Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuporomoka kwa Jamii ni Mojawapo ya Matunda Machungu ya Mfumo wa Kibepari!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Matumizi ya dawa za mfadhaiko kwa kila mtu nchini Uturuki yaliongezeka kwa asilimia 76 katika kipindi cha miaka 12 iliyopita. Katika miaka 2 iliyopita, mauzo yaliongezeka kwa masanduku milioni 10. Uuzaji wa masanduku milioni 49 na elfu 857 ya dawa za mfadhaiko mnamo 2019 uliongezeka hadi masanduku milioni 54 na elfu 625 mnamo 2020 na masanduku milioni 59 na elfu  641mnamo 2021.

Maoni:

Kwa kweli, takwimu hizi ni taswira ndogo ya jinsi mporomoko wa kijamii ulivyo wa kina. Mgogoro wa kiuchumi, ambao umezidisha na kulaani mamia ya maelfu ya familia kwa umaskini, umegeuza mizani ya kisaikolojia ya nchi juu chini. Baadhi ya mambo hasi kama vile kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, umaskini na uchochole, kupungua kwa uwezo wa ununuzi, kushuka kwa thamani ya lira, kuongezeka kwa bei ya vyakula na mafuta kumezorotesha sana afya ya akili ya watu. Hakuna tena uaminifu na amani miongoni mwa watu. Ni nadra sana kuona watu wenye furaha katika jamii. Mwenendo huu mbaya umesababisha baadhi ya majeraha ya kisaikolojia kwa watu. Kwa kawaida, kutoaminiana huko kunasukuma watu kutumia dawa za kupunguza mfadhaiko. Wataalamu wanasema kuwa ongezeko la matumizi ya dawa za mfadhaiko limefikia viwango vya kutisha katika suala la afya ya umma. Watu wameanza kutafuta dawa na furaha katika vidonge hivyo. Kwa hakika, ni ubepari badala ya dawa hizi ndio unaowatia watu ganzi. Unaondoa uwezo wao wa akili na kufikiri.

Lakini, haikuwezekana kuona picha hii mbaya hapo awali. Jamii hii ilikuwa na furaha sana karne moja tu iliyopita. Ilikuwa ni jamii yenye hadhi na heshima. Afya ya akili ya jamii haikuvunjika. Mababu wa jamii hii walikuwa wakiteka nchi na mabara ili kumridhisha Muumba wao na kuufanya Uislamu ambao wanauamini, utawale duniani. Walikuwa wakiichukua bendera ya Uislamu wakiivukisha bahari. Hii ilikuwa ni kwa sababu hukmu za Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Ta’ala, Mmiliki wa mwanadamu, uhai na ulimwengu, zilikuwa zikitekelezwa kwenye jamii hiyo. Pindi utabikishaji wa hukmu za Sharia ulipositishwa, fungamano la mwanadamu na Muumba wake lilivunjwa, na kwa utabikishwaji wa ubepari na "maadili" ya kiliberali kwenye jamii, kuporomoka kwa kiroho, kifikra, kimaadili na kimada kulifuata. Hili limesababisha viwango vya juu vya machafuko na ukosefu wa furaha.

Kwa sababu ubepari umemtafuna mwanadamu mara kwa mara. Sio tu kwamba umemfukarisha mwanadamu kimada, pia imemfanya kuwa masikini na kumfukarisha kiutu na kiakhlaki. Umemuacha bila chochote kwa jina la kipimo na ubora. Mfumo wa kibepari hauchoki kuzalisha mengine mapya, unaendelea kufisidi jamii, kudhalilisha watu, kutofautisha watu, kwa ufupi, unaharibu kila kitu kuhusu binadamu na kumtafuna binadamu. Kwa sababu hivi ndivyo ubepari unavyofanya. Kwa sababu ubepari umewaathiri sio tu Waislamu bali wanadamu wote, umechukua kila kitu kutoka kwa katika maadili ya utu. Umemuua mwanadamu. Umeiiba shakhsiya yake, tabia yake, maadili yake, na kumgeuza kuwa kiumbe duni kabisa. Umemdhalilisha mwanadamu. Umemfanya mwanadamu asahau ubinadamu wake na Muumba wake. Kwa kweli, umemsaga mwanadamu kama kinu, na kutosaza chochote kwa mwanadamu kwa jina la utu.

Wakati huo huo, chini ya jina la uhuru wa kibinafsi, umempa mwanadamu uhuru wa kufanya chochote anachotaka. Umemfanya mwanadamu kuwa muasi dhidi ya Muumba wake. Umewavuta wanadamu kwenye upotevu. Umeharibu nafsi, utu, na shakhsiya. Umemfanya mwanadamu kuwa zimwi. Umechana kujitolea na ukarimu kutoka kwake. Umemfanya mwanadamu kuwa bakhili na mbinafsi. Umeuponda upande wa kumpendelea ndugu yake Muislamu kuliko nafsi yake. Umechafua sura ya mwanadamu kwa kutanguliza manufaa ya mali, cheo, umaarufu na mambo ambayo watu wanahadaiwa kwavyo zaidi na wanavitamani zaidi. Umeondoa amani na furaha kutoka kwa mwanadamu. Umeharibu afya ya akili ya watu. Umebadilisha maumbile asili ya wanadamu. Kwa hiyo, si ajabu kwamba watu wanaojiua, ukosefu wa maadili, kiwewe cha kisaikolojia na viwango vya uhalifu viko juu sana kote ulimwenguni.

Kwa hiyo, ubepari, ulio na umbo bovu, umewaacha wanadamu na ulimwengu wakijaa maangamivu wa kiuchumi, migogoro na vita. Ubepari hauna thamani chanya iliyobaki kutoa kwa wanadamu. Ubepari umefilisika na kifo chake cha ubongo kimetokea. Kama vile zamani, wanadamu walipata njia ya kuuangamiza mifumo inayoondoa ubinadamu kwa watu, kusimamisha mfumo wa ulimwengu, na kutoka ndani ya nyakati za giza totoro, bila shaka leo watapata njia ya kutoka katika hali hii na kupata njia ya kumfanya mwanadamu kuwa na heshima na utukufu, kuwainua kutoka daraja ya wanyama hadi daraja ya wanadamu, kuwakumbusha ubinadamu wao, kuwarudisha kwenye maumbile yao asili na kuanzisha mfumo mpya wa dunia. Hakika njia hii ni Uislamu. Mfumo kamili wa maisha wa Uislamu. Kama vile ilivyowatoa wanadamu katika giza na kuwaingiza kwenye nuru hapo awali, bila shaka unaweza kufanya hivyo tena leo. Umekusudiwa kufanya hivyo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz Çelik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu