- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Kongamano la kila Mwaka la Khilafah “Kwa Khilafah Tunakabiliana na Udhibiti wa Marekani”

Mnamo Jumamosi 02 Mei 2026 M, Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa kongamano la kila mwaka la Khilafah katika ukumbi wa mikutano na makongamano ulio katika makutano ya Sakiet Ariana katika mji mkuu wa Tunis, lenye kichwa:
“Kufeli kwa Dola ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah”
Kongamano hilo lilizungumzia mada kuu tatu:
1. Mwisho wa Demokrasia na Usasa na Kuanguka kwa Hadhara ya Epstein
2. Uislamu na Khilafah... Kuelekea Mfumo Mpya wa Kimataifa
3. Muungano wa Da'wah na Nusrah na Kuchomoza kwa Khilafah
Kufuatia kampeni kubwa za utangazaji zilizofanywa na mashababu wa hizb kwenye mitandao ya kijamii na kote nchini, ikiwa ni pamoja na kutundika mabango na usambazaji wa mialiko ya kongamano hilo katika wiki iliyotangulia, kumbi hizo mbili zilijaa wahudhuriaji kutoka kote nchini. Kongamano hilo lilifunguliwa kwa usomaji mzuri wa aya kutoka Quran Tukufu, kuanzia mwanzo wa Surah Al-Qasas hadi aya ya 14, zilizosomwa na shababu Muhammad Ali Al-Awni.
Kisha, ustadha Hanan Al-Khamiri kutoka Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia alitoa hotuba yenye kichwa “Mwisho wa Demokrasia na Usasa na Kuanguka kwa Hadhara ya Epstein.”
Hii ilifuatiwa na ujumbe kutoka kwa msimamizi wa kongamano hilo, Ustadh Najm Al-Din Shuaibin, ulioelekezwa kwa watu wa Tunisia haswa na kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla, ukisema kwamba Ummah wa Kiislamu leo una uwezo na rasilimali zote za kusimamisha Khilafah, kama ilivyotabiriwa na Mtume Muhammad (saw).
Ujumbe wa video kutoka Lebanon kutoka kwa Ustadh Ahmad Al-Qasas ulionyeshwa, ukizungumzia Khilafah kama suluhisho pekee linaloweza kuzuia kiburi cha Marekani na kutibua mipango yake katika eneo hili.
Kisha, Ustadh Mundhir Abdullah, mzungumzaji mgeni katika kongamano hilo, alitoa hotuba yenye kichwa “Uislamu na Khilafah: Kuelekea Mfumo Mpya wa Kimataifa.” Na kufuatia baada yake, ujumbe wa video kutoka Palestina ulitangazwa, ukimwonyesha Sheikh Yusuf al-Mukharza akijadili jihad na kutoa wito kwa majeshi kuinusuru Palestina.
Kongamano lilimalizika kwa hotuba ya Ustadh Tariq Rafi' yenye kichwa “Muungano wa Da'wah na Nusrah na Jua Linalochomoza la Khilafah.” Bendera ya Uqab na Liwaa ya Mtume (saw) zilipepea ukumbini, na hotuba zilipigiwa kauli mbiu kutoka kwa hadhira kama vile, “Ewe Amerika, sikiliza... Khilafah yetu itarudi,” “Inueni Bendera ya Uqab, Khilafah imekaribia,” “Hapana mola wa haki ila Mwenyezi Mungu... Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu,” “Hapana mola wa haki ila Mwenyezi Mungu... Khilafah ni utawala wa Mwenyezi Mungu,” na “Hapana mola wa haki ila Mwenyezi Mungu... Khilafah ni faradhi ya Mwenyezi Mungu.”
Kongamano hilo limekuja wakati ambapo Tunisia na ulimwengu wote wa Kiislamu unapitia kutoridhika sana kutokana na hali iliyopo ya umaskini, kutengwa, bei za juu, uhalifu, na kuvunjika kwa familia. Zaidi ya hayo ni msiba na uhalifu unaoendelea dhidi ya binadamu huko Gaza na Sudan. Kongamano hilo lililenga kuonyesha kwa ulimwengu wa Kiislamu kwamba hakuna wokovu isipokuwa kupitia kusimamishwa kwa jengo kubwa la Kiislamu, Khilafah, ambayo Mwenyezi Mungu amewafaradhishia Waislamu. Khilafah hii itasitisha kiburi cha Amerika na umbile la Kizayuni, utaokoa Umma wa Kiislamu, na kukomesha utawala wa ruwaibidha (wafisadi na watepetevu) ambao wamesababisha mateso juu yake kwa miongo kadhaa. Utaongoza ulimwengu wa Kiislamu kutoka kwenye giza la ubepari na dola ya kisasa, pamoja na mifumo yake ya kijamhuri na ya kifalme, hadi kwenye uadilifu na nuru ya mfumo mtukufu wa Kiislamu.
((وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)).
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Jumamosi, 15 Dhu al-Qi'dah 1447 H - 2 Mei 2026 M

- Video ya Amali za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -

- Picha za Amali za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -
https://hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/5332.html#sigProIdb3cc43f05f

- Ualishi na Utangaziaji wa Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -





Alama Ishara za Kongamano la kila Mwaka
#أقيموا_الخلافة
#كيف_تقام_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
#TurudisheniKhilafah



Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir




