Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Malaysia: Hizb ut Tahrir Inamtaka Modi Kusitisha Mateso dhidi ya Waislamu nchini India

KUALA LUMPUR, Tarehe 6 Machi, 2020. Licha ya kuwepo na machafuko ya kisiasa nchini Malaysia, Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) haikusahau madhila ya Waislamu nchini India ambao wanauliwa na Wahindu wenye misimamo mikali wakipata idhini ya Waziri Mkuu Narendra Modi. HTM iliandaa maandamano ya amani mbele ya Tume Kuu ya India uliopo Kuala Lumpur ili kuukabidhi waraka wa kumpinga Modi.

Mkusanyiko ambao ulianzia karibu na msikiti, uliongozwa na Msemaji wa HTM, Ustadh Abdul Hakim Othman. Takribani umati wa watu 200 waliandamana wakitembea kutoka katika msikiti hadi katika Tume Kuu wakibeba bendera na mabango huku wakitamka Takbeer kwa sauti kubwa.

Katika waraka huo, HTM inalaani vikali mateso ya Waislamu yanayofanywa na Modi na Wahindu wenye misimamo mikali nchini India na kumtaka Modi aache maramoja mauaji ya halaiki na aina zote za ubaguzi dhidi ya Waislamu. HTM pia imemkumbusha Modi kwamba Khilafah ambayo Hizb ut Tahrir na Waislamu ulimwenguni kote wamekuwa wakifanya juhudi usiku na mchana, haina muda mrefu itasimama, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), na kwamba Modi atapata funzo kama hatakoma.

Yalipowasili maandamano, hakukuwepo na mwakilishi yeyote kutoka Tume Kuu ya India aliyekubali kupokea waraka. Mara tu baada ya maandamano, katika hutuba yake kwa umati uliokusanyika, Abdul Hakim alielezea tukio la kutokupokea waraka kama ni uoga. Msemaji wa HTM pia aliilaumu serikali ya Malaysia kwa kutochukua hatua yoyote kwa kuwa hakuna hata kauli ya kulaani iliyotumwa kwa India kuhusu suala hili. Pia aliitaka serikali ya Malaysia kuifunga Tume Kuu na kumtoa nchini Kamishna wake.

Kabla ya kumaliza hotuba yake, Ustadh Abdul Hakim Othman alitoa ujumbe mkali kwa majeshi ya Waislamu, hususan ya Pakistan na Bangladesh, kutangaza Jihad na kwenda mara moja nchini India kuwaokoa kaka na dada zao, na aliukumbusha umati kuungana na Hizb ut Tahrir kuirejesha tena Khilafah kama suluhisho la pekee la matatizo ya Ummah ulimwenguni kote.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Malaysia

- Video iliyorekodiwa ya Maandamano –

#TurudisheniKhilafah #ReturnTheKhilafah  #YenidenHilafet   أقيموا_الخلافة#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 20 Machi 2020 07:15

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu