Jumatatu, 23 Shawwal 1446 | 2025/04/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Je, Kura ya Kutokuwa na Imani ni Mchakato wa Kisiasa au wa Kimahakama?

Wabunge nchini Kenya wameanza mchakato wa kumwondoa naibu rais wa nchi hii afisini. Wale wanaounga mkono juhudi hizo wanamshutumu Rigathi Gachagua kwa kuhusika katika maandamano ya Juni ya kupinga serikali - ambayo yaligeuka kuwa mabaya - pamoja na kuhusika katika ufisadi, kuhujumu serikali na kuendeleza siasa za mgawanyiko wa kikabila. Naibu rais amepuuzilia mbali madai hayo.

Soma zaidi...

Sintofahamu ya GISB: Nukta ya Mabadiliko ya Kushughulikia Upotofu na Kuregesha Khilafah

Katika wiki za hivi karibuni, Global Ikhwan Sdn Bhd (GISB) imekabiliwa na uchunguzi mkali kutoka kwa mamlaka kufuatia wasiwasi wa muda mrefu juu ya desturi zake potovu. Ingawa ripoti zilikuwa zimewasilishwa dhidi ya GISB mapema zaidi, hatua za hivi majuzi za polisi zinaashiria hatua ya kwanza muhimu ya kupunguza shughuli za kundi hili. GISB, ambayo mizizi yake inatoka kwenye vuguvugu la Al-Arqam ambalo sasa limezimika, imevutia umakini wa watu wengi kwa kulingania vitendo vya upotofu vya Aurad Muhammadiyah na madai ya utovu wa nidhamu, hasa katika uendeshaji wa nyumba za misaada.

Soma zaidi...

Je, Tunapaswa Kuzingatia Maneno Yako Mazuri au Matendo Yako Mabaya!

Katika hotuba yake katika Programu ya Ufunguzi wa Wiki ya Mawlid al-Nabi Rais Erdoğan alisema, “Mtu pekee katika ulimwengu huu ambaye tunamuiga, tunafuata nyayo zake na ambaye tunajitolea maisha yetu kwake ni Mtume wetu wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye kiongozi wetu na kipenzi chetu ambaye tutakufa kwa ajili yake. Mola wetu atujaalie tutembee katika nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu, tujenge shakhsiya yetu kwa maisha yake, na tuwe na maadili mema ya kupigiwa mfano.”

Soma zaidi...

Mabadiliko Ndio Fikra Inayopiganiwa Zaidi katika Historia

Barabara za Kenya zilisalia kuwa uwanja wa vita huku maandamano, yaliyochochewa na ongezeko la ushuru lenye utata, yakibadilika na kuwa kilio kikubwa dhidi ya tofauti za kiuchumi zilizokita mizizi na kukosekana kwa uwajibikaji wa serikali. Mstari wa mbele wa vuguvugu hili ni kizazi cha vijana wa Kenya, wanaokataa kunyamazishwa licha ya kukabiliwa na msako mkali wa polisi.

Soma zaidi...

Uzbekistan: Faini za Mamilioni ya Soum kwa Kuwafunza Watoto Uislamu

Mnamo Juni 25, wawakilishi wa Oliy Majlis ya Jamhuri ya Uzbekistan walipitisha katika usomaji wa kwanza mswada unaokataza wazazi kupeleka watoto wao kusoma katika mashirika ya kidini ambayo hayajasajiliwa au kwa watu binafsi bila kibali kinachofaa. Mswada huo ulianzishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Uzbekistan.

Soma zaidi...

Mwito wa Mabadiliko: Uislamu Mfumo pekee Usiocheza Shere na Kuhujumu Maisha ya Watu

Kenya, imekumbwa na maandamano makubwa katika masiku ya hivi majuzi baada ya bunge kupitisha mswada wa kuongeza ushuru – ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kila siku kama vile mafuta ya kupikia, nepi, na mkate – kwa idadi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumko wa bei na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira. Rais Ruto alikataa kutia saini mswada huo baada ya maandamano makubwa ambayo kufikia sasa watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu