- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Halaqa ya Mjadala Mjini Anatolia Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi
Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi mjini Anatolia.
Wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa ni maustadh; Yilmaz Şilek (mwanachama wa afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Uturuki), Suleyman Ugurlua (Mhariri mkuu wa gazeti la kokludegisim), na Hakki Eran (mwandishi wa gazeti la kokludegisim)
Katika mkutano wetu, ilisisitizwa udharura wa kuwekwa masuluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja kwenye ajenda, na kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na ya asili katika utawala, uchumi, elimu na nyanja za kijamii, na kwamba ni lazima yabainishwe katika kila jambo.
Mkutano wetu ulimalizika kwa hamu na msisitizo juu ya udharura wa kuwekwa mikutano hii ya mashauriano na masuluhisho mara kwa mara katika maeneo yote.
Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa
Jumapili, 12 Rajab Al-Muharram 1443 H sawia na 13 Februari 2022 M
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/uturuki/2167.html#sigProId0cec8aaaa2
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki