Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa:

Kutoka Mji Wa Hebron, Maelfu Wayataka Majeshi Kuhamasika Kuinusuru Gaza!

Maelfu ya watu wa Palestina walijitokeza kwa wingi katika mji wa Hebron kama wito kwa Umma, vikosi vyake na majeshi yake kuchukua hatua za haraka kuinusuru Gaza na watu wake, na hata kuukomboa Mji Mtakatifu na ardhi nzima iliyobarikiwa.

Nchi ya Khalil al-Rahman iliyapigia kelele majeshi ya Jordan, Misri, Pakistan, na Uturuki, ikiyahamasisha kupigana jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kumkomboa mfungwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Umati wa watu hao walisisitiza kuwa, Gaza haihitaji dawa wala msaada, bali inahitaji kusonga mbele kwa majeshi ya Umma ili kuliondoa umbile la Kiyahudi, kuwaondolea watu maovu yake, na kuitakasa sehemu ya ibada ya Mtume (saw).

Sauti zilizotoka kwenye koo za umati huo zilisisitiza kuwa, nchi za Magharibi kwa ujumla wake sio tu kwamba zina upendeleo, bali ni maadui wa Umma wa Kiislamu. Kwa silaha zao tunaua, na kwa maneno yao, nyumba zinabomolewa juu ya vichwa vya wakaazi wake. Lugha yao inasema kuwa ukafiri ni mila moja, na chuki imedhihiri midomoni mwao na yale yanayofichwa na vifua vyao ni makubwa zaidi. Anatarajia suluhu kutoka kwao, si kutoka kwetu.

Umati huo wa watu unamchukulia mtu yeyote anayedai upatanishi kutoka kwa watawala, kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati, kutaka kutekelezwa kwa maazimio ya Baraza la Usalama, na wito wa suluhisho la Marekani la dola mbili, ni msaliti wa damu ya mashahidi na mlaji njama pamoja na maadui.

Umati ulitoa wito kwa wanazuoni wa Umma kutekeleza wajibu wao na kuyachochea majeshi kufanya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kutoa afueni na ushindi kwa Gaza.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Jumatatu, 1 Rabi’ al-Akhir 1445 H - 16 Oktoba 2023 M

- Sehemu ya Amali Hiyo -

Kutoka Hebron, maelfu wayataka majeshi yahamasike kuinusuru Gaza!

Hizb ut-Tahrir inatoa wito kwa Umma na majeshi yake kutangaza vita kwa ajili ya kuinusuru Gaza na Palestina!

Dkt. Ibrahim Al-Tamimi

Hii ni amana ya Sultan Abdul Hamid, Enyi Watu wa Uturuki, basi chukueni hatua ya kuinusuru!

Dkt. Musab Abu Arqoub

- Sehemu ya Swala -

#Al-Aqsa Flood

#Armies_to_the_Aqsa

#ArmiesToAqsa

#AksaTufanı

#OrdinaryAksaya

#Al-Aqsa_crying_armies

Aqsa_calls_armies #

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Ukurasa wa X wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 01 Novemba 2023 12:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu