- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Enyi Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Fanyeni Mapinduzi dhidi ya Watawala Waovu wala Msiwategemee wao”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliandaa matembezi yenye kichwa “Kutoka Tunis Hadi Gaza... Takbira za Idd zinayahamasisha Majeshi ya Waislamu!” baada ya swala ya Ijumaa kutoka Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu, ambayo yalipangwa kufika Al-Barabara ya Al-Thawra kama ilivyo kila Ijumaa. Ni matembezi ya 27 mfululizo tangu vita vya mauaji ya halaiki vizuke dhidi ya Waislamu katika Ukanda wa Gaza katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina).
Wakati wa maandamano hayo, umati wa watu ulipiga takbira za Idd muda wote wa matembezi hayo na kuinua mabango, ambayo la kwanza lilikuwa na kichwa cha matembezi hayo: “Kutoka Tunis Hadi Gaza... Takbira za Idd zinayahamasisha Majeshi ya Waislamu!” kwenye bango kuu iliandikwa: “Enyi Majeshi ya Waislamu, Ardhi Iliyobarikiwa inalilia nusra yenu je mutajibu?” Jengine lilikuwa limeandikwa juu yake takwimu za mashahidi na waliojeruhiwa, na matembezi hayo yalihitimishwa kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa hizb mbele ya ukumbi wa michezo wa manispaa kwenye barabara ya Al-Thawra.
Na hivyo, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia itaendeleza uungaji mkono wake kwa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kwa watu wetu wa Gaza, Hashem, hadi Mwenyezi Mungu atakapowaleta watu wenye ikhlasi kutoka kwa majeshi ya Waislamu ambao watawang'oa watawala hawa wasaliti na kuanzisha jengo kubwa la Uislamu, Khilafah Rashida, juu ya magofu ya viti vyao vya utawala, hivyo kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina kuanzia mto wake hadi bahari yake) na nchi nyingine za Kiislamu... na siku hiyo Waumini watafurahi kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu .
Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 03 Shawwal Al-Khair 1445 H sawia na 12 Aprili 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/3873.html#sigProId8f5729f50c
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: