- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:
Kampeni “Katika Kumbukumbu ya Miaka 14 ya Kutekwa Nyara Kwake… Mwachilieni Huru Naveed Butt!”
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan ilizindua kampeni ya mitandao ya kijamii, haswa kwenye mtandao wa X (zamani ikijulikana kama Twitter), yenye kichwa “Katika Kumbukumbu ya Miaka 14 ya Kutekwa Nyara Kwake... Mwachilieni Huru Naveed Butt!” Kampeni hii inalenga kuishinikiza serikali dhalimu ya Pakistan, ambayo huduma zao za siri zilimteka nyara Mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, miaka 14 iliyopita mbele ya familia yake na majirani zake. Kutekwa nyara kwake kulikuwa ni matokeo ya uwazi wake katika kutetea haki na kuwaita Waislamu kutimiza wajibu wao wa kidini kwa kumchagua Khalifa muongofu ambaye atawatawala kulingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw). Hili limepitiliza mipaka yote ya ukatili. Pazeni sauti zenu kudai kuachiliwa huru kwa ndugu yetu Naveed Butt.
Ewe Mwenyezi Mungu, turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume... Allahumma ameen.
Ijumaa, 28 Dhu al-Qi'dah 1447 H sawia na 15 Mei 2026 M

- Tarehe ya kampeni ya Twitter -
Jumamosi, 16 Mei 2026 M
Saa: Tatu Usiku kwa Saa za Wilayah ya Pakistan
(Saa Moja Usiku kwa saa za Madina Al-Munawwara)

Dua
Kwa Ndugu Naveed Butt Mwenyezi Mungu amfungue kifungoni mwake
(وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَرِيبًا)
“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!”
Mwenyezi Mungu akubali matendo yako mema, Naveed.
Mola atupe amani ya akili kuhusu ndugu yetu na mpendwa wetu Naveed.
Ewe Mwenyezi Mungu, mlinde kwa jicho lako lisilo lala,
Mlinde kwa nguvu zako zisizoweza kushambuliwa,
Na umsitiri kwa pazia lako lisilopenyeka.
Ewe Mwenyezi Mungu, mjalie afya katika mwili wake, kusikia kwake, na kuona kwake.
Ewe Mwenyezi Mungu, mlinde kutoka pande zote,
na ninakimbilia kwako, Ewe Mola Mlezi, kutokana na madhara yoyote yanayoweza kumpata.
Ewe Mwenyezi Mungu, mlinde akili yake na ustawi wake,
Na umlinde kutokana na maovu ya walinzi wa gereza na wakandamizaji,
Na kutokana na maovu ya viumbe vyako vyote.
Ewe Mwenyezi Mungu, mrudishe kwa familia yake na kwetu sisi salama, timamu, mwenye afya njema, mwenye heshima, na mwenye heshima, pamoja na wafungwa wote wa Kiislamu, wanaume na wanawake, kutoka katika magereza ya wakandamizaji.
Ewe Mwenyezi Mungu, teremsha rehma na amani yako juu ya Mtume wetu Muhammad na juu ya familia yake na maswahaba zake wote.
Imetolewa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Jumatatu, 24 Dhu al-Qi'dah 1447 H, sawia na 11 Mei 2026 M



Makala ya Ustadh Musab Umair – Wilayah ya Pakistan
Kwa kichwa:
Tarehe ya Kumi na Moja ya Mei
Kumbukumbu ya Kutekwa Nyara kwa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, Naveed Butt
Jumatano, 26 Dhu al-Qi'dah 1447 H, sawia na 13 Mei 2026 M
Bonyeza Hapa
(Hivi Punde InshaAllah)

Ili kupata taarifa kuhusu kampeni iliyozinduliwa mapema na Afisi Kuu ya Habari ili kuunga mkono kesi ya Mhandisi Naveed Butt, Mwenyezi Mungu ampe faraja kifungo chake na uhuru na amrudishe kwetu akiwa salama.
Bonyeza Hapa
(Hivi Punde InshaAllah)

Alama Ishara za Kampeni
#أطلقوا_سراح_نفيد_بوت
#أطلقوا_سراح_نفيد_بوت_الداعي_للخلافة
#FreeNaveedButt
#FreeNaveedButt_AdvocateOfKhilafah
#خلافت_کے_داعی_نویدبٹ_کو_رہا_کرو

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Akaunti ya Facebook ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Akaunti ya Jukwaa la X ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan




