- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Semina kwa Anwani “Vipaumbele vya Umma”
Hizb ut Tahrir / Uholanzi ilifanya semina katika mji wa Utrecht wa Uholanzi kwa anwani "Vipaumbele vya Umma", ili kuangazia na kuwasilisha Uislamu kama badali tukufu ya kimfumo inayobeba hukmu zake zinazotatua changamoto na hatari zote kama vile usekula, uzalendo, uhuru, kadhia ya jinsia, na mambo yasiyo ya kawaida na suluki ya aibu iliyotokana nayo.
Jumapili, 01 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 21 Mei 2023 M
Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Semina kwa Anwani “Vipaumbele vya Umma”
Hizb ut Tahrir / Uholanzi ilifanya semina katika mji wa Utrecht wa Uholanzi kwa anwani "Vipaumbele vya Umma", na kwa sababu sisi, kama Waislamu, sawa iwe tunaishi katika nchi za Kiislamu au katika nchi za Magharibi, tunakabiliwa na changamoto nyingi, hatari, na majaribio yasiyokoma ya kutupotosha kutoka katika dini ya Mwenyezi Mungu, na kutoka katika mlango wa kulingania mema na kuamrisha mema na kukataza maovu, imekuwa ni katika wajib, hasa katika ulimwengu ambao Uislamu hautawali, lakini badala yake giza la ubepari fisadi ndilo linalotawala, kuuangazia Uislamu na kuuwasilisha kama badali tukufu ya kimfumo unaobeba hukmu ambazo zinatatua changamoto na hatari zote kama vile usekula, uzalendo, uhuru na kadhia ya jinsia na yanayochipuza kutokana nayo miongoni mwa suluki ya aibu.
Semina hii ilifunguliwa kwa usomaji mzuri wa Qur'an Tukufu, na kufuatiwa na hotuba ya kwanza iliyotolewa na Ndugu Abdul Malik iitwayo “Fiqh ya Vipaumbele” ambapo alizungumzia ufahamu wa kipaumbele katika kuwasilisha hukmu zinazotokea kwa Waislamu hilo ni lazima lipatikane kwa wakati mmoja, na akaeleza kuwa suala la kuweka vipaumbele pindi faradhi zinaposongana haliachiwi akilini, bali Sharia, kwani ndiyo inayoamua ya moja baada ya nyengine kupitia kwa maandiko yake ya wazi yanayoonyesha hilo, au kupitia kwa ijtihad na uvuaji wa mujtahidina ikiwa ya kwanza kutangulizwa haiko wazi.
Kisha akatoa baadhi ya mifano inayoonyesha jinsi Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi, walivyokuwa wakilifahamu vyema suala la vipaumbele na kulitanguliza lile lililo la kwanza. Hayo yalidhihirika pale walipoakhirisha mazishi ya Mtume (saw) pamoja na ukubwa wa faradhi hii, mpaka pale kiapo cha utiifu (bay’ah) kwa Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kilipokamilika na Abu Bakr Al-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, akateuliwa kuwa Khalifa wa Waislamu.
Ama kuhusu hotuba ya pili, ilitolewa na Ustadh Okai Bala, mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi, na ilizingatia kipaumbele cha wajibu kwa Waislamu katika wakati huu, na kwamba kila wakati na hali ina vipaumbele fulani vyenye kuamuliwa na Sharia, kwa mfano pindi zilipokusanywa Hadith za Mtume (saw) kulikuwa na udharura wa hilo kwa sababu ya vifo vya maswahaba wengi na idadi kubwa ya riwaya zilizotungwa na kumzulia yeye (saw), na kuwekwa elimu ya kuchunguzwa dosari (jarh) ya wapokezi na kuadilisha na elimu juu ya wapokezi, ili kuzitakasa Hadith sahihi kutokana na Hadith za kutunga, na vile vile wakati Matartari waliposhambulia na kuharibu Baghdad na Ash-Sham, kipaumbele kilikuwa katika kukabiliana nao na kuwaondoa katika vita vya Ain Jalut, na pia Msikiti wa Al-Aqsa ulipotekwa nyara mikononi mwa Makruseda, kipaumbele kilikuwa ni ukombozi Wake kutoka kwao katika vita vya Hattin, vilivyoongozwa na Salah al-Din al-Ayyubi, Mwenyezi Mungu amrehemu.
Ama hivi leo, wajibu wa Waislamu ni kufanya kazi ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah juu ya faradhi nyengine yoyote; Hii ni kwa sababu kukosekana kwa Khilafah kunamaanisha kusitishwa kwa hukmu nyingi za Sharia katika maisha ya Waislamu, na hukmu za Sharia hazikomei kwenye ibada tu, bali Uislamu ni mfumo kamili ambao kwao ni utatuzi na masuluhisho kwa matatizo yote ya wanadamu, kiuchumi, kijamii, kisiasa na kadhalika.
Ustadh Bala aliwashutumu wale wanaolingania Uislamu kwa mujibu wa yale yanayoafikiana na mfumo wa kisekula yanayolingana na matamanio ya makafiri wa Magharibi, na wala hawaulinganii Uislamu kama alivyouteremsha Mwenyezi Mungu kuwa ni mfumo kamili wa maisha, hivyo basi wanaiwekea mipaka da’wah yao katika kushikamana na Sunnah na Nawafil, ama kuhusu ulinganizi wa faradhi kubwa na kadhia nyeti, wao hawazingatii kamwe! Ustadh Okai Bala alimalizia hotuba yake kwa kuangazia mambo mawili ambayo Waislamu lazima wayaweke juu ya vipaumbele vyote. Ama la kwanza, ni wajibu wao kujua kwamba Uislamu ni mfumo kamili na kwamba ndio badali pekee inayoweza kusuluhisha maisha yao. Jambo la pili ni kwamba wafanye kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kwa kujitahidi kusimamisha dola ya Khilafah ambayo ni taji la faradhi zote kama ilivyoelezwa na Imam Al-Qurtubi Mwenyezi Mungu amrehemu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uholanzi
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/uholanzi/3251.html#sigProIdc15851ae23
Kwa maelezo Zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi