Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gaza Inahitaji Kukusanywa kwa Majeshi ya Khilafah katika Mwezi wa Ushindi na Ufunguzi, Ramadhan, Bila kuchelewa!

(Imetafsiriwa)

Habari:

BBC iliripoti tarehe 28 Februari kwamba, "Rais wa Marekani Joe Biden anasema anatarajia kuwa na usitishaji vita katika vita kati ya 'Israel' na Hamas huko Gaza kufikia Jumatatu... "Tuko karibu," Rais Biden aliwaambia waandishi wa habari jijini New York Jumatatu. “Bado hatujamaliza. Matumaini yangu ni kufikia Jumatatu ijayo tutakuwa na usitishaji mapigano.” [BBC]

Maoni:

Hebu tuelewe ukweli uliopo nyuma ya Marekani kushinikiza kusitishwa kwa mapigano kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Haipaswi kuwa na makosa katika kuona hii kwa jinsi ilivyo. Biden asiye na roho hana huruma na Ummah wetu wa Kiislamu. Haifanywi kwa ‘kuheshimu’ dini yetu. Je, mtu yeyote anawezaje hata kuanza kutoa madai hayo, wakati Biden hajali maisha ya mama, baba, na watoto, kama inavyoonekana wazi kutokana na kumuunga mkono Netanyahu tangu tarehe 7 Oktoba 2023?

Motisha yoyote ya kusitisha mapigano lazima ionekane jinsi ilivyo, hofu. Makafiri daima wamekuwa wakiogopa umoja wa Umma wa Kiislamu, adabu zetu za kimsingi, nguvu, na kupendana sisi kwa sisi na Mola wetu (swt). Wanaiona Ramadhan kuwa wakati ambapo Waislamu watakusanyika pamoja kusherehekea na kuimarisha imani yao. Umekuwa mwezi wa ushindi kwenye medani za vita. Itakuwa vigumu kiasi gani kutunyamazisha na kutudhibiti, wakati huo?!

Wakati viongozi wa nchi za Magharibi wakishikilia hofu hii, majeshi ya Waislamu yanajiandaa kuingia katika Mwezi huu Mtukufu, bila hata ya kufanya jaribio la kutimiza wajibu wao na kuokoa maisha ya Waislamu, ambao inawajibu wa kuwalinda. Wanatayarisha nyumba zao kufanya Suhuur na Iftaar, wakati ndugu na dada zetu Waislamu wana njaa. Wanajiandaa kujisikia furaha tele katika ujio wa Idd, huku watu wa Palestina wakikosa hata mahitaji ya kimsingi.

Kuhusu suala la kutuma majeshi yetu, kwa wakati huu, hakuna hoja inayoweza kutolewa dhidi ya hili kuwa suluhu pekee. Tayari tulikuwa na usitishwaji wa mapigano mnamo Novemba 24 hadi 30. Mara tu ilipomalizika, baada ya viongozi kuzunguka kwa duru, kusukuma tarehe na kurudi na kucheza na maisha ya watu, Mayahudi wa Kizayuni walirudi kwetu, kwa nguvu zaidi.

Ama kuhusu dhana ya kususia, ni hisia ya ajabu. Ni jambo la kupongezwa sana jinsi kila mtu amesimama kidete katika kufanya kadiri awezavyo, kwa njia yoyote anayojua. Mwenyezi Mungu (swt) azikubali juhudi zetu za kupunguza mtiririko wa fedha kwa adui. Hata hivyo, ni dhahiri katika hatua hii, kwamba Marekani itatumia fedha zake zozote, na zote, kusaidia kituo chake cha kijeshi katika moyo wa Ummah, "Israel."

Kuhusu msaada, tuliona misaada ikitumwa Gaza na vikosi vya jeshi vya Jordan. Mnamo tarehe 28 Februari 2024, Al-Jazeera iliripoti tukio la kusikitisha, "Maelfu ya Wapalestina kutoka Ukanda wa kusini wa Gaza walikusanyika ufukweni baada ya ndege kuangusha msaada wa chakula." [Aljazeera.com] Misaada mingi iliishia baharini, ambapo Wapalestina waliokuwa na njaa walipanda juu ya boti ndogo ili kujaribu kuzichukua. Viongozi wa Waarabu na Ajm wanarusha maneno kama "msaada wa kibinadamu." Wanataka tuwapongeze kwa jitihada zao. Hata hivyo, majeshi hayakuundwa kwa ajili ya misaada au kusitisha mapigano. Waliumbwa kwa ajili ya hatua, nusra, ulinzi, kumrudisha nyuma adui na ushindi. Kwa hakika imekuwa hali chungu, tangu tulipopoteza ngao yetu ya Khilafah, miaka mia moja iliyopita, tarehe 3 Machi 1924. Enyi Waislamu, simamisheni Khilafah, ili hatimaye tukusanye majeshi kwa ajili ya kuinusuru Gaza. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Sura Muhammad 47:7].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Nur Musab

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu