Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mizozo ya Kibiashara ya Amerika na China Haina Uhusiano Wowote na Kuthamini Haki za Wanawake Kiislamu

Habari:

Mnamo Septemba 14, 2020 CNBC iliripoti juu ya tathmini ya Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la sovereign wealth Choi Heenam juu ya Shirika la Uwekezaji la Korea. Alisema kuwa "wawekezaji hawapaswi" kuwa na msimamo mkali" juu ya masoko hata ikiwa uhasama kati ya Amerika na China unaendelea kuongezeka" kama "kwani ni mzozo wa kiubwana unaotokana na matatizo ya kimuundo kuliko maslahi ya kisiasa ... itaendelea kuwa kuwa ni kitanzi kwa uchumi wa ulimwengu, lakini hatimaye, sio haribifu ”.

Maoni:

Mnamo Juni 2020 New York, mamlaka za majimbo zilikamata shehena ya tani 13 za nywele fuma za binadamu zinazoshukiwa kuchukuliwa na kuundwa kutokana na wanawake wa Uyghur waliowekwa kizuizini katika kambi za mahabusu za Wachina. Forodha ya Amerika na Ulinzi wa Mipaka (CBP). Mnamo Mei 1, 2020, vikwazo viliwekwa kwa bidhaa za nywele zilizotengezwa na kampuni ya Vifaa vya Nywele ya Hetian Haolin baada ya kuhusishwa na kuwafanyisha kazi ya kulazima Waislamu wa Uyghur. Cha kutisha zaidi, ushahidi kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu wameshuku kuwa chanzo cha nywele hizo kinaweza kuwa ni nywele zilizonyolewa kutoka kwa maelfu ya wanawake wa Kiislamu waliouawa ambao wananyofolewa sehemu zao za mwili, kama wanyama.

Ukweli kwamba wachambuzi wakuu wa uchumi wanatambua kuwa michezo ya kisiasa inachezwa huku ukiukwaji mbaya zaidi wa haki za binadamu ukionyesha kwamba kwa kweli "biashara ni kama kawaida" kwa serikali halifu zaidi ulimwenguni. Hatuwezi kamwe kutarajia haki za binadamu kuchukua nafasi ya kwanza juu ya faida ya kifedha chini ya sheria za uajiri katika Urasilimali. Ukweli kwamba eneo salama la ukimya na ukosefu wa nia ya kuzichunguza kambi za mateso ambazo zinaweza kuonekana kutoka angani inatoa ujumbe wazi kwamba Waislamu wa China hawana matumaini kabisa ya kuokolewa kutokana na chuki na dhulma za serikali zao.

Viongozi wetu wenyewe wa Kiislamu wanafumbia macho, wanaongeza ununuzi wao wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa kampuni za silaha za Kimagharibi ili kuokoa uchumi wa wale wanaounga mkono mauaji ya Waislamu.

Majeshi yao na vifaa vyao vinapeanwa kwa hiari kama inavyoeleweka kuwa zitatumika nchini Yemen, Syria na dhidi ya Waislamu wowote kama inavyohitajika.

Hatuwezi kuwavumilia wasaliti hawa wa haki na kunyamazia kimya mateso na unyofoaji wa ndugu na dada zetu wapendwa!

Hatuwezi kukubali kuishi chini ya kivuli cha uovu huu wa kiulimwengu unaohubiri uhuru huku ukikubali magereza wazi nchini China na Palestina.

Tunatoa wito kwa Waislamu wote kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah kama alivyoamuru Mwenyezi Mungu (swt) kuwa na uongozi wa kweli wa Quran na Sunnah ili kuukomboa Ummah wetu mpendwa. Tunafanya hivi bila woga au kuchelewesha kwani ni hili hitajio la haraka zaidi la zama zetu na kwa njia hii tunajitofautisha na watu waovu katika Dunia hii.

(كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aali Imran: 110]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 28 Septemba 2020 21:55

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu