Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vladimir Putin Amechukua Mahali pa Karimov

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 11 Agosti, shirika la habari la RIA Novosti liliripoti: "Muungano wa gesi tatu wa Urusi, Uzbekistan na Kazakhstan huenda ukapanuliwa ili kujumuisha nchi zengine, Dmitry Birichevsky, mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, aliiambia RIA Novosti.

Hatuondoi uwezekano wa kupanua ushirikiano wa pande tatu katika sekta ya gesi. Tunajua kuwa dola zengine pia zinavutiwa nao. Tuko wazi kwa ushirikiano kama huo kwa kuelewa kwamba unapaswa kuwa na manufaa na kujenga, kwa kuzingatia nafasi za washiriki wote,” alisema.

Maoni:

Kulingana na data ya OPEC ya 2021, Uzbekistan ilishika nafasi ya 17 kwenye orodha ya nchi kwa suala la uzalishaji wa gesi kwa mwaka, huku Urusi ikishika nafasi ya 2. Pamoja na hayo, Urusi, baada ya uvamizi wa kijeshi dhidi ya Ukraine, imekuwa chini ya vikwazo, ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa usambazaji wa gesi kwa Ulaya na nchi nyingine. Na nchi za Ulaya zenyewe, licha ya haja ya gesi, zinaanza kukataa kununua gesi ya Urusi.

Mamlaka ya Kremlin katika medani ya kimataifa imeshuka hadi kufikia kiwango cha madikteta wa Asia ya Kati. Ziara ya mwisho ya Putin barani Ulaya ilikuwa Uswizi mnamo 2021. Leo Putin anacheza kwenye mazingira yasiyo na tija pamoja na wasaidizi wake, marais madikteta wa Uzbekistan, Kazakhstan na Tajikistan. Katika kipindi cha mwaka mmoja hivi uliopita kumekuwa hakuna habari kuhusu ziara ya Putin barani Ulaya au ziara ya viongozi wa Ulaya nchini Urusi. Putin alifukuzwa kutoka G8 na hakubaliwi tena barani Ulaya.

Sasa Kremlin inapaswa kuuza gesi yake ili kukwepa vikwazo kupitia Uzbekistan au Kazakhstan. Dhalimu Karimov, rais wa kwanza wa Uzbekistan, alikuwa akiuza gesi kwa njia hii. Wakati huo, Uzbekistan ilikuwa chini ya vikwazo, na Karimov alikuwa na hasira na ugomvi kila wakati na Kremlin kwa sababu Putin alikuwa akinunua gesi kwa bei ya chini na kisha kuiuza tena kwa Ulaya kwa bei ya juu zaidi. Sasa, Putin yumo ndani ya viatu vya Karimov na hawezi kuuza gesi Ulaya au nchi nyingine kwa sababu ya vikwazo.

Uzbekistan nayo inajihalalisha kwa jumuiya ya kimataifa kufanya biashara na Urusi kwa ukosefu wa gesi nchini humo, ingawa iko katika viongozi 20 wa juu katika uzalishaji wa gesi duniani. Haishangazi kwamba uwongo mbaya kama huo unawafaa viongozi wa serikali kuu za ulimwengu. Kwa sababu leo sera nzima ya jumuiya ya ulimwengu imejengwa juu ya udanganyifu na unafiki.

Katika Uislamu, gesi kama maliasili ni mali ya umma. Serikali au mtu binafsi hawezi kutumia maliasili hii na kuitumia kwa khiyari yake pekee. Imepokewa na Abu Dawud kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلاَثٍ فِي الْمَاءِ وَالْكَلإِ وَالنَّارِ وَثَمَنُهُ حَرَامٌ» ‏

“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto”. Hadith hii hii imepokewa na Anas kwa ziada ya “...na mauzo yake ni haramu”. Imepokewa na Ibn Majah kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: »ثَلاَثٌ لاَ يُمْنَعْنَ  الْمَاءُ وَالْكَلأُ وَالنَّارُ «"Vitu vitatu havinyimwi watu: maji, malisho na moto." Hii yaashiria kwamba watu ni washirika katika maji, malisho na moto na ni haramu kwa mtu binafsi kuchukua umiliki wa vitu hivi.

Ni Dola ya Khilafah Rashida ya Pili pekee inayoongozwa na mtawala mwadilifu ndiyo inayoweza kusitisha uuzaji wa gesi na kukomesha jinai za watawala wetu madhalimu na mabwana zao wakoloni. Tuna imani kuwa ahadi hii itakuwa kweli hivi karibuni, kwani Mwenyezi Mungu hutumiza ahadi zake. Na sisi tunamtegemea Mwenyezi Mungu!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu