiuchumi zinaunganishwa.

Marekani ilipoibuka kuwa dola kuu katika zama za baada ya Vita vya Dunia, walitumia nguvu zao za kiuchumi kuunda upya utaratibu wa Dunia; kuanzisha mashirika ya kimataifa, kuingiza dolari katika mfumo, kuanzisha miungano mbalimbali, na kuhakikisha kwamba ni kwa manufaa ya mataifa kufanya kazi ndani ya sura yao ya Mfumo wa Kibepari. Marekani ilipoanzisha Mfumo huu wa Ulimwengu, ilifanya hivyo kwa usaidizi wa mataifa mengine yenye nguvu, ambayo yote yalikubali kupunguza sehemu ya ubwana wa dola zao kwa Mfumo wa Kimataifa ili kupata manufaa ambayo wangepata kwa kufanya kazi ndani ya Mfumo huo kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na Marekani.

Matokeo yake, hata wakati dola zimekwama katika mchezo wa sifuri, yameingizwa kwenye mfumo ambao Marekani inatawala- na kuiondoa Marekani, inamaanisha kuwa watahitaji kuwa na dola ambayo inaweza kuchukua nafasi yake ndani ya Mfumo wa sasa wa Dunia - ambapo hilo halitatokea hivi karibuni. Hii ni kwa sababu mataifa mengine hayana mamlaka au uhalali sawa na ambao Marekani unao kwa sasa, ambayo yote yanahitajika ili mtawala mpya akubalike badala ya Marekani. Na hiyo ina maana kwamba Dolari itabaki kama sarafu inayotawala, hata kama mataifa yatajaribu kupunguza utegemezi wao juu yake. Hii ni kweli hasa unapozingatia ukweli kwamba kila sarafu- ikiwemo Yuan ya China- inafungamanishwa na dolari.

China sio mgombeaji wa nafasi ya Mtawala wa Dunia - kwa hivyo sarafu yao haitachukua nafasi ya Utawala wa Dolari

“Sarafu pekee inayoweza kuchukua nafasi ya dolari ya Marekani kwa muda mrefu ni renminbi, lakini ili iweze kuchukua dori hiyo, lazima sarafu hiyo ibadilike kikamilifu... Sarafu hubadilika kikamilifu wakati inapoweza kubadilishwa kwa uhuru kuwa sarafu nyenginezo kwa madhumuni yote - katika masoko ya fedha, biashara au katika masoko ya kimataifa ya fedha za kigeni. Hata hivyo, yuan inaweza kubadilishwa tu kwa madhumuni machache pekee, kama vile biashara, kuzuia kuvutia kwake licha ya athari zinazoongezeka za China kwenye uchumi wa dunia”. (Chanzo: Al Jazeera)

Lakini masuala ya fedha kando, lengo la muda mrefu la China si kuiangamiza Marekani- ni kuongeza uhuru wao katika Mfumo wa Dunia ambao Marekani iliuunda, ili waweze kutekeleza maslahi yao ya kitaifa bila kuingiliwa na Marekani. Nchi hizi mbili zinafanya kazi ndani ya mfumo mmoja, na uchumi umezifanya kutegemeana.

Hii ndiyo sababu Kukataliwa Kamilifu kwa Mfumo wa Sasa - na Sarafu yake- ni muhimu

Mjadala wa suala la Uondoaji wa dolari unaweka jambo moja wazi kabisa - kuna sababu muhimu sana kwa nini tutazikataa sarafu za sasa pindi Khilafah itakaposimamishwa tena inshAllah.

Kuwa sehemu ya mfumo huu wa kiuchumi, na kukubali sarafu za sasa zisizo na thamani ya kidhati (fiat) hutufanya kuwa wategemezi kikamilifu wa dola adui kama Marekani. Kupitia Dolari, wanaweza kuhakikisha kuwa uchumi wetu unawategemea wao na hii inaruhusu Marekani kuamuru sera zetu (moja kwa moja pamoja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja) na kuhakikisha kuwa tunasalia watumwa kwao.

Haturuhusiwi kujinyenyekesha au kuwa tegemezi kwa dola za kigeni katika Uislamu. Hili ni kweli hasa linapokuja suala la dola adui kama Marekani, Urusi, China, Uingereza na Ufaransa, ambao wangetaka kutawala au kuiangamiza Khilafah. Ni lazima tuchukue tahadhari dhidi yao, jambo ambalo halitawezekana ikiwa tunategemeana nazo.

Hakuna shaka kwamba kutumia fedha zisizo na thamani ya kidhati (fiat) zilizopo leo kutatufanya tuwe wategemezi dola hizi.

Kwa hivyo, chini ya Khilafah, tutakuwa na sarafu yetu inayojitegemea, na hairuhusiwi kuunganishwa na sarafu yoyote ya kigeni.

“Kutengeneza sarafu mahususi kwa ajili ya Serikali ni katika masuala yanayoruhusiwa (mubah), hivyo inaruhusiwa kwa Serikali kuunda sarafu maalum, na kwa njia hiyo hiyo inaruhusiwa kwa Serikali kutofanya hivyo. Kwa hivyo kutoa sarafu si wajibu kwa Serikali, isipokuwa kwa kulinda uchumi wa nchi dhidi ya uharibifu na kuulinda dhidi ya maadui zake kunahitaji kutoa sarafu, ambapo utoaji wake utakuwa ni wajib.

Ni haramu kuiunganisha sarafu yetu na sarafu za kigeni kwani hiyo “itaifanya Dola ifuate dola yoyote ya kikafiri inaunganisha sarafu yake kwake na (kutuacha) kwenye rehema ya dola hiyo ya kikafiri kutoka kwa upande wa kifedha.” (Ibara ya 166 ya Rasimu ya Katiba)

Sarafu hiyo itafungamanishwa na dhahabu na fedha pekee, iwe imetengenezwa kutokana nazo au la. Hakuna aina nyingine ya sarafu ya Dola inayoruhusiwa.

“Serikali inaweza kutoa sarafu au pesa za karatasi, badala ya dhahabu au fedha mradi Bayt Al-Mal ina kiasi sawa cha dhahabu na fedha ili kufidia sarafu iliyotolewa.” Na haturuhusiwi kuruhusu sarafu nyingine yoyote katika ardhi ya Dola ya Kiislamu ikiwa inaweza kusababisha madhara kwa sarafu, fedha au uchumi wetu…” Hii inatumika kwa kuuza nje sarafu ya Serikali, na kuagiza na kuuza nje sarafu za kigeni, kwa njia sawa na ambayo inatumika katika shughuli za ndani ya Serikali.” (Ibara ya 167 ya Rasimu ya Katiba)

Mwenyezi Mungu ameupa Ulimwengu wa Kiislamu nyenzo za kulifanikisha hili. Tuna dhahabu na tuna fedha. Tatizo ni kwamba kwa sasa hatuna udhibiti wowote juu yake. Na sisi tumegawanyika, kwa hiyo rasilimali katika sehemu moja ya ardhi za Kiislamu haziwafikii Waislamu katika maeneo mengine ya Waislamu. Hili litabadilika mara tu Khilafah itakaposimamishwa tena kwa Njia ya Utume ingawa inaweza kufanya iwe vigumu kwetu kupata taswira ya uhalisia huu leo.

Ndiyo maana ni muhimu kuelewa kwamba mambo ni lazima yabadilike pindi Khilafah inapokuja, na kwa nini hatuwezi kutekeleza sheria za Kiislamu ndani ya Mfumo wa Kibepari unaotutawala leo hii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu