Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni
Ulanguzi wa Binadamu: Sekta ya Uhalifu ya Kirasilimali Iliyo Nawiri Ambayo Khilafah Itaing’oa

Habari:

Mmoja kati ya waathiriwa sita wanao languliwa kwa ajili ya kufanyishwa kazi kwa lazima, dhulma ya kimapenzi na sababu nyinginezo kama vile omba omba nchini Kenya ni mtoto, shirika la uchunguzi la ‘Nation Newsplex’ limefichua. Thuluthi mbili za waathiriwa wa ulanguzi wa binadamu, pia unaojulikana kama utumwa mamboleo, wana umri kati ya miaka 18-29, asilimia 17 nyingine wana umri kati ya miaka 30 na 47 huku chini ya asilimia 1 wakiwa na zaidi ya miaka 47, inaashiria tarakimu kutoka kwa kituo cha Taarifa za Ushirikiano katika Kupambana na Ulanguzi wa binadamu. Imetajwa kuwa Kenya inasalia kuwa chimbuko, nukta ya kati ya usafiri na mafikio ya watu wanaosibiwa na ulanguzi wa ngono na kufanyishwa kazi kwa lazima. [Daily Nation Julai 29, 2019]

Maoni:

Ulanguzi wa binadamu ni uhalifu dhidi ya wanadamu wa kuogofya unao fafanuliwa kama biashara ya watu kwa lengo la kufanyishwa kazi ya lazima, utumwa wa ngono, au biashara ya dhulma ya kingono kwa walanguzi au wengineo. Kote ulimwenguni, watoto ndio wanaochukua sehemu kubwa (asilimia 30) ya waathiriwa walio gunduliwa, takriban maradufu ya mgao wa Kenya, huku wasichana wakiwa wengi zaidi kuliko wavulana. Ripoti ya Kiulimwengu juu ya Ulanguzi wa Watu ya 2018 ya Afisi ya Umoja wa Mataifa juu ya Mihadarati na Uhalifu (UNODC) inaeleza. Kufikia 2014, kazi ya kulazimishwa pekee ilizalisha kadiri ya faida ya dolari bilioni 150 kwa mwaka. [Shirika la Wafanyikazi la Kimataifa (ILO)]. Mnamo 2012, Shirika hilo lilikadiria kuwa waathiriwa milioni 21 wamekwama katika utumwa mamboleo. Kati ya hawa, milioni 14.2 (asilimia 68) walidhulumiwa kwa ajili ya kazi, milioni 4.5 (asilimia 22) walidhulumiwa kingono, na milioni 2.2 (asilimia 10) walidhulumiwa katika kazi ya lazima iliyo shinikizwa na serikali.

Ukweli ni kuwa biashara ya binadamu ni mojawapo ya mpangilio wa uhalifu wa kiulimwengu unaokuwa kwa kasi mno, idadi ya waathiriwa ni kubwa mno kushinda tarakimu zilizo tajwa. Huku ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Ulimwengu dhidi ya Ulanguzi wa Watu Julai 30 kila mwaka, ulanguzi wa binadamu ungali unaendelea kuteka umakinifu wa vyombo vya habari vya kiulimwengu kama mojawapo ya uhalifu unaoogofya. Ni wazi kuwa, ulimwengu umeathirika na ulanguzi wa binadamu, ima kama nchi unakoanzia, nukta ya kati ya usafiri, au mafikio ya waathiriwa. Walanguzi kote duniani wanaendelea kuwalenga wanawake na wasichana kwa ajili ya dhulma za kingono na kazi ya kulazimishwa. Ukubwa wa sera kuu tatu zilizo tabanniwa na Muongozo wa Sera Dhidi ya Ulanguzi unao tathmini juhudi za kiserikali dhidi ya ulanguzi; (3ps); Kuwashtaki wahalifu wa ulanguzi wa binadamu, Kuzuia ulanguzi wa binadamu, Kuwalinda waathiriwa wa ulanguzi wa binadamu bado hayajakomesha uhalifu huu. Kampeni dhidi ya ulanguzi imekosa nukta muhimu: Kupigana na dalili za ugonjwa badala ya kupigana na chanzo chake!

Chanzo cha kitendo hiki cha kuogofya kimetokana na:

Sifa ya ukosefu wa utu: Watu wengi wanatoroka makwao ili kutafuta maisha mwanana. Lakini kiu yao hii ya kutafuta usaidizi hupatilizwa na baadhi ya watu kujinufaisha kibinafsi. Kwa kuwa kipimo cha urasilimali ni manufaa, binadamu walafi hupatiliza fursa ya hali hii ya dhiki kujipatia faida. Huu ndio msimamo wa Demokrasia ambapo mateso na dhiki ya wengine hugeuzwa kuwa manufaa kwa wengine!

Nidhamu mbovu ya kiuchumi ya kirasilimali: Muundo wa uchumi wa kirasilimali huziweka rasilimali mikononi mwa warasilmali wachache na washirika wao na ugavi wa mapato usioingia akilini hivyo ukiwaacha mamilioni kutekesa katika lindi la umasikini. Hii imewalazimu watu hususan kutoka katika ‘nchi za ulimwengu wa tatu’ kuhamia nchi nyingine zinazo dhaniwa kuwa bora kama vile Mashariki ya Kati na nchi za magharibi ili kutafuta ‘maisha mazuri’.

Ukatili wa serikali za kisekula: Viongozi wa kiulimwengu wakiwemo viongozi Waislamu hawajali watu wao. Ni ukweli usiopingika kuwa watoto, wanawake na wazee ndio waathiriwa wa vita. Nchi za kimagharibi pamoja na vibaraka wao wanaendelea na mashambulizi katika ardhi za Waislamu. Mauwaji katika Ardhi Tukufu ya Palestina, ambako majeshi ya Kiyahudi yanaendelea kuwaweka kizuizini watoto na mama zao, Waislamu wa Uyghur wanao lazimishwa kuingia katika “kambi za kisiasa kwa ajili ya kugeuzwa fikra zao” nchini China na mauwaji ya utakaso wa kikabila wa Rohingya nchini Myanmar! Kutokana na vitendo hivi vya kinyama vya serikali hizi dhalimu za kisekula, mamilioni ya watu wameishia katika kambi za wakimbizi na kusibiwa na unyama.

Haya ndio mambo makuu yanayo pelekea ulanguzi wa binadamu, ambayo ulimwengu mzima unajua hayawezekani kutokea isipokuwa kwa usaidizi wa mamlaka makuu kote ulimwenguni. Ni ukweli usiopingika kuwa watoto, wanawake na wanaume wanaweza tu kukumbwa na unyama huu na kukiukwa haki zao kwa kukosekana nidhamu ya kuwalinda. Nidhamu hiyo ilikuwa na itakuwa Khilafah pekee kwa Njia ya Utume. Chini ya Khilafah, uchumi hupelekwa kwa msingi wa nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu inayoweka sera imara za kiuchumi zinazo lenga kuweka ugavi stahiki wa mali, ili mahitaji msingi ya watu wote yakidhiwe hivyo basi kutatua umasikini. Aina zote za dhulma na unyanyasaji wa binadamu zitamalizwa kwa kuwa Khilafah inayachukulia maisha ya wanadamu kuwa matukufu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:18

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu