Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vita vya Kisasa ni Aina ya Uwindaji wa Kibeberu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Maafisa wanne wa Iran walisema katika mahojiano ya simu wiki hii kwamba kiongozi mkuu, Ayatollah Ali Khamenei, ameamuru jeshi kuandaa mipango mingi ya kijeshi kwa ajili ya kujibu mashambulizi ya ‘Israel’. (NY times)

Maoni:

Hali na mwitikio wa hali katika ulimwengu wa Kiislamu ni hatari na mbaya sana. Vifo na uharibifu katika kiwango hiki na kwa ufahamu huu mwingi wa kijamii si rahisi kuficha na athari haziepukiki kwa wale wanaodai kuwa na imani moja (Uislamu) na hivyo, kauli humiminika.

Uchambuzi unafanywa juu ya kauli hizo, maonyesho ya mazungumzo na mahojiano hufanywa, na hivyo jaribio linafanywa ili kuanzisha maoni. Tangu Oktoba 2023, watu wamepoteza kabisa imani yao katika suluhisho la Magharibi, na “Ndoto ya Marekani” ilibadilika na kuwa jinamizi, hakuna mtu anayeonekana kulitoroka.

Watu wameshuhudia toleo lililobadilika la vita na mapigano. Vita vilivyobadilishwa katika historia, kabla ya kuvunjwa Khilafah, Waislamu walipigana kwa ajili ya kusimamisha na kutangaza Ubwana wa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt), huku wengine wakipigania upanuzi na udhibiti wa kieneo. Ubeberu ulianzisha manufaa ya kilafi na kwa mara ya kwanza ramani ya dunia ikageuzwa kuwa ramani ya kisiasa, yenye migawanyiko ya kisiasa na mipaka ya kitaifa, na mgawanyiko huu ukazaa diplomasia ya kisasa, ambayo kwa maana nyengine ni sanaa ya udanganyifu.

Licha ya kauli mbiu zinazosisitizwa na Wairani wenye misimamo mikali, uhalisia wa fikra za kimkakati za Iran ni wa kutilia maanani zaidi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kanani hivi karibuni ametoa wazo hilo rasmi huku akisema kuwa, “hakuna haja ya kutuma vikosi vya ziada au vya kujitolea vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” na kuongeza kuwa Lebanon na wapiganaji katika maeneo ya Palestina “wana uwezo na nguvu ya kujilinda wenyewe dhidi ya uvamizi.”

Huku tukisoma na kusikia taarifa zinazokinzana zinazoendelea kutoka kwa Iran na viongozi wengine wa Waislamu, hatuwaoni kamwe wakiichukulia kama faradhi ya kidini. Si jambo la khiari na wala halimo ndani ya himaya yao kupima uwezo wa watu ambao vita vinafanywa dhidi yao. Je, ulimwengu wote wa Kiislamu haupaswi kuunganishwa dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu ambao wameungana katika kuwaua watu wasio na hatia wa Gaza kwa mashambulizi ya mabomu, njaa na maradhi? Hivi sio vita, hiki ni kitendo cha uwindaji wa kibeberu, wakati uwindaji unakusanywa katika eneo lililofungwa na kulindwa, na wawindaji wanawinda walionaswa na wasio na msaada. Kujiepusha kwa Iran na hatua halisi huenda kukachelewesha jambo lisiloepukika lakini hakutaiokoa kutokana na kuwindwa. Mwitikio wa sasa wa viongozi wa Waislamu hautokani na Ahkaam (hukmu) za Mwenyezi Mungu, wala hauegemei kwenye silika ya makafiri ya wawindaji. Jibu ni la mnyama aliyenaswa mtegoni ambaye anamtazama ndugu yake akiliwa na adui, bila kujua, ijayo itakuwa zamu yake.

Waislamu wameamrishwa kuwa imara na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, ndipo watakapoweza kuiona njia ya ushindi. Wakati Mughira ibn Zara alipowasilisha machaguo matatu kwa mfalme wa Uajemi na mfalme akakataa kusilimu au kutoa Jizya, Mughira alirudi kwa Saad ibn Waqas na kusema, “Jipe moyo, kwani Wallahi Mwenyezi Mungu ametupa funguo za ufalme wao”. Ndugu zetu hawauawi kwenye uwanja wa vita, kama Iran ingepeleka majeshi yake mara moja na wana askari waliopewa mafunzo wa Ummah huu wakapigana na kukumbatia kifo cha kishahidi basi tungeviita vita. Hivi sasa ni mauaji na hakuna mwenye haki ya kudai kuwa wanaouawa wana uwezo wa kutosha wa kupigana na hawahitaji msaada.

Kiongozi mkuu wa Iran Khamenei anajua ana mkono mbaya, na kwamba ameukunja mara kwa mara mbele ya shinikizo la ‘Israel’. Akumbuke kuwa Waislamu wamekatazwa kucheza kamari. Sisi Umma wa Muhammad (saw) tunajua kwamba umewasaliti Waislamu wa Gaza na Waislamu unaowatawala moja kwa moja. Watu wote wenye nguvu na mali, wanaodai kuwa Waislamu na hawatambui kuupa kipaumbele mgogoro wa Gaza lazima wakumbuke kwamba Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu:

[وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَى فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ]

Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu. [Al-Anfal:16].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu