- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Halaqa ya Mjadala Mjini Esenyurt Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi
Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", na sanjari na mnasaba wa kumbukumbuka ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Muharram 1342 H, Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi mjini Esenyurt katika jimbo la Istanbul.
Wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa ni maustadh; Ali Gurgun (Msimamizi wa jarida la kokludegisim mjini Esenyurt), Muhammedu Kar (mkuu wa Afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Uturuki), Muhammed Emin Yildirim (mwanachama wa afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Uturuki), na Dkt. Abdurrahim Shin (imamu na khatibu).
Katika mkutano wetu, ilisisitizwa udharura wa kuwekwa masuluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja kwenye ajenda, na kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na ya asili katika utawala, uchumi, elimu na nyanja za kijamii, na kwamba ni lazima yabainishwe katika kila jambo.
Mkutano wetu ulimalizika kwa hamu na msisitizo juu ya udharura wa kuwekwa mikutano hii ya mashauriano na masuluhisho mara kwa mara katika maeneo yote.
Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa
Jumapili, 12 Rajab Al-Muharram 1443 H sawia na 13 Februari 2022 M
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/uturuki/2170.html#sigProId87b2ae0217
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki