Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mwaliko wa Rais wa Umbile Vamizi la Kiyahudi nchini Uturuki ni Uhalifu Mkubwa na Usaliti

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Kwa mujibu wa mwaliko wa rais Erdogan, rais wa ile inayoitwa Israel Herzog aliwasili jijini Ankara kufanya mazungumzo rasmi.

Maoni:

Rais wa umbile vamizi la Kiyahudi Rais Herzog, alizuru Uturuki kufanya mawasiliano rasmi. Ziara hiyo ilifanyika kwa mwaliko wa Rais Erdogan. Wakati wa mkutano huo, hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuendeleza ushirikiano kati ya Uturuki na "Israel" zilichukuliwa ambapo masuala ya sasa ya kieneo na kimataifa yalijadiliwa.

Herzog, anayejulikana kwa ugaidi wake, amekaribishwa kwa sherehe ya kiserikali kana kwamba yeye sio mvamizi. Huku damu ya watoto wachanga wa Aqsa na Gaza ikiwa bado haijakauka, Erdogan alipiga picha za upendo na mkuu wa gaidi hilo.

Muuaji Herzog, Kafiri na fedheha yake, mkuu wa umbile la Kiyahudi, alikaribishwa kwa zulia jekundu nchini Uturuki. Alikanyaga eneo la Uturuki huku miguu yake ikiwa imepakwa damu za ndugu zetu Waislamu wa Palestina. Tena kwa mikono yake ilojaa damu na michafu iliwapa mikono viongozi Waislamu nchini Uturuki.

Lakini, yule anayeitwa Rais wa umbile nyang'anyi la Kiyahudi Herzog, ambaye pia ni mwakilishi wa umbile hilo la kijambazi lililolipua watoto wasio na hatia kwenye pwani ya Gaza, kuwaua Waislamu kwenye Meli ya Mavi Marmara mithili ya maharamia katika Bahari ya Mediterania, alikuja Uturuki kwa mwaliko rasmi, kufanya mazungumzo hasa na Rais Erdogan na mamlaka kana kwamba mambo haya yote kamwe hayakutokea.

Kadhalika, Herzog, Rais wa ile nchi inayoitwa "Israeli", aliyekuja Uturuki kwa mwaliko rasmi wa Rais Erdogan, ni mwakilishi wa viumbe waoga na wakuchukiza ambao huweka vizuizi pambizoni nao kila mwaka wakati wa Ramadhan na kuwakataza Waislamu kuingia katika Msikiti wa Aqsa, kuwazuia kufanya ibada na kumwaga damu mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa visingizio tofauti tofauti kila mwaka. Mtu huyu hana tofauti na watangulizi wake, Netanyahu, Sharon na Peres.

Lakini la kudhalilisha zaidi kuliko hili ni kwamba uwepo wa Mayahudi Wavamizi walisoma Surah Inshirah kwenye mkutano wa kundi la Rais Erdogan kabla ya Rais Herzog kukanyaga nchini Uturuki na miguu yake michafu. Hata hivyo, mtawala anayemcha Mwenyezi Mungu alipaswa kusoma aya hii badala ya Surah Inshirah:

لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُواْ الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُواْ﴿

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Al-Maidah: 82].

Si kitambo, rais Erdogan ambaye alitamka maneno yafuatayo ya kifasihi "Hatua ambazo İsrael inachukua sio tu kwa sababu ya kadhia ya watoto 3. Dola inayojua vyema kuua watoto wachanga bila shaka ni Israel. Nilitaja hili huko Davos. Waliua watoto ufuoni. Lakini wanadamu ni wazembe tu. Maadamu niko kazini, kwamwe sitakuwa na mawazo chanya yoyote na Israel. Quds ni mstari wetu mwekundu” pia alimkaribisha rais wa Israel kwa zulia jekundu. Kwa njia ile ile alivyoifanya damu ya Waislamu kuwa mada ya mazungumzo kwa manufaa ya Waamerika na Mayahudi. Aliitoa sadaka Ardhi Tukufu kwa sera ya "usawazalishaji mahusiano".

Ewe Erdogan!

Hakuna kheri kwako kushirikiana kimkakati na maadui dhahiri wa Uislamu na Waislamu, bali ni uovu.

Je, vilio vya wanawake, mtiririko wa machozi ya watoto, maombolezo ya waliofiwa na wapendwa wao, na damu ya mashahidi kamwe havijaifanya nafsi yako kuuma pindi ulipowakaribisha katika ardhi yetu?

Je, kamwe hujawahi kumuogopa Mwenyezi Mungu wakati ulipo kamata mikono yenye damu ya wauaji huku damu za ndugu zetu waliouawa katika ua wa Msikiti wa Al-Aqsa zikiwa hazijakauka mikononi mwao?

Basi tunakukabili kwa matamshi ya Mtume Muhammad (saw):

 «إذَا لَمْ تَسْتَحِ فَاصْنَعْ مَا شِئْت»“Ikiwa huna haya, basi fanya unavyotaka.”

Hata kama tunajua kuwa hili hutalifanya, tutakuambia la kufanya:

Unachotakiwa kufanya sio kuwakaribisha wauaji wa Waislamu na kuvamia ardhi zetu, bali ni kuwafukuza.

Futilia mbali mikataba yote ya uhaini iliyotiwa saini na Mayahudi! Komesha mahusiano yote na hii inayoitwa dola  ya “Israel” na uweke vikwaz vitakavyowatikisa! Wafukuze mabalozi wa umbile la Kiyahudi, afisi ndogo za ubalozi, na mashirika ya kijasusi kutoka nchini! Hamasisha majeshi yatakayowaondoa Mayahudi wote kutoka katika ardhi ya Palestina ili kutatua tatizo katika ardhi yetu!

Ni wakati wa kuhamasisha majeshi badala ya jumbe zisizo na athari za kulaani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz ÇELİK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu