- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan:
Amali na Shughuli Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 1447 H
Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iliongeza shughuli zake za umma wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ikihimiza jamii ya Waislamu kufanya kazi nayo ili kuanzisha jengo kuu la Uislamu: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo ilivunjwa miaka 105 iliyopita. Iliendesha hotuba za kisiasa, mihadhara, na visimamo katika viwanja vya misikiti, masoko, na maeneo mengine ya umma, pamoja na programu zake za kawaida katika afisi zake katika miji mbalimbali ya Sudan. Na hii hapa ni baadhi ya mifano ya amali zake:
Mjini Port Sudan, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa ya kila wiki mbele ya uwanja wa Hoteli ya Al-Haramain katika soko kuu. Wazungumzaji walizungumzia maoni ya hizb kuhusu matukio ya sasa, ya ndani na ya kimataifa, na kuwasilisha hukmu ya Kiislamu kuhusu kila suala. Hotuba ya mwisho ya hizb wakati wa Ramadhan, ilikuwa kwa kichwa “Vita vya Ain Jalut na Kurudi kwa Izza kwa Waislamu,” ilitolewa mnamo Jumatatu, 16 Machi 2026. Ndani yake, Ustadh Adel Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza, akiamsha hima za jamii ya Waislamu na kuwakumbusha kwamba ni umma wenye dhamira na taifa la mapambano. Alielezea kwamba wakati wowote umoja wa jamii ya Waislamu unapovunjika na kugawanyika, viongozi wakuu hujitokeza kwanza kuiunganisha, na kisha kupigana kama walivyopigana na Matatari, na kuwasababishia ushindi mkubwa. Alitaja Vita vya Ain Jalut kama moja ya vita vikubwa zaidi katika historia ya Waislamu. Hotuba zengine zilitolewa chini ya vichwa kama vile “Saumu: Dhihirisho miongoni mwa Madhihirisho ya Umoja wa Waislamu” na “Shura ni Hukmu ya Kisheria, Sio Mfumo wa Utawala,” miongoni mwa nyenginezo.
Miongoni mwa amali muhimu zaidi ilikuwa ni kisimamo kilichofanywa na wanachama wa Hizb ut Tahrir katika uwanja wa Msikiti Mkuu huko El Obeid, kama sehemu ya amali za kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah. Ustadh Al-Nadhir Muhammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alihutubia mkutano huo, akikumbusha umma kuhusu taji la faradhi zote: Khilafah, na wajibu wa kufanya kazi kuelekea kusimamishwa kwake tena. Hotuba yake yenye nguvu na yenye athari ilikubaliwa pakubwa. Kufuatia hili, vikosi vya usalama viliwakamata wanachama wanne wa Hizb ut Tahrir na kuwafungulia mashtaka ya uongo chini ya Kifungu cha 69 cha Kanuni ya Adhabu ya Sudan (uvurugaji amani ya umma na utulivu). Hili ni moja ya mashtaka ya ajabu zaidi kuwahi kurekodiwa katika ripoti za polisi huko El Obeid.
Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Sudan alitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakati huo akikanusha mashtaka dhidi ya mashababu hao, ambao ni wabebaji wa ujumbe wa manabii na mitume. Pia alifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo Jumamosi, 21 Februari 2026, afisini kwake Port Sudan, kuhusu kesi za mashababu hao huko El Obeid. Katika mkutano huo, aliishutumu serikali kwa kushiriki katika vita vya Amerika dhidi ya Uislamu kwa kutumia kisingizio cha “ugaidi” kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko vile Amerika yenyewe ilivyotarajia. Pia alikosoa msimamo wa aibu wa upande wa mashtaka, majaji, na vyombo vya usalama kuhusu ujumbe huu. Msemaji huyo alisema, “Misimamo hii haishangazi; tumeishuhudia kutoka kwa serikali zilizopita katika miaka michache iliyopita.”
Amali nyengine muhimu ilikuwa iftar ya Ramadhan (mlo wa kufunga saumu) katika afisi ya hizb mjini Al-Qadharif. Mashababu waliandaa iftar, ambayo ilihudhuriwa na mkusanyiko mkubwa wa watu walioitikia mwaliko huo mkarimu. Hili lilifanyika mnamo Ijumaa, tarehe 17 Ramadhan, 1447 H. Baada ya iftar hiyo, Ustadh Maysara Yahya Muhammad Noor, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alitoa hotuba. Alijadili matukio ya Vita vya Badr, akichora masomo na ufahamu kutoka kwake, na kuangazia umuhimu wa wakati huu. Alisisitiza kwamba Ramadhan ni mwezi wa utiifu, kufunga, swala, jihad, na ushindi, akisisitiza kwamba ushindi unategemea utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu. Kisha akazungumzia hali ya sasa ya Waislamu chini ya ukandamizaji wa Mayahudi, inayoungwa mkono na Amerika na vibaraka wake miongoni mwa watawala wa Waislamu na tawala dhalimu mbazo Sheikh Taqi al-Din al-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema kuzihusu: “Umbile la Kiyahudi ni kivuli cha tawala za Kiarabu; pindi tawala hizo zitakapotoweka, kivuli chake pia kitatoweka.”
Jijini Khartoum, mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walifanya Iftar ya Ramadhan, ambayo iliwaleta pamoja watu mashuhuri wa eneo hilo. Ustadh Abdullah Hussein, mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, alizungumzia kuhusu uthabiti kwa kanuni pamoja na umoja wa Ummah, na kwamba Khilafah ya Kiislamu ni mojawapo ya wajibu muhimu zaidi katika wakati huu, na kwamba Ummah unahitaji wanazuoni ambao hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu katika haki, na akalingania kufanya kazi pamoja na wanaofanya kazi ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu.
Kongamano la kila mwezi, lililofanyika tarehe 18 Ramadhan 1447 H (7 Machi 2026 M), liliandaliwa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika afisi yake mjini Port Sudan. Wazungumzaji walizungumzia mgogoro wa Marekani na Uingereza nchini Sudan, udhibiti wa Marekani juu ya faili ya vita, kurefushwa kwake, zana zinazotumika katika mgogoro huu, na udanganyifu wa makubaliano ya uongo ya usitishaji vita yaliyotangazwa na Amerika. Walijadili kwamba makubaliano haya hayakusudiwi kutatua tatizo bali kulidhibiti, na hatimaye kuiongoza Sudan katika hali inayofanana na hali ya Libya, ambayo inaleta tishio la kweli la kujitenga kwa eneo hilo na Sudan. Pia, katika mji wa Al-Qadharif, hizb ilifanya kongamano lake la kawaida la Ramadhan kuhusu maendeleo katika juhudi za Amerika za kuigawanya Sudan na jinsi ya kuzizuia. Wazungumzaji waliwasilisha mapambano ya ushawishi kati ya Waamerika wa Wazungu nchini, wakionya waziwazi kuhusu majaribio ya Wamarekani ya kutenganisha Darfur kwa kuwawezesha Vikosi vya Msaada wa Haraka kudhibiti eneo lote la Darfur na kupunguza juhudi za jeshi kulichukua tena, kama utangulizi wa kutengana kwake hatimaye. Hizb ilitoa ujumbe kwa watu wenye ikhlasi wa umma huu, ikiwasihi wasiruhusu Amerika kuichana Sudan kama ilivyokuwa hapo awali na Sudan Kusini. Hizi zilikuwa baadhi ya amali, na nyengine nyingi zilifanyika katika miji mbalimbali kote nchini Sudan.
Amali hizo zilimalizika kwa swala ya Idd, ikiongozwa na wanaharakati kadhaa wa da'wah. Mjini Port Sudan, Ustadh Yaqoub Ibrahim alihutubia mkusanyiko wa waswaliji katika kitongoji cha Yathrib, akiwakumbusha umoja wa Ummah na umoja wa nembo na mtendo yake ya ibada. Alielezea kwamba tofauti katika wakati wa kufunga na Idd miongoni mwa Waislamu zinatokana na kutokuwepo kwa Khilafah, ambayo inaunganisha Ummah. Aliwasihi Waislamu—wanaume, wanawake, na vijana—kushirikiana na wale wanaojitahidi kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Wakati huo huo, Ustadh Adel aliongoza swala ya Idd huko Yathrib, Port Sudan, huku Abdullah Hussein akiongoza swala ya Idd katika eneo la Al-Dukhainat jijini Khartoum, na mashababu wengine wakiongoza swala hiyo katika miji mbalimbali kote nchini Sudan.
Mwenyezi Mungu awasaidie mashababu wa Hizb ut Tahrir wanapofanya kazi bila kuchoka mchana na usiku, wakijitahidi kuelimisha Ummah kuhusu njama zinazopangwa dhidi yake. Wanafanya kazi baina ya Ummah na pamoja nao, wakitumaini ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na hilo si gumu Kwake.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
Jumatatu, 26 Shawwal Al-Khair 1447 H – 13 Aprili 2026 M

https://hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/sudan/5330.html#sigProId5c32cbe265

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan




