Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Amerika:

Kongamano la Khilafah 2024 “Gaza: Migogoro na Suluhisho – Dori ya Waislamu wa Amerika”

Hizb ut Tahrir/Amerika inaandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa mwaka huu wa 2024 chini ya kichwa:

 “Gaza: Migogoro na Suluhisho - Dori ya Waislamu wa Amerika”

Kongamano hili la kila mwaka la Khilafah litawasilisha msururu wa mihadhara yenye thamani inayozungumzia masuala ya kihistoria na kisiasa ya Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na litatoa njia ya kusonga mbele kwa Waislamu wa Amerika kusaidia kuwanusuru kaka na dada zao huko Gaza.

Kongamanano hilo litaangazia maudhui “Miaka 100 Bila Ngao”, ambayo inatoa uchunguzi muhimu wa karne iliyopita, ukiangazia dhulma na ukatili dhidi ya Waislamu na wanadamu. Kongamano hilo litafafanua maudhui “Palestina: Hadithi Isiyosimuliwa!” Ambayo inatoa uchunguzi wa kina wa athari za tamaa ya ukoloni na athari za kuanzisha na kulinda koloni la Kizayuni katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina). Na inachunguza kwa kina dori ya watawala wasaliti katika nchi za Kiislamu na athari za sera za kikoloni kwa Umma wa Kiislamu.

Kongamano hilo litaangazia mustakabali mzuri, na litajadili kuibuka upya kwa Umma wa Kiislamu, jinsi ukuu wa Umma huu unavyokita mizizi katika imani na rasilimali zake, na umuhimu wa umoja kwa ajili ya ukombozi. Na inasisitiza nafasi muhimu ya Waislamu katika Amerika katika utetezi na uanaharakati, na inatoa wito kwa juhudi za pamoja kushughulikia na kushinda changamoto za kihistoria na za sasa. Kongamano hilo litakuwa tukio la kufungua macho, kutoa mtazamo juu ya matukio ya kihistoria na masuala ya sasa ya kijografia na kisiasa, na njia ya kusonga mbele kwa Waislamu katika Amerika kutatua migogoro hii.

Basi kuweni pamoja nasi na mushiriki malipo...

Jumamosi, 22 Sha’aban 1445 H sawia na 02 Machi 2024 M

- Video Fupi ya Kongamano la kila Mwaka -

- Video za Kongamano la kila Mwaka la 2024 -

[Miaka Mia bila ya Imam ambaye ni Ngao]

Imetolewa na Ustadh Muhammad Shirazi

[Dori ya Waislamu katika Amerika]

Imetolewa na Ustadh Samar Abu Omer

 

[Kisa ambacho bado Hakijasimuliwa!]

Imetolewa na Dkt. Osman Bakhash (Abu Obeida)

Shairi lililokaririwa wakati wa Amali za Kongamano kwa Anwani:

[Kimbunga cha Khilafah]

Lilikaririwa na Dkt. Ghazy Saleem

- Mikutano ya kando ya Kongamano la kila Mwaka la Khilafah la 2024 -

- Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano (1) -

- Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano (2) -

- Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano (3) -

- Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano (4) -

- Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano (5) -

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu