Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Idadi Kubwa ya Wafungwa wa Kisiasa Nchini Urusi ni Mashabab wa Hizb ut Tahrir!

Habari:

Mnamo 14 Juni mtandao wa IA “Memo.ru” uliripoti: “Huku Kombe la Dunia likielekea kufanyika nchini Urusi, “Memorial” ilichapisha orodha ya wafungwa wa kisiasa. Orodha ya wale walioteswa kuhusiana na kupatikana kwa haki ya uhuru wa kuabudu na kujinasibisha na dini ilikuwa kutoka watu 97 mpaka watu 108. Idadi kubwa ya wale ambao majina yao yalikuwemo ndani ya orodha hii wanatuhumiwa kushiriki ndani ya harakati ya “Hizb ut Tahrir al-Islami”, iliyotangazwa kuwa ya kigaidi nchini Urusi pasi na ushahidi wowote – hawa ndio walioshtakiwa katika kesi mbili jijini Moscow na Bashkortostan; Aidar Aydarbekov, Radik Imangulov, Sukhrob Ironov, Mirzobahovaddin Kurbonov, Nail Miniakhmetov, Akmalchon Numonchonov, Maxim Puigin, Naimjon Khodzhaev, Albert Shafiev; na Nariman Memedeminov, mwanaharakati wa Kitartari wa Crimea aliyetuhumiwa kwa kesi sawa na hii. Kuna watu wapatao 158 katika orodha tunazozichapisha leo: 50 kati yao wamo ndani ya orodha jumla ya wafungwa wa kisiasa, 108 – wamo ndani ya orodha ya watu walionyimwa uhuru wao kuhusiana na kupata haki ya uhuru wa kuabudu.”

Maoni:

Kuna Mashabab 237 ambao kwa sasa wamenyimwa uhuru kutokana na kesi za Hizb ut Tahrir kwa jumla katika orodha ya Memorial. Katika orodha hio kuna wanawake pia. Mashabab wanahukumiwa vifungo visivyo na masharti vya muda mpaka wa miaka 19 gerezani. Leo, Mashabab 20 wanahukumiwa mjini Bashkiria. Kiongozi wa mashtaka ametaka Mashabab hawa wahukumiwe miaka 25 gerezani na faini ya ruble elfu 500.   

Urusi katili wa muda mrefu imekuwa ikijiorodhesha kama adui wa Uislamu na Waislamu. Tukiiangalia historia kwa haraka, tutaliona hilo, tangu karne ya 16, kiongozi muovu, Tsar Ivan, alizinyakua ardhi za Waislamu – Kazan, Astrakhan na Siberia Khanates. Walipoteka miji, makatili hawa hawakuwasaza wanawake, wazee, wala watoto; walivamia miji na kuuwa maelfu ya Waislamu.  

Kampeni za kijeshi za makatili hawa katika ardhi za Waislamu ziliendelea katika karne za 17-18, haya yalitokea katika Caucasus. Karne ya 19 iligubikwa na vita dhidi ya Khilafah ya Kiuthmani. Udikteta mpya ulioundwa wa ukomunisti mwanzoni wa karne ya 20 ndani ya Umoja wa Jamhuri Huru za Kisovieti (USSR), juu ya msingi wa fikra ya mada, uliendeleza vita dhidi ya Uislamu na Waislamu katika eneo la Asia ya Kati. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, serikali ya makafiri wa kikomunisti ilitekeleza ufurushaji mkubwa wa Waislamu Crimea na Caucasus. Matartari wa Crimea, wachechnia, Waingush, Wadagestani wote walipelekwa eneo la Asia ya Kati. Katika eneo la Asia ya Kati lenyewe, maelfu ya Waislamu waliuwawa, wakiwemo wengi wa maulama wa dini na wasomi.

Sera hii ya chuki kwa Uislamu na Waislamu inaendelea hadi leo. Idara zinawatesa Waislamu wa Urusi kwa ukatili maalumu wa hali ya juu, hususan Mashabab wa Hizb ut Tahrir. Ili kumkamata Shab mmoja wa Hizb ut Tahrir utawala huu wa kinyama hutuma takriban polisi 20 waliojihami kwa silaha kochokocho wakivalia sare maalumu na viziba uso. Hakuna utawala wa nchi yoyote nyengine huituhumu Hizb ut Tahrir kuwa harakati ya kigaidi, isipokuwa idara za Urusi. Hakuna idara katika nchi yoyote nyengine ulimwenguni inayoweza kupitisha hukumu juu ya Mashabab wa Hizb ut Tahrir ya kuanzia miaka 15 hadi 20 gerezani. Hii ni ishara kuwa utawala wa kinyama wa Urusi inauogopa Uislamu na neno la haki kutoka kwa Mashabab wa Hizb ut Tahrir!

Hivyo basi, msimamo wa Waislamu kuhusiana na utawala katili wa Urusi unapaswa kuwa wazi na wa kukatikiwa. Waislamu wanakabiliana na adui kwa sura ya serikali ya Urusi, ambayo inawatesa Waislamu sio tu nchini Urusi pekee, bali pia nchini Syria, Asia ya Kati na sehemu nyenginezo ulimwenguni.

Ukombozi wa Waislamu wa Urusi, Asia ya Kati na nchi nyenginezo kutokana na uadui wa kinyama wa idara za Urusi uko kwa sura ya kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw), nao ni, kurudisha tena dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Haya ni mapambano ya kimfumo na ya kisiasa pamoja na Hizb ut Tahrir dhidi ya serikali za madhalimu na makafiri.

Kwa kurudisha tena dola tukufu, Khilafah, inayoongozwa na mtawala mwema, Waislamu watapata ngao itakayowalinda Waislamu wote duniani kutokana na mateso ya wakoloni makafiri na vibaraka wao, usoni mwa watawala fisidifu wa Waislamu. Kama alivyosema kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw):

«إنما الإمام جنة يقاتل من ورائه و يتقى به»

“Hakika Imam ni ngao, nyuma yake watu hupigana na kujilinda.” Hadith hii imesimuliwa na Imam Muslim.”

Na twamuomba Allah atunusuru.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:57

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu