- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Amerika
Ujumbe wa Idd ul-Fitr!
Ndugu na Dada, uthabiti wenu ni muhimu. Kila kitendo, kila dua ya ikhlasi, na kila juhudi ya kusimamisha haki huchangia katika kuhuisha Uislamu na kuregea kwa Khilafah Rashida kwani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake. Mwenyezi Mungu amesema:
[وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَاٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢبَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًۭا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًۭٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao ...” [24:55].
Hebu Idd hii na iwe ukumbusho kwamba faraja iko pamoja na dhiki. Kupitia umoja, ukakamavu, na imani isiyoyumbayumba, tunatoa njia kwa ajili ya mustakabali wa heshima na nguvu. Simameni imara katika Dini yenu, na simamisheni haki, hebu Taqwa na iongoze kila kitendo.
Mzungumzaji: Haitham Ibn Thbait
Jumatatu, 01 Shawwal 1446 H - 31 Machi 2025 M