- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Enyi Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Fanyeni Mapinduzi dhidi ya Watawala Waovu wala Msiwategemee wao”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliandaa matembezi yenye kichwa “Enyi Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Fanyeni Mapinduzi dhidi ya Watawala Waovu wala Msiwategemee wao” baada ya swala ya Ijumaa kutoka Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu, ambayo yalipangwa kufika Al-Barabara ya Al-Thawra kama ilivyo kila Ijumaa. Ni matembezi ya 26 mfululizo tangu vita vya mauaji ya halaiki vizuke dhidi ya Waislamu katika Ukanda wa Gaza katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina).
Hata hivyo, mara baada ya kuzinduliwa kwa matembezi hayo ya kuinusuru na kuiombea nusra Gaza mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu, vikosi vya usalama viliyazuia kwa kisingizio cha bango kuu la matembezi hayo, lililokuwa limeandikwa: “Enyi Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Fanyeni Mapinduzi dhidi ya Watawala Waovu wala Msiwategemee wao” na ambalo linawataka wanausalama wawaondoe, lakini umati mkubwa wa watu waliohudhuria matembezi hayo ulionyesha kuondolewa kwao na hivyo kupelekea wanausalama hao kusimamisha matembezi hayo na hawakuruhusu kufika barabara ya Al-Thawra, kama kawaida.
Licha ya jaribio la kuyazuia, shab mmoja wa Hizb alitoa kalima ambapo alitoa wito kwa majeshi kuangusha viti vya ufalme na kuinusuru Palestina, mabango mengine pia yalisomeka, "وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ" “Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa,” [Hud: 113] na kwenye mingine, “Takwimu za mashahidi na Waislamu waliojeruhiwa mjini Gaza”.
Waliohudhuria walionyesha ghadhabu na hasira zao kwa wanausalama na kuimba miito kama vile “Enyi watawala wa aibu, Gaza iko chini ya moto,” “Enyi majeshi, enyi majeshi, haribu viti hivi vya utawala," na kauli mbiu zingine.
Kweli, ni aibu iliyoje! Wakati ambapo watu wetu wa Gaza wanasagwa na kuvunjiwa heshima yao, bango hili linapigwa marufuku Tunis, mji mkuu, kwa sababu kwa maoni yao limewatukana watawala wasaliti Ruwaibidha waliowazingira watu wetu huko Gaza, na kuwatia njaa, na wakajifungamanisha na umbile halifu la Kiyahudi na kulipatia mahitaji yote ya maisha... Mwenyezi Mungu anatutosha, na Yeye ndiye wakili bora wa mambo katika watawala jeuri, madhalimu, wahalifu.
Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 19 Ramadhan 1445 H sawia na 29 Machi 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/3857.html#sigProId4dc5ff9484
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: