Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Modi Mchinjaji wa Waislamu wa India Afungua Hekalu Kubwa Zaidi la Kibaniani nchini Imarati

(Imetafsiriwa)

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alifungua hekalu kubwa zaidi la Kibaniani nchini Imarati huko Abu Dhabi, kwa nia ya kuongeza umaarufu wake kabla ya uchaguzi mkuu wa India uliopangwa kufanyika Mei 2024 [1]. Ujenzi wa hekalu hilo ulianza mnamo 2019, na licha ya kudhulumiwa kwa Waislamu zaidi ya milioni 200 wa India na  Chama cha Bharatiya Janata (BJP) cha Modi uhusiano kati ya Imarati na India umenawiri.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Imarati imepuuza kwa makusudi hali mbaya ya Waislamu wa India kwa kufadhilisha mafungamano ya karibu na Modi mchinjaji wa Gujrat. Imarati haikunyamazia tu ukosoaji wake wa India kuiondoa hadhi maalum ya Kashmir lakini iliendelea kuwekeza sana Kashmir baada ya jimbo hilo lenye Waislamu wengi kugawanywa vibaya na serikali ya Kibaniani yenye msimamo mkali.

Mnamo Oktoba 2021, Imarati ilitangaza kwamba itawekeza kiasi kisichojulikana katika miradi ya miundombinu huko Kashmir. Miaka miwili baadaye, msanidi anayeishi Dubai, Emaar alitangaza kuwa angetumia $60m katika jengo la maduka ya ununuzi na afisi [2]. Jarida la ‘The Economist’ mwezi huu linaripoti kuwa tangu 2019, uwekezaji wa Imarati nchini India umeongezeka mara tatu hadi kufikia $9.8 bilioni na nchi zote mbili zimetia saini makubaliano ya biashara huria mnamo 2023 yaliyoundwa kukuza biashara isiyo ya mafuta hadi $100 bilioni ifikapo 2030 [3].

Kuimarishwa kwa mafungamano ya kibiashara ya Imarati kunakuja kwa gharama ya wakereketwa wa Kibaniani kumwaga damu ya Waislamu chini ya maagizo ya BJP. Ziara ya Modi huko Abu Dhabi inakuja wiki chache tu baada ya kusherehekea ufunguzi wa Ram Mandir-eneo ambalo wafuasi wa Kibaniani wenye itikadi  kali walivunja Msikiti wa Bari wa karne 16 mnamo 1992. Sherehe za ushabiki zilizoandaliwa na BJP ziliwahimiza Mabaniani wenye itikadi kali kufanya vurugu kubwa zaidi dhidi ya raia Waislamu wa India — ikiwa ni pamoja na kupora biashara na mali binafsi, kuchinja Waislamu na kunajisi misikiti.

Hata hivyo hakuna lolote kati ya haya lililoonekana kuwakera watawala wa Imarati, huku wakimkumbatia kwa furaha mchinjaji wa Gujrat, wakachafua mikono yao kwa damu safi ya Kiislamu na kuwepesisha mkusanyiko mkubwa zaidi wa waabudu masanamu katika Bara Arabu. Badala ya kulinda damu ya Waislamu na kuhakikisha ukuu wa Uislamu, watawala wa Imarati waliwapa nguvu Washirikina wa India. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Al Tawbah: 33].

Ili kutia msumari moto kwenye jeraha, Imarati pamoja na Jordan na Saudi Arabia zinashirikiana kwa uwazi na India na dola ya Kiyahudi kutoa daraja la ardhini kusafirisha bidhaa zinazohitajika sana kutoka India hadi umbile la Kiyahudi-ambalo limekatiliwa mbali na Bahari Nyekundu-lakini wanawanyima chakula na maji Waislamu wa Gaza. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa mfano kwa kuupindua muungano wa khiyana kati ya washirikina wa Kiquraish na Mayahudi wa Quraydha baada ya Vita vya Khandaq. Leo, serikali za Imarati, Jordan na Saudi Arabia zinafanya kazi kwa bidii sio tu kuregesha mafungamano thabiti kati ya washirikina na Wayahudi lakini pia kuhakikisha ukuu wao juu ya Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوَاْ إِن تُطِيعُواْ الَّذِينَ كَفَرُواْ يَرُدُّوكُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُواْ خَاسِرِينَ]

“Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.” [Aali-Imran: 149].

Licha ya propaganda za kisasa za Mayahudi na Wahindi dhidi ya Uislamu, ni chini ya Khilafah pekee ambapo washirikina, Mayahudi na Waislamu wanaweza kuishi kwa amani. Katika karne ya 13, Alauddin Khalji wa ufalme wa Delhi alilishinda kundi la Wamongoli mara tano. Hii ilimaanisha kwamba India yenye mabaniani wengi hawakuangamizwa. Badala yake, walinawiri na kustawi chini ya utawala wa Kiislamu. Kadhalika, katika karne ya 15, Mayahudi walioteswa na kufukuzwa kutoka Uhispania ya Kikatoliki walikaribishwa na Khilafah ya Uthmani ambako walistawi kwa karne nyingi chini ya utawala wa Kiislamu.

[وَقُلْ جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [Al-Isra: 81]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu