Al-Waqiyah TV: Filamu ya Makala “Palestina Yote ni Wajibu Ikombolewe!"
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Filamu ya Makala “Palestina Yote ni Wajibu Ikombolewe!"
Filamu ya Makala “Palestina Yote ni Wajibu Ikombolewe!"
Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi kwetu kumbukumbu ya uchungu ya miaka 103 H na 100 M ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu (ra), na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H, sawia na 03/03/1924 M, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ilipotea kwa kupotea Imam ambaye ni ngao, Khalifa wa Waislamu ambaye kwaye wanapigana nyuma yake na kujihami..
Kwa Majeshi katika Ardhi za Kiislamu: Je, hamna nyoyo za kuhisi, macho ya kushuhudia, na masikio ya kusikia? Je, hamuoni mito ya damu inayotiririka kutoka kwa watoto wa Waislamu huko Gaza?
Enyi Majeshi katika Nchi za Kiislamu, Inatosha!
Je, Munasubiri amri ya Watawala ndipo muinusuru Gaza Hashem?!
Katika mwezi Mtukufu wa Rajab wa mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi tena kumbukumbu uchungu ya 103 ya kuvunjwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume wote Muhammad, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na maswahaba zake watukufu, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa Mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na 3 Machi 1924 M
Huku umbile halifu la Mayahudi (Wazayuni) likiendelea na ulipuaji mabomu wa kinyama na kikatili wa Gaza, wanawake na watoto ndio wanaohimili uzito wa mauaji haya ya halaiki ambayo yamesababisha vifo na majeraha kwa zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu elfu 72 hadi kufikia sasa
Kalima iliyotolewa na Mhandisi Salah Eddine, Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwenye kongamano "Jibuni Wito: Ikomboeni Palestina!" lililofanywa nchini Uingereza mnamo 24/12/2023 M.
Kuna vita vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya Gaza na kukosekana uingiliaji kati wa majeshi ya Waislamu, haswa yale yanayoizunguka Palestina, licha ya mauaji yote yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, mchana na usiku.
Kampeni ya Kiulimwengu na Siku ya Wanawake Kuchukua Hatua Kuyaamsha Majeshi ya Waislamu na Wito kwao Kuwaokoa Wanawake wa Gaza na Watoto wake na Ukombozi Kamili wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)
Mnamo Jumamosi, 11/11/2023, takriban watawala sitini wa Kiarabu na wasiokuwa wa Kiarabu wa nchi za Waislamu walikutana jijini Riyadh kujadili uvamizi wa Mayahudi dhidi ya Gaza, yaani zaidi ya mwezi mmoja baada ya uvamizi wa Mayahudi kuanza, na baada ya mashahidi zaidi ya elfu kumi na moja na Karibu elfu thelathini kujeruhiwa.