- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan:
Ripoti ya Habari 08/08/2021 [Mukhtasari]
Muendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mikoa na wilaya tofauti tofauti za nchi ili kujenga rai jumla juu ya vipengee vya Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na nidhamu tofauti tofauti za maisha, ambazo zinashughulikia mada anuwai, zikiwemo: kadhia ya Bwawa la An-Nahdha, sera ya kuondoa ruzuku, njia ya kisheria ya mabadiliko, na vita vya kikabila katika maeneo tofauti tofauti ya Sudan.
Mnamo Julai 7, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya mkutano wao wa kawaida huko El Obeid, ambao ulikuwa na anuwani: "Sera ya Kuondoa Ruzuku ... Je! Itatatua Tatizo la Uchumi nchini Sudan?" Bwana Muhammad Al-Amin Dafa alizungumza ambapo alionyesha kwamba sera ya msaada haitashughulikia uchumi wa Sudan; badala yake, itaharibu uchumi wa Sudan, kwani kila mtu anapitia maisha duni kama matokeo ya serikali kutekeleza sera hii.
Mnamo Julai 12, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi huko Souk Libya, yenye kichwa: "Bwawa la An-Nahdha ... Ahadi ya Vita na Uzembe wa Watawala", ambapo Ustadh Abd al-Rahim Abdullah alizungumza, akielezea hamu ya Hizb ut Tahrir katika maswala yote ya Ummah na utoaji wake wa taarifa na machapisho ambayo yanaonyesha masuluhisho sahihi kutoka kwa kanuni kuu ya Uislamu.
Mashababu wa Omdurman Magharibi pia walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya mnamo Julai 14, 2021 kwa anwani: Kuenea kwa Ukabila Nchini, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza, ambaye aliihimiza hadhira wamuogope Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliyewaumba kutokana na nafsi moja, na akaelezea kusudi kuwepo makabila. Ni kwa ajili ya kufahamiana na mafungamano ya kindugu, sio kushikamana na kabila na kujikusanya kwa misingi yake ili kupata haki na kutoa malalamiko, kama tunavyoona sasa katika maeneo anuwai ya Sudan, na kwa hivyo mapigano na umwagaji damu kutokea!
Hotuba ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Al-Obeid mbele ya Mlima Al-Dhahab Musalah mnamo Julai 14, 2021, kwa anwani "Mabadiliko ya kweli yatatokea kwa Kuachana na Mfumo wa Kirasilimali na Kuubadilisha na Mfumo wa Uislamu.” Imam Muhammad Ibrahim alielezea ufisadi wa kanuni ya kirasilimali katika suala la imani. Na mfumo huo, ambao ndio sababu ya mateso ya wanadamu na kuenea kwa dhulma na ufisadi katika ardhi, ambayo wamewafanya watu kuibuka na mapinduzi dhidi ya udhalimu.
Kwenye suala la Bwawa la An-Nahdha pia, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa mnamo 15 Julai 2021 katika eneo la Dukhainat la soko la Kalakila, kwa anwani: "Bwawa la An-Nahdha… Usaliti wa Watawala na Wajibu wa Umma ”, ambapo Ust. Al-Fateh Abdullah alizungumza juu ya hatari ya Bwawa la An-Nahdha nchini Sudan na Misri, na kwamba ni tishio la kihakika kwao la kiu au kuzama ikitokea kuporomoka kwa bwawa hilo baada ya kujazwa mara ya pili, akifichua sababu za kuporomoka kwake kuwa limejengwa katika eneo la tetemeko la ardhi, na vile vile ukubwa wake na uwiano wa usalama wake sio zaidi ya moja nukta tano ikilinganishwa na Bwawa Kuu huko Misri (kiwango chake cha usalama ni zaidi ya nane).
﴾وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ﴿
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aali-Imran: 103]. Chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Kosti Ijumaa, Julai 16, 2021 katika Rabik Souq, makutano ya reli na Barabara ya 50. Abdul Majeed Othman alielezea fahamu ya aya hiyo na sababu ya kuteremshwa kwake kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kushikamana na kamba thabiti ya Mungu na kuharamisha mgawanyiko na tofauti kwa misingi ya kieneo au ya kikabila, ambayo ndio sababu ya umwagaji damu, ukiukaji wa heshima na ulaji utajiri wa watu kinyume cha sheria katika Bara Arabia, kwa hivyo Uislamu ulikuja na kuwayeyusha ndani chungu cha Uislamu na kuwafanya Umma mmoja.
Kuhusu kadhia ya Bwawa la An-Nahdha, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan jijini Gadharef walitoa hotuba yao ya kila wiki kwa anwani: "Bwawa la An-Nahdha… Hatari" katika Uwanja wa Rowena King Square, mnamo Julai 15, 2021 M, ambapo wahudhuriaji walihutubiwa na Bwana Nasr El-Din El-Haj, ambaye alizungumza juu ya umuhimu wa maji kwa kila kiumbe hai, kwani haiwezekani kuishi bila hayo, na yanachukuliwa katika Uislamu kama mali ya umma, kwani hairuhusiwi kwa yeyote kuyafanyia ukiritimba ili kuizuia jamii isiyatumie.
Hotuba ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la El-Obeid ilikuja chini ya kichwa: "Njia ya Kisheria ya Mabadiliko," mnamo Julai 27, 2021 mbele ya Sowar al-Dhahab Musalah. Suluhisho la matatizo ya wanadamu, na inahitajika kuandaa wanaume ambao ndani yao mtaala unajumuisha fahamu na njia huku bidii ikijengwa juu ya msingi wa imani na masuuhisho yatokanayo kwayo.
Kuhusu suala la Bwawa la An-Nahdha, ambayo ni mada moto siku hizi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi mnamo Agosti 5, 2021 katika soko la Libya ilifanya mazungumzo ya kisiasa yaliyohutubia sera inayoitwa: "Bwawa la An-Nahdha ... Ni nani anayelipia gharama?" Ust. Abdul Rahim Abdullah alianza hotuba yake kwa aya tukufu
﴾وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاء كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ﴿
“Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai.” [Al-Anbiya: 30]. Alitaja umuhimu wa maji na hadithi ya Wamisri wa kale na Mto Nile na jinsi walivyokuwa wakiwatoa kafara kila mwaka wasichana wazuri zaidi wa Misri ili kuufanya mto kufurika, na jinsi Uislamu ulivyokomesha mila hii na kuwa rehema kwa walimwengu. Mzungumzaji pia alitaja njama ya watawala wa Misri na Sudan na makubaliana yao ya kujenga bwawa hilo, wakipuuza maslahi ya watu wao. Halafu akaongeza kuwa ni dola tu yenye maadili pekee ndio inayoweza kumaliza hatari hizi; dola ya uchungaji, sio dola utozaji ushuru; ambayo ni, Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, hivi karibuni Inshallah, baada ya utawala huu wa ukandamizaji. Lazima sote tufanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kuondoa hatari kutoka kwa taifa letu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/sudan/1789.html#sigProId51cead3bae