Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watoto wa Kiislamu ndio Walengwa wa Michezo ya Bunduki ya Maadui wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Umbile la Kiyahudi linasema vikosi vyake vinaonekana kumuua bila kukusudia msichana mmoja wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 16 wakati wa mapigano ya bunduki na wanamgambo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Mwili wa Jana Zakarneh ulipatikana kwenye paa la nyumba yake huko Jenin baada ya mapigano ya risasi mnamo siku ya Jumapili usiku. Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh aliituhumu "Israel" kwa kumuua kijana huyo "kikatili." Zakarneh ni mmoja wa Wapalestina wachanga zaidi waliouawa mwaka huu.

Maoni:

Maoni ya kushutumu ya Waziri Mkuu Shtayyeh yanastahili kutotambuliwa kwani yeye mwenyewe ni mshirika wa mauaji na ukandamizaji wa Ummah wetu. Hatoi suluhisho la Uislamu kwa muundo wa Khilafah kama Mtume (saw) alivyoamuru. Kukubali kwake kuwa kiongozi katika mazingira ambayo ni kinyume na Quran na Sunnah ni kosa lenyewe. Mwenyezi Mungu (swt) alikataza kuwepo kwa muundo mzima wa kijamii na kisiasa wa eneo hili, lakini "kazi" yake ni kuhifadhi Haram hii kama kiongozi wa kirongo wa kuzungumza kwa niaba ya Waislamu. Hatutoi ridhaa yetu kwa taarifa zozote za Mamlaka ya Palestina, utiaji saini wa makubaliano au kura za imani. Tunasimama na hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee kwa kuwa tunaogopa kukutana naye Siku ya Kiyama. Ufyatuliaji risasi kiholela na kuwalenga watoto wetu kwa silaha ni jambo la kawaida la kila siku ambalo sio bahati mbaya wala hatudanganyiki na machozi ya mamba ya wale waliojitolea ubaguzi rangi wa kinyama na kiudhalilishaji ambao ni kibali cha utawala wa mfumo wa kirasilimali. Aina zote za ugaidi zinaruhusiwa katika dola za Kisekula, ndio maana zake pekee na upigiaji upatu ambao hutofautisha ni nani ataitwa "mwanamgambo" au mpiganiaji uhuru. Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Muumba wa uhai na kifo lakini tunawajibika kwa ukiukaji wa maisha ya Waislamu na kutoa ruhusa kwa maadui wa Uislamu kutawala katika ardhi zetu. Wajibu wetu ni kufanya kazi bila kuchoka kuuokoa Ummah huu kutokana na utawala wa ukafiri na kukipa kizazi kijacho cha Umma huu haki zao kama zilivyofafanuliwa katika Qur'an na Sunnah.

(وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ)

“...Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini.” [Al-Qur’an 6:151]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah #TurudisheniKhilafah
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
أقيموا_الخلافة# كيف_تقام_الخلافة#
#YenidenHilafet #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu