Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanajificha Chini ya Jiwe Gani na Katika Sayari Gani Wanajeshi na Majenerali wa Majeshi ya Waislamu Wakati Hata Askari wa Jeshi la Adui Yetu Hawawezi Kukaa Kimya?!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika kupinga mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa juu ya watu wa Gaza, mwanajeshi wa Marekani anayeitwa Aaron Bushnell alijitolea maisha yake mbele ya ubalozi wa ‘Israel’ kwa kujichoma moto. Alisema alipokuwa akielekea kifo chake kwamba hawezi kushiriki tena katika mauaji ya watu wasio na hatia huko Gaza, na maneno yake ya mwisho yalikuwa ‘Iacheni Huru Palestina’.

Maoni:

Mwaka wa 2010, Mohamed Bouazizi alijichoma moto akipinga ukandamizaji nchini Tunisia, ambao ulizusha maasi ya ‘Mapinduzi ya Kiarabu’. Hawa walishindwa kwani walikosa kuungwa mkono na majeshi. Mapinduzi mapya yanahitajika. Ni wakati muafaka kwa majeshi ya Waislamu kutoka nje ya kambi zao; kwa ajili ya wokovu wa yale yaliyosalia ya Gaza, kwa kila Muislamu aliyekandamizwa na kwa dunia nzima inayougulia chini ya unafiki wa ubepari. Makumi ya maelfu ya wanawake na watoto wamechomwa moto, kupigwa risasi na kupigwa mabomu na jeshi la watu wanaojipenda na waoga zaidi duniani, na mwanajeshi pekee aliyesema hapana ni Mmarekani! Ziko wapi hisia za aibu kwa askari na majenerali wa Misri na Jordan, na nchi nyingine za Kiislamu, ambao majeshi yao makubwa na maghala ya silaha yamekaa bure!? Mmarekani, Aaron Bushnell, hakuweza kuishi na yeye mwenyewe akijua kwamba serikali yake inaunga mkono umbile la Kizayuni na inashiriki katika mauaji yake ya kila siku huko Gaza.

Enyi askari na majenerali wa Kiislamu, hamuoni kwamba serikali zenu pia zinashiriki katika kumwaga damu ya ndugu zenu na dada zenu huko Gaza, na kwamba watawala hawa daima wamekuwa, kwa msaada wenu, wakinyonya damu ya familia zenu? Je, haya yote si mengi sana kwenu, kwa vile sasa mmekoma kuwa watoto na kuwa na macho ya kuona na masikio ya kusikia, na bado hamna akili kama majumba ya makumbusho ambayo roho zao ziliiacha miili yao zamani? Je, munaamini kweli kauli mbiu za matusi za watawala wenu na vipaza sauti vyao vya vyombo vya habari vinavyokuambia kwamba ushujaa na heshima ni katika kujenga, na kisha kujificha nyuma, kuta mpya zinazowatenganisha na ndugu zenu wa Gaza?

Inukenu na muwe watu ambao mamia ya mamilioni ya Waislamu wanataka kutoka kwenu. Khilafah ndio njia, na kuvunja mipaka kati ya ndugu ambayo ilijengwa na makubaliano ya kikoloni ya Sykes-Picot ni kujikomboa nyinyi na ulimwengu. Je, mutaitikia wito wa Biden, Sunak na Schultz, ambao watakufedhehesheni katika dunia hii na kukutelekeza katika haja, au mutaitikia wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake:

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ  *وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ[

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 47:7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu