Ufunguzi wa Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan mjini Port Sudan
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu, leo, Jumapili, tarehe 7 Ramadhan 1445 H, sawia na tarehe 17 Machi, 2024, Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan imezinduliwa mjini Port Sudan (mtaa wa Al-Athmah), kusini-mashariki mwa uwanja. Itatumika kama nguzo ya kueneza fikra za Kiislamu, jukwaa la thaqafa ya Kiislamu, kitovu cha utambuzi wa kisiasa, na nukta kianzilishi cha ubebaji ulinganizi kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya utume.