Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mgogoro wa Kitambulisho wa Marekani:

Usekula, Uliberali, Uhafidhina au Kitu Chengine?

(Imetafsiriwa)

Kitambulisho cha Marekani kimekita mizizi katika historia yake ya ukoloni wa Ulaya na hatimaye kuundwa kwa Marekani. Mababa waanzilishi walisisitiza mgawanyo wa mamlaka kama majibu kwa mifumo ya kiimla ya Ulaya. Uhuru ukawa fahamu muhimu ya kijamii: uhuru wa kumiliki unaopelekea ubepari uliokithiri, ambapo utajiri wa mtu binafsi unathaminiwa zaidi ya yote; uhuru wa dini, unaosisitiza utenganishaji kanisa na dola; na uhuru wa kujieleza, kuruhusu fikra na namna zote za kujieleza kibinafsi bila vikwazo vikali.

Maadili haya, hata hivyo, hivi karibuni yalikabiliwa na changamoto kwa maumbile msingi ya binadamu na busara. Kitambulisho cha kisekula cha Marekani kilikuja kutiliwa shaka, na kusababisha matatizo kama vile haki za kazi dhidi ya maslahi ya shirika, wajibu wa kijamii dhidi ya ubinafsi, uhuru wa mtu binafsi dhidi ya maslahi ya umma, haki za wanawake dhidi ya haki za mtoto ambaye hajazaliwa, na mijadala ya adhabu ya kifo. Changamoto hizi zilijaribu uhalisi na ufaafu wa maadili msingi ya Marekani.

Usekula wa Marekani unakumbwa na mgogoro mkubwa wa kitambulisho, ambao umeakisiwa hivi majuzi katika maoni yanayozidi kuwa tofauti kuhusu haki za LGBTQ+ na dori ya dini katika maisha ya umma. Msukumo wa ajenda ya kisekula iliyokithiri kwa kampeni zinazolenga watoto, kutambulisha maudhui ya LGBTQ+ kupitia vyombo vya habari mbalimbali, ikiwa ni pamoja na katuni na nyenzo za elimu, inalenga kuhalalisha maadili ambayo yanatilia shaka ngono ya kibayolojia na kukuza uingiliaji wa kimatibabu bila idhini ya wazazi. Maadili haya mapya na msukumo kutoka upande uliokithiri uliacha athari kali kwa mtu yeyote asiyekubaliana na ajenda hiyo ambayo inakinzana na imani zilizobebwa muda mrefu za jamii, ilizua mgawanyiko mkubwa wa kijamii na taharuki. Mgawanyiko huu unatia shaka ni wapi ulipo mstari wa uvumilivu kutoka pande zote. Kizungumkuti cha kitambulisho na maadili.

Chama cha Colorado Republican hivi majuzi kilitetea chapisho la mtandao wa kijamii na barua pepe lenye kuhimiza kuchomwa kwa bendera za Ufahari wakati wa Mwezi wa Ufahari. Chapisho kwenye mtandao wa X lilisema, “Choma bendera zote za #pride mwezi huu wa Juni,” na barua pepe kutoka kwa mwenyekiti wa chama Dave Williams ililaani Mwezi wa Ufahari kama shambulizi dhidi ya staha na tishio kwa watoto. Vile vile, Chama cha Republican cha Texas kilipitisha jukwaa linalolenga usawa wa ndoa na uzazi wa jinsia moja wakati wa kongamano lao la kila mwaka la serikali. Jukwaa hili linapinga uamuzi wa kesi ya Mahakama ya Upeo ya 2015 ya Obergefell dhidi ya Hodges, kunyima leseni za ndoa za watu wa jinsia moja, na kuruhusu wafanyibiashara na wafanyikazi wa serikali kukataa kutambuliwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja, na kuuita ushoga “chaguo lisilo la kawaida la maisha.”

Hatua hizi zinaonyesha msukumo mpana wa chama kwa maadili ya kihafidhina katika elimu na nafasi za umma, zikiangazia hali ya kuzorota na kuibua maswali kuhusu kitambulisho cha Marekani. Utafiti ulionyesha kuwa 59% ya Wamarekani wanaamini ubadilishaji jinsia na fikra ya jinsia imekwenda mbali sana, na kura ya maoni ya Gallup ilibaini kupungua kwa kukubalika kwa mahusiano ya jinsia moja. Masuala kama vile ushiriki wa watu waliobadili jinsia katika michezo na utunzaji wa uthibitishaji wa jinsia kwa watoto yanasalia kuwa na utata, na hivyo kuchangia mazingira yenye mgawanyiko. Mwanasiasa Joe Rogan alionyesha kufadhaika na umaarufu wa Mwezi wa Ufahari, akisema, “Watu wanaenda, ‘Imetosha, Inatosha!’ Achenu kulazimisha hili kwa kila mtu!”

Kutatua kizungumkuti hiki kunahitaji kufikiria zaidi ya ajenda za kimaendeleo na za kihafidhina. Uislamu unatoa mtazamo wa kipekee juu ya kitambulisho, maadili, uhuru, ubinafsi, uwajibikaji wa kijamii, na dori za kijinsia kwa masuluhisho ya haraka, ya busara na ya usawa. Kwa mujibu wa Uislamu, Mwenyezi Mungu, Muumba wa vyote, anatufafanua sisi ni nani. Madhumuni ya kuumbwa kwetu na tofauti katika dori, jinsia, makabila na rangi! Vigezo vya mwisho! Kuweka msingi wa maadili na sheria za jamii zinazokuja.

Mwenyezi Mungu (swt) anaeleza katika Quran:

Surah Ar-Rum, Ayah 20-21 (30:20-21):

[وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ * وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ]

“Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote (20) Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri. (21)”

Surah Al-Hujurat, Ayah 13 (49:13):

﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.”

Surah An-Nisa, Ayah 1 (4:1):

﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُواْ رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالاً كَثِيرًا وَنِسَاء وَاتَّقُواْ اللّهَ الَّذِي تَسَاءلُونَ بِهِ وَالأَرْحَامَ إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.”

Kwa kuzingatia aya hizi, Mwenyezi Mungu (swt) anabainisha kwa uwazi kabisa kuumbwa kwetu kutoka kwa mwanamume na mwanamke ili kuzaana na kukuza wanadamu. Muundo wa familia huanza na ndoa yenye utulivu, upendo, na heshima kati ya mwanamume na mwanamke. Uislamu unakataza mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa ili kulinda muundo wa familia na kujenga maadili makubwa zaidi ya kijamii dhidi ya matamanio ya mtu binafsi.

Uislamu unafafanua dori na majukumu ya wazi, thabiti kwa kila mwanadamu kulingana na uwezo na nguvu yake, ukimuhisabu kila mtu kwa matendo yake.

Surah An-Nahl, Ayah 97 (16:97):

﴿مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

“Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.”

Uislamu unamtendea kila mtu kwa usawa bila ubaguzi lakini unatarajia kuzingatiwa kwa maadili yake na kanuni za jamii kwa ajili ya ustawi kamili. Katika Uislamu, uthabiti wa kushikamana unatokana na imani kwamba Mwenyezi Mungu, Muumba aliyeweka kanuni, anajua kilicho bora kwa wote. Uislamu unatoa mfumo kamili wa maisha ulio wazi, thabiti, na wa kina, wenye kurekebisha vurugu la leo la kitambulisho.

Waislamu nchini Marekani wanapaswa kusimama kidete na Uislamu wao kama suluhisho la kina la mgogoro wa kitambulisho, na kurudisha dori yetu kama Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu:

Mwenyezi Mungu (swt) anaeleza katika Quran:

Surah Aali-Imran, Ayah 110 (3:110):

﴿كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Haitham Ibn Thbait

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu