Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Karimov Amekufa lakini Udhalimu Wake Ungali Unaendelea Hadi Leo!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Runinga ya Uzbek ilitangaza kipindi mnamo 17/10/2020 kwa jina "Hatima ya Wasio na Shukrani", ambacho ni ripoti ya habari inayozungumzia juu ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir ambao walikaa gerezani miaka 18 na kufuatia kuachiliwa kwao waregelea tena ulinganizi wao wa kusimamisha Khilafah ya Kiislamu. Mashababu hao wakati wa kuachiliwa kwao, kama kipindi hicho kinavyodai, waliwasiliana kupitia Facebook na mtu anayeitwa Mahmoud Abdul Mu’omin na kuchukua habari kutoka kwake juu ya kazi ya Hizb na amali zake. Jina langu, Islam Abu Khalil, lilitajwa na kutuhumiwa kufadhili mara kwa mara na kutuma pesa kwa Mashababu wa Dawah huko, na waliituhumu Hizb na kuitaja kama ya kigaidi wakati hapo awali serikali ya Uzbek ilikuwa ikiisifu kama yenye msimamo mkali.

Maoni:

Kipindi hicho ni kazi ya ujasusi wa Uzbek, na ni kutokana na sera ya mhalifu Karimov, ambaye alikuwa dhalimu na aliwaua Mashababu wengi wa Hizb ut Tahrir kwa miaka mingi ya utawala wake, na sasa serikali mpya inafuata nyayo za mhalifu Karimov katika dhulma yake dhidi ya Mashababu na uzushi wake dhidi ya wabebaji wa Dawah. Hii hapa, baada ya kumalizika kwa hukumu ya Mashababu waliotumikia miongo kadhaa katika magereza yake, inawakamata tena baada ya kurudi katika kazi yao ya kawaida katika Ummah wakibeba ulinganizi na kufanya kazi kuregesha mfumo kamili maisha wa Kiislamu ambao kwao Waislamu wa Uzbekistan na ulimwengu wote hutukuzwa. Na hii hapa serikali inarudi kwenye sera yake ya msimamo mkali na ya kigaidi, kuwakamata, kuwachukua filamu na kuwatisha na kuwalazimisha wazungumze dhidi ya Hizb na Dawah, na kuizulia Hizb na Mashababu wake, na kutuhumu kwa kutuma pesa nyingi kwa Mashababu huko, na huu ni uongo na uzushi. Sijatuma pesa kwa mtu mwingine yeyote isipokuwa familia yangu ambayo inaishi chini ya ukandamizaji wa serikali hii ambayo mara kwa mara, inakwenda nyumbani kwetu, inavunja na kuuliza kunihusu, labda itanipata na kunikamata. [مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُون] "Mna nini? Mnahukumu vipi?" [Al-Qalam: 36].

Ewe Serikali ya Uzbekistan:

Kutoka kwa yote mnayoyafanya ya kuzusha uongo na kashfa dhidi ya Dawah na kuwatesa Mashababu wake na kutekeleza ugaidi dhidi yao hayataizuia Dawah na hayataweza kuikomesha, kwani inatokama na Aqeedah ya Waislamu wa Uzbekistan. Serikali ya zamani, serikali ya Karimov ilijaribu na haikuweza, kwa sababu Dawah hii ni ya Mwenyezi Mungu na kwa usuluhishi wa sheria ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu (swt) anailinda na wale wanaoibeba na kuitafuta. Na watu wa Uzbekistan wanajua ukweli wa Hizb ut Tahrir, na Ummah na ulimwengu mzima wanajua kuwa ni chama cha kisiasa kinachofanya kazi kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah wa pili kwa njia ya Utume. Kwa hivyo, kila mnavyojaribu kuipotosha na kuupotosha wito wake, na kuwatisha Mashababu wake na uzushi wenu dhidi yake, itabaki kuwa kiongozi asiyewadanganya watu wake, na itabaki kuwa mbebaji wa bendera ya Uislamu na utekelezaji katika maisha, wanaotafuta kuangamiza viti vya enzi vya wakandamizaji na wenye itikadi kali kutokana na serikali za kigaidi nchini Uzbekistan na katika maeneo ya mashariki na magharibi ya ulimwengu.

Enyi Watu wetu wa Uzbekistan:

Je! Hamtamani maisha mema, yenye hadhi, na ya haki yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na ambaye ameridhika nanyi? Mtakaa kimya hadi lini kuhusu uonevu wa watawala na nidhamu zao za kirasilimali zilizooza?! Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi Waislamu wafanyikazi wenye ikhlasi wa Khilafah; na Mtume wake (saw) alitoa bishara njema kuihusu. Kwa hivyo, ni wakati kwenu kufanya kazi kufikia ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Nabii Wake (saw), na ni nani mkweli zaidi na anayetimiza zaidi ahadi na agano lake kuliko Mwenyezi Mungu.

]وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao …” [An-Nur: 55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Islam Abu Khalil

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu