Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Kongamano la Kiuchumi Mjini Inegol "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi"

Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano la kiuchumi mjini Inegol katika jimbo la Bursa chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", sanjari na mnasaba wa kumbukumbuka ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Muharram 1342 H.

Ambapo kongamano lilianza kwa utangulizi wa mwakilishi wa jarida la Kokludegisim katika jimbo la Bursa Ustadh Muhammed Steinbodek, ikifuatiwa na usomaji mzuri wa aya za Quran Tukufu na Ndugu Muhammad.

Kisha kalima ya ufunguzi ikatolewa na Ustadh Mehmet Amin Yildirim, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki, ambapo alieleza kwamba migogoro inaangukia kila mtu, haswa serikali na wasimamizi, na akasema kwamba wasimamizi wamepuuza jukumu hili. Kwa mara nyingine tena, akibainisha kwamba tunachotakiwa kuondokana na migogoro hii ni Uislamu mtukufu, Yildirim alieleza kuwa Uislamu ni dini na mfumo utakaotoa ufumbuzi wa matatizo yatakayojitokeza hadi mwisho wa dunia, sawa na ulivyotoa ufumbuzi kwa matatizo yote katika kipindi cha miaka 1,300 iliyopita.

Baada ya kalima ya Ustadh Mehmet Amin Yildirim, Ustadh Musa Beyoglu (mmoja wa waandishi wa jarida la Kokludegisim) anayejulikana kwa kitabu chake "Ibada Inayoongoza kwenye Ushindi" alitoa kalima yake ambayo alisema kwamba Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki imetayarisha Utafiti wenye kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu ya Migogoro ya Kiuchumi katika Vipengee 10." Kama sharti la uwajibikaji huo, alielezea katika kalima yake yenye kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu ya migogoro ya kiuchumi katika vipengee kumi" sababu halisi za migogoro tunayopitia na masuluhisho yake ya Kiislamu.

Kisha ikaja kalima ya Ustadh Mahmud Kar (Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki), ambayo ilikuwa na anwani: “Je, bado tungali tunatafuta suluhisho la mgogoro ndani ya utekelezaji wa mfumo kikatili wa ubepari, au ndani ya hukmu safi za Kiislamu?” Alitoa takwimu kujibu swali hilo na akagusia masuluhisho ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na namna ya kuutabikisha. Kar aliweka wazi kwa mifano kutoka katika historia tukufu ya Kiislamu kwamba ardhi hizi kamwe hazikupata masaibu na umasikini kwa muda wa karne 13, na kwamba kuokoka kutokana na mgogoro na matatizo ya sasa kutawezekana tu kupitia nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu haswa, na mfumo wa Kiislamu kwa jumla.

Pamoja na mawasilisho yote katika kongamano hili lililofanyika Bursa/Inegol, ukweli ulisisitizwa kwamba wokovu pekee kwa wanadamu wanaokumbwa na janga la migogoro ya kimaadili na kiuchumi kutokana na urasilimali uliofilisika ni mfumo wa uchumi wa Kiislamu na hukmu za Uislamu. Kongamano hilo lilihitimisha kazi yake kwa kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa moyo mmoja tuone na tuishi pamoja katika kivuli cha Dola ya Khilafah Rashida - itakayosimama hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu - itakayotabikisha mfumo wa Kiislamu.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumamosi, 18 Rajab Al-Muharram 1443 H sawia na 19 Februari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu