Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uoga ni Fedheha, Ilhali katika Kumkabili Adui Kuna Heshima

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la ‘Express Tribune’ la Pakistan liliripoti mnamo tarehe 1 Mei 2024 kwamba, "Pakistan, China na Iran hivi karibuni zitafanya mkutano wa pande tatu juu ya kukabiliana na ugaidi na usalama katika ishara nyingine ya kukua kwa dori ya Beijing, kuwaleta pamoja majirani katika masuala muhimu. Mkutano wa kwanza wa Mashauriano ya pande tatu za Pakistan-China-Iran kuhusu kukabiliana na ugaidi na usalama ulifanyika jijini Beijing mwezi Juni mwaka jana." [Tribune]

Maoni:

Iran na Pakistan zilikutana pamoja na China kwa ajili ya nini mnamo Juni 2023? Je, wanakusudia kukutana tena na China kwa ajili ya nini? Kushirikiana katika kukabiliana na ugaidi! Kushirikiana na gaidi China, ambayo inawapiga vita Waislamu huko Xinjiang na Dini yao! Kushirikiana na dola adui, huku ikiipa Dola ya Kibaniani uhuru juu ya Kashmir Inayokaliwa kimabavu, na umbile la Kiyahudi uhuru juu ya Palestina! Mkutano huu haungeweza kuwa mbaya na wa kuchukiza zaidi hivi, kwani unajiri katika wakati ambapo kina dada na watoto wetu wanauawa na magaidi halisi wa zama zetu.

Ilhali, serikali za nchi mbili kubwa za Waislamu zitakutana tena kuhusiana na ugaidi, wakati ambapo umbile la Kiyahudi limeendesha zaidi ya siku mia mbili za ugaidi kwenye Ardhi Iliyobarikiwa ya Masjid Al-Aqsa. Zaidi ya watu 34,000 wameuawa shahidi na uvamizi wa Kiyahudi, kwa kutumia silaha na mifumo ya silaha kutoka nchi za Magharibi. Kupoteza maisha ni kando na uharibifu wa karibu miundombinu na makaazi yote. Tangazo la serikali zenye majeshi mawili yenye nguvu zaidi ya Kiislamu, katika wakati kama huo wa kuhuzunisha moyo kwa Umma, ambalo sio la kutangaza uhamasishaji wa majeshi kukomesha ugaidi wa Kizayuni, ni usaliti kwa matukufu ya Uislamu.

Amri kwa askari mashujaa wa Uislamu, na mifumo ya silaha katika matumizi yao si chochote ila ni neema ya Mwenyezi Mungu, Al-Aziz Al-Mutakabbir. Kabla ya vita vya Mu’tah, habari ziliwafikia askari 3000 wa Kiislamu kwamba Hiraqla alikuwa amekusanya askari laki moja kwa pamoja, pamoja na askari wengine laki moja wa Lakham, Judham na Balqain, makabila ya Waarabu  yanayoungana na Wabizantini. 'Abdullah bin Rawaha aliwahutubia Waislamu kwa  kusema, وما نقاتل الناس بعدد ولا قوة ولا كثرة، ما نقاتلهم إلا بهذا الدين الذي أكرمنا الله به، فانطلقوا، فإنما هي إحدي الحسنيين، إما ظهور وإما شهادة “Katika pambano letu hatutegemei idadi ya askari au zana bali juu ya Dini ambayo Mwenyezi Mungu ametukirimu kwayo. Jitahidini kushinda mojawapo ya hayo mawili, ushindi au shahada.” Imepokewa na Al-Bukhari kwamba Khalid bin Waleed, Upanga wa Mwenyezi Mungu, alitumia panga tisa ambazo zilivunjika wakati alipokuwa akipambana na maadui wa Uislamu bila kuchoka na kwa ujasiri. Hakika amri ya askari wa Kiislamu inafananishwa na upanga wa Mwenyezi Mungu. Inawajibisha kwamba silaha zitumike kwa utukufu wa Neno la Mwenyezi Mungu (swt). Inawajibisha kwamba silaha hizo zitumike na watu ambao wana imani kamili katika ushindi (Nasr) ya Mwenyezi Mungu (swt).

Kuhusu silaha za Waislamu, kumbukeni tukio la kabla ya Vita vya Uhud pale Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipochukua upanga mkali, akaushika mkononi mwake na akawaita Maswahaba zake na kusema, «من يأخذ هذا السيف بحقه‏؟» “Ni nani aliye tayari kuchukua upanga huu na kuupa haki yake inayostahili?” Wanaume wengi walikuwa tayari kuuchukua. Baadhi yao walikuwa ni ‘Ali bin Abi Talib, Az-Zubair bin Al-‘Awwam na ‘Umar bin Al-Khattab. Lakini haikupewa yeyote. Abu Dujana Sammak bin Kharsha akauliza, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni ipi thamani yake?” Mtume (saw) akasema: «أن تضرب به وجوه العدو حتى ينحني» “Ni kukata kwa kwao nyuso za adui mpaka upinde.” Basi Abu Dujana akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nitauchukua kwa thamani hiyo. Kwa hiyo, akapewa upanga huo.

Je, majeshi ya Pakistan na Iran yamewapa askari wao na silaha zao haki yake kamili? Majeshi yao ni miongoni mwa majeshi yenye nguvu zaidi duniani, achilia mbali Ulimwengu wa Kiislamu. Ilhali, viongozi wasaliti wametumia mifumo ya zana na silaha za Ummah kinyume na alivyoamrisha Mtume (saw). Kwa hakika, tunawaona wakizionyeshwa ima kwa ajili ya fahari ya kitaifa, au kutumika kuwaunga mkono maadui wa Waislamu, chini ya bendera ya kupambana na ugaidi. Msimamo kama huo uko chini ya hadhi ya dola hizo zenye nguvu za Waislamu. Historia tukufu ya Kiislamu ni ushahidi wa ukweli kwamba dola ya Kiislamu siku zote imekuwa ikibadilisha mfumo wa dunia. Hata hivyo, viongozi hawa wawili duni wa dola hizi mbili kubwa za Kiislamu wanaunga mkono mfumo mbovu wa kimataifa, na dola kuu za kikoloni zinazonufaika nao.

Umefika wakati sasa kwa wenye uwezo na ujasiri kuwaondoa viongozi wa aina hii ambao hawastahili kuwa katika nafasi ya kuongoza majeshi haya yenye nguvu. Ni wakati sasa wa kuondoa nembo na miundo ya dola za kitaifa, na wote wanaozitetea, kwani ndizo zinazoimarisha mfumo wa kimataifa na udhibiti wake. Wakati uwewadia sasa wa mashujaa na wajasiri kujitokeza kuunga mkono kusimamishwa kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Dola ambayo Mtume Muhammad (saw) alitabiri kurudi kwake. Ni dola itakayorudisha heshima na hadhi inayostahiki Uislamu na Waislamu.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ ٱلْأَمْرِ مِن شَىْءٍۢ قُلْ إِنَّ ٱلْأَمْرَ كُلَّهُۥ لِلَّهِ يُخْفُونَ فِىٓ أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ ٱلْأَمْرِ شَىْءٌۭ مَّا قُتِلْنَا هَـٰهُنَا قُل لَّوْ كُنتُمْ فِى بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ ٱلَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ ٱلْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ وَلِيَبْتَلِىَ ٱللَّهُ مَا فِى صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِى قُلُوبِكُمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ]

“Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo hili? Sema: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.” [Aali-Imran:154].

#ArmiesToAqsa

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhannad Mujtaba – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu