Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

China Inapita Mle Mle Kwenye Uchumi wa Kimagharibi wa Kikoloni na Kinyonyaji

(Imetafsiriwa)

Habari:

Siku ya Alhamisi tarehe 09/05/2024, kampuni ya Kichina, Saturn Corporation Limited ilizindua kiwanda cha kuunganisha malori katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni hiyo ina uwezo wa kuunganisha hadi matrekta 30 na malori 9 kwa siku.

Maoni:

Kampuni ya Saturn Corporation Limited ni miongoni mwa makampuni mengi ya kimataifa yanayofanya shughuli zake nchini Tanzania. Kampuni hiyo huunganisha matrekta na malori ya Howo kutoka China ikilenga zaidi soko la Tanzania.

Chini ya kisingizio cha sera ya ‘soko huria’ ya kibepari, makampuni mengi ya kikoloni ya Kimagharibi yanayonya masoko na rasilimali nyingi za Afrika, na sasa China inafuata mwelekeo huo huo wa Wamagharibi katika uporaji wa rasilimali za Afrika na kwa mikataba ya kibiashara isiyo ya haki.

Inaripotiwa kuwa mwaka 2022, thamani ya bidhaa kutoka nje ya Afrika na China ilifikia dolari bilioni 257.67, huku China ikiwekeza dolari bilioni 1.8 pekee katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022.

Afrika inauza nje rasilimali za thamani kwenda China kama vile mafuta ghafi, madini, chuma na bidhaa za kilimo ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya maisha ya watu wa China, wakati huo huo ikiwa ni chanzo cha soko la bidhaa za China. Uhusiano huu usio wa haki, usawa, na wa kinyonyaji kati ya China na Afrika chini ya jina la soko huria umesababisha madeni yasiyoelezeka kwa nchi za Afrika.

China imekuwa mkopeshaji katili barani Afrika, na mikopo yake ni kati ya dolari bilioni 170 hadi 170.8 kwa takriban nchi 39 hadi 49 za Kiafrika mnamo mwaka 2023.

Uchumi huu wa Kibepari wa China unaonesha wazi wazi ukweli kwamba tangu miaka ya tisiini China imeacha kimya kimya mfumo wake wa Ujamaa ulioasisiwa tangu miaka ya 1890 kwa kushikilia na kuukumbatia ubepari hususan katika nyanja ya kiuchumi. Kwa kuliangalia hilo, inathibitika ukweli kwamba upinzani wa Ujamaa dhidi ya Ubepari ulishindwa, na pia ni dhihirisho kuwa ujamaa ni mfumo ulioshindwa kuwahudumia wanadamu.

Katika namna hiyo hiyo (ya kushindwa) Ujamaa, pia na ubepari nao ni mfumo unaoangamia na kushindwa umekwisha igeuza dunia kuwa mahala pa maafa na mabalaa badala ya utulivu.

Kwa hivyo, mifumo yote miwili (ujamaa na ubepari) imeshindwa kuwatumikia wanadamu (ipasavyo), hivyo, ulimwengu unahitaji mfumo mbadala ambao ni Uislamu.

Sera ya Kiislamu ya kiviwanda itakapotekelezwa chini ya serikali yake ya Kiislamu ya kiulimwengu (Khilafah) itajenga viwanda vyenye nguvu na vya aina mbalimbali, itahakikisha umiliki wa Umma wa viwanda vinavyohusiana na rasilimali za Umma, umiliki wa serikali na wa kibinafsi wa viwanda muhimu, na kuondoa mzunguko wa kinyonyaji wa mali katika jamii.

Pia (Khilafah) itaanzisha utafiti thabiti wa viwanda na maendeleo, na kukomesha mara moja mikopo ya wakoloni yenye masharti ya kinyonyaji kwa mbadala wa vyanzo halali vya mapato ya Kiislamu, ikiwemo mapato ya milki za Umma kutokana na utajiri mwingi wa Afrika kama vile mafuta, gesi asili nk.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu