- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Serikali za Kijamhuri na za Kifalme Zimeisaliti Gaza... Kwa Khilafah tutainusuru Gaza”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ilifanya matembezi makubwa katika mji mkuu wa Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fath baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 25 Julai 2025 M chini ya kichwa:
“Serikali za Kijamhuri na za Kifalme Zimeisaliti Gaza... Kwa Khilafah tutainusuru Gaza”
Mabango yaliinuliwa wakati wa matembezo hayo, bango kuu likiwa na kichwa cha matembezi, na bango la pili likiandikwa “Enyi majeshi ya Waislamu, Umma wenu unakuombeni nusra yenu. Zaidi ya watu 61,000 wameuawa shahidi na zaidi ya watu 11,200 wapo chini ya vifusi. Kwa hiyo mtawanusuru lini?” na mabango mengine yakiwandikwa, “Khilafah itatangaza jihad,” “Khilafah itaikomboa Palestina,” “Khilafah utaitabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu”...
Wakati wote wa matembezi hayo, waliohudhuria waliimba kauli mbiu dhidi ya serikali ya kijamhuri, utawala wa kifalme, na dola ya kitaifa, kama vile “Hakuna jamhuri, hakuna ufalme... Khilafah ya Kiislamu.” Pia waliita miito mengine, kama vile “Netanyahu, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itaregea,” “Ewe Amerika, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itaregea,” “Ewe Mzayuni, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itaregea,” “Enyi majeshi ya Waislamu, jihad iko Palestina,” na “Watawala wameiuza Palestina kwa mamilioni”
Matembezi hayo yalipita katika barabara kuu za mji mkuu zinaoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo yalihitimishwa mbele ya Jumba la Michezo la Manispaa kwa hotuba iliyotolewa na shababu miongoni mwa Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, ambapo alieleza kwamba walioiangusha Gaza ni tawala hizi za kijamhuri na za kifalme. Serikali ya kijamhuri nchini Misri ndio ya kwanza kuwazingira ndugu zetu mjini Gaza, na utawala wa kifalme nchini Jordan ndio unaounga mkono umbilr hilo kupitia ukanda wa ardhini na kulilinda dhidi ya mashambulizi ya Iran. Kwa upande wa utawala wa kijamhuri nchini Uturuki, umesalidia umbile hilo kwa misafara ya ufadhili kupitia bandari, na ndio misimamo hii hii ya fedheha ambayo Imirati na tawala zengine za Kiarabu zilizoanzishwa na Waingereza na Wafaransa katika Mkataba wa Sykes-Picot ndio zilizo chukua. Suluhisho ni yale ambayo dini yetu imetuwajibisha kuyafanya, nayo ni kusimamisha dola ya Khilafah Rashida inayoongozwa na mtu mchamungu na msafi watu wanayepigana nyuma yake na kujilinda kwaye, hivyo anairegesha ardhi ya Isra na Miraj na kuwarudisha Mayahudi wahalifu na kila dhalimu kwenye bonde lenye kina kirefu.
Hivyo basi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendelea na wito wake wa wazi na wa ukaidi katika mazingira haya ambayo watu wa Gaza wanapitia, kwa njaa, mashambulizi ya mabomu, na vitisho vikubwa, pamoja na Waislamu wengine wanaokandamizwa. Inaendelea na wito wake kwa wenye ikhlasi katika majeshi ya Misri, Jordan, Uturuki, Pakistan, na watu wengine wenye nguvu na uwezo, kunusuru dawah ya Uislamu na kusimamisha dola yake, ambayo itaiokoa Gaza, kuikomboa Palestina, kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu ardhini, na kubeba ujumbe wa uongofu na nuru kwa walimwengu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 30 Muharram Tukufu 1446 H sawia na 25 Julai 2025 M
- Picha za Amali ya Matembezi -
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
https://hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/4849.html#sigProId44c0d3ae24
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir