Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Malaysia: Kongamano la Khilafah 2020 "Kurudi kwa Khilafah Ili Iongoze Ulimwengu"

 

Kampeni ya kiulimwengu chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa Ataa bin Khalil Abu Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, imeanzisha kampeni pana ya kiulimwengu ya Kumbukumbu ya 99 ya Kuanguka Khilafah, haswa mnamo 28 Rajab 1441 H  / 2020 M na katika tukio hili Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Malaysia iliandaa kongamano lao la kila mwaka "Kongamano la Khilafah 2020" chini ya anwani: "Kurudi kwa Khilafah ili Iongoze Ulimwengu", kupitia kupeperushwa moja kwa moja mtandaoni kwa sababu dhahiri inayo ukumba ulimwengu kwa sasa, Covid-19

Jumapili, 27 Rajab 1441 H - 22 Machi 2020 M

Hizb ut Tahrir / Malaysia Imehitimisha Kampeni ya Kumbukumbu ya 99 ya Kuanguka kwa Khilafah kwa Kongamano la Mtandaoni

KUALA LUMPUR 22 Machi 2020 – Waislamu, hususan nchini Malaysia wanalinganiwa kuungana kufanya kazi ya Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwani ni faradhi ambayo imecheleweshwa kwa muda mrefu tangu kuanguka kwa taasisi hii kuu mnamo 28 Rajab 1432 H, miaka 99 kamili iliyo pita.

Hii ndiyo iliyo kuwa risala kuu ya Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) katika Kongamano la Mtandaoni lililo fanywa asubuhi ya leo katika kukumbuka kuanguka kwa Khilafah. Lilikuwa ndio kilele cha amali zote zilizo fanywa na HTM pamoja na kampeni ya Rajab iliyo fanywa na chama hiki kote ulimwenguni. Kabla ya Kongamano hili la Mtandaoni, HTM ilikuwa imefanya mazungumzo ya kina ya moja kwa moja katika Ukurasa wa Facebook kwa siku tatu mtawalia ikijadili haja ya Khilafah.  

Kampeni ya mwaka huu ilijifunga na mbinu ya mtandao kuafuatia mkurupuko wa COVID-19 ambao tayari umefikia kiwango cha kuwa janga, iliyo sababisha serikali ya Malaysia kulazimisha Amri ya Kudhibiti Matembezi ya watu tangu Machi 18.

Kongamano hili la Mtandaoni liliwaleta pamoja wazungumzaji wanne akiwemo msemaji wa HTM aliyetoa hotuba zao chini ya kauli mbiu ya Kongamano hilo "2020: Kurudi kwa Khilafah Ili Iuongoze Ulimwengu".

Hafla hiyo ilianza kwa muhadhara wa Ustaadh Mu’adz Abu Talhah kwa anwani "Utabiri wa NIC juu ya Kurudi kwa Khilafah". Mzungumzaji huyu alikusudia ripoti ya Baraza la Kitaifa la Ujasusi la Amerika (NIC) ya 2004. Baada ya kuwasilisha kwa mukhtasari ripoti hiyo, mzungumzaji huyu alisisitiza kuwa Hizb ut Tahrir kamwe haitegemei ripoti hii katika kazi zake, bali ripoti hiyo yaonyesha umakinifu wa adui wa Uislamu na hofu zao za Umma kurudisha tena umbile lao la kisiasa.

Muhadhiri wa pili, Ustaadh Muhammad Amin alitoa muhadhara wake kwa anwani: "Hofu ya Viongozi wa Makafiri ya Kurudi Khilafah", ambapo alionyesha vipande vya hotuba zilizo tolewa na viongozi hao wa Makafiri tangu wakati huo, zinazo mulika hofu yao ya kurudi kwa Khilafah. Zaidi ya hayo, pia alifichua mikakati ya maadui wa Uislamu katika juhudi zao za kuzuia kurudi tena Khilafah.

Hafla ikiendelea, mzungumzaji wa tatu, Ustaadh Umar Hussein alizungumzia kadhia ya "Demokrasia kama mojawapo ya Miradi ya Makafiri ili Kuzuia Kurudi kwa Khilafah". Mzungumzaji huyu alifafanua uhalisia wa Demokrasia, mgongano wake na Uislamu, na jinsi Wamagharibi walivyoipanda katika biladi za Waislamu na kuitumia kuzuia kurudi kwa Khilafah.

Muhadhara wa mwisho ulitolewa na Ustaadh Abdul Hakim Othman, msemaji wa Hizb ut Tahrir / Malaysia, aliye angazia bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kuhusiana na kurudi kwa Khilafah. Mzungumzaji huyu alifafanua Hadith chache za Bishara njema hii na hatimaye akasisitiza wajibu wa Umma kufanya kazi kwa umakinifu ili kuipata, na kunyamaza kimya itakuwa ni dhambi kwa kila Muislamu. Kwa bishara njema hizi nyingi kutoka kwa Rasulullah (saw), Msemaji wa HTM alitamatisha kuwa Khilafah itasimama tena hivi punde, na sio muhali kuwa Khilafah huenda ikarudi mwaka huu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

Kongamano hili la Mtandaoni lilifuatiwa na ukumbi wa maswali kutoka kwa watazamaji, kabla ya kufungwa takriban saa 12.30 mchana. Rekodi kamili ya kongamano hili na matukio mengine yaliyo fanywa wakati wa kampeni yote hii zinapatikana katika ukurasa rasmi wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Malaysia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir \ Malaysia

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru tovuti za Hizb ut Tahrir / Malaysia:

Ukurasa Rasmi wa Hizb ut Tahrir/ Malaysia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir/ Malaysia
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir/ Malaysia
Akaunti ya Telegram ya Hizb ut Tahrir/Malaysia

#ReturnTheKhilafah     #YenidenHilafet    #TurudisheniKhilafah   أقيموا_الخلافة#

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 08 Aprili 2020 22:01

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu