Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Matukio mjini Gaza Yanaonyesha Kwa Uwazi Jinsi Uislamu Ulivyo Bora Kiakhlaki na Kifikra kuliko Thaqafa Danganyifu ya Kimagharibi ambayo Kirongo Inaitwa ni Mwangaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirika karagosi la vyombo vya habari liitwalo CNN lilichapisha makala ya propaganda ya Wazayuni mnamo Juni 12, 2024 yenye kichwa: “Mateka wa Israel” walikabiliwa na “adhabu” wakati wa miezi minane katika uzuizi wa Hamas, familia moja yasema.” Makala hiyo iliundwa na watu watano na inazungumza juu ya kile familia ya mmoja wa mateka, Andrey Kozlov -27, ilisema baada ya IDF kuua watu 274 ili kumwachilia yeye na mateka wengine watatu mnamo Juni 9.

Maoni:

Kabla ya kujadili simulizi ya pili na ya tatu ya aliyoyapitia Andrey akiwa kizuizini huko Gaza, zingatia jinsi walivyofanyiwa mateka wa Palestina. Wapalestina wasiopungua 40 wameuawa wakiwa chini ya ulinzi wa ‘Israel’ tangu Oktoba 7 kwa mujibu wa ripoti za Israel, ambazo pia zilieleza kwa kina matumizi makubwa ya mateso kwa wafungwa. Wale ambao wamerudi wanaonyesha dalili zinazoonekana za unyanyasaji, njaa na mateso. Miili iliyodhoofika baada ya majuma marefu ya mgao mdogo wa chakula, kukatwa mikono na miguu kutokana na kuzuiwa kwa muda mrefu kwa kufungwa kamba za plastiki, magonjwa ya ngozi na kuvunjika mifupa ni sifa za kawaida za Wapalestina wanaoregea kutoka kwa kile wanasiasa waongo wa Magharibi wamekiita 'demokrasia pekee katika Mashariki ya Kati.'

Kwa kuongezea, siku nyingi za kufungwa macho na kutoweza kupata choo na kuvuliwa nguo na chini ya hali hizi kushambuliwa na mbwa na kupigiwa kelele na teke kila mara na walinzi. Kwa kulinganisha, madai kwamba mateka waliochukuliwa kutoka Gaza walikuwa na hofu au walikuwa na hali mbaya yanaonekana kuwa duni; hasa kwa kuzingatia kwamba kila mtu katika Gaza ana hofu, wasiwasi na kuteseka kwa ukosefu wa maji safi au vifaa vya matibabu, wakati upatikanaji wa chakula ni wa kushtukizia kutokana na uharibifu wa makusudi wa viwanda na kilimo mjini Gaza na ugaidi wa Kizayuni pamoja na uzuizi mkali wa utoaji wa misaada ya kibinadamu.

Kwa Wapalestina walioshikiliwa katika umbile la kidemokrasia la Kizayuni ukosefu wowote wa chakula au dawa haungeweza kulaumiwa juu ya mazingira ya kutisha ambayo mateka pamoja na watekaji wanayopitia. Badala yake, unyanyasaji wa umbile la Kizayuni unapigiwa hesabu kwa uangalifu. Wakati hospitali za Palestina zilizosalia ambapo wagonjwa wanatibiwa sakafuni katika hali mbaya na dawa chache kutokana na kulengwa huduma za afya na wavamizi ndio sehemu ya matumaini kwa wanawake na watoto wanaotafuta msaada wa majeraha ya kuungua na makombora, hospitali za Kizayuni ambapo mateka wa Kipalestina walipelekwa zilikuwa kuzimu mbaya zaidi. “Waliwanyima chochote kinachofanana na ubinadamu,” alisema daktari mmoja anayefanya kazi katika hospitali ya uwanjani. Mfanyikazi mwengine alikiri kwamba “aliombwa kujifunza jinsi ya kufanya mambo kwa wagonjwa, kufanya operesheni ndogo za matibabu ambazo ziko nje ya taaluma yangu,” aghlabu bila ganzi na “ikiwa watalalamika kuhusu maumivu, wangepewa paracetamol. Kuwepo pale tu nilihisi kama kushiriki katika unyanyasaji.”

Makala ya CNN ilishindwa hata kutaja mateso ya kikatili ya wafungwa wa Kipalestina ambapo kuna ushahidi mwingi wa kimwili na mashahidi walioona kwa macho kutoka kwa wahasiriwa na watoa taarifa ambao walifanya kazi katika vituo vya uzuizini. Badala yake, CNN ilichagua tu kukuuza simulizi za uzushi za kusikia kwa wengine za wale walioregeshwa huku wakitabasamu na walionekana dhahiri kuwa sawa na wenye afya nzuri kutoka Gaza katika operesheni ya kijeshi iliyoacha nyuma mamia ya raia waliokufa na kuyajaza mahospitali kwa majeruhi.

Ni muhimu kutaja kwamba kuna shinikizo kubwa kwa mateka wa zamani kusimulia hadithi kuhusu dhuluma kwani wale waliosema chochote chanya kuhusu hali ya kuzuiliwa kwao wamechukuliwa kama wasaliti na vyombo vya habari vya Kizayuni na jumuiya za kiraia. Mtangazaji wa chaneli ya 12, alifutwa kazi baada ya kuzungumzia afya njema na mwonekano wa Noa Argamani, mmoja wa mateka walioachiliwa kutoka Gaza: “Hivi ndivyo msichana aliyekaa kifungoni kwa miezi tisa anavyoonekana? Tazama nyusi zake, zinaonekana kuwa nzuri kuliko zangu! Ngozi yake! Kucha zake! Hiki ni nini? Haya ndiyo yanayopelekea wanawake na watoto wasio na hatia kuuawa huko Gaza?”

Ndio kwa hakika, wanawake na watoto wanauawa mjini Gaza na wengine wanatekwa nyara kutoka Gaza ili kuteswa na kuuawa kizuizini na yote haya kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, Uingereza na Ujerumani na uungaji mkono wa kiasi fulani wa nchi nyingine nyingi za Magharibi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu