Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Maldives Yatumbukia Zaidi ndani ya Mgogoro wa Kifedha, huku Ikiyumba Kati ya China na India

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 26 Oktoba 2024, gazeti la Deccan Herald liliripoti, “Maldives inajadili matarajio ya sekta ya utalii na India. Maendeleo hayo yanakuja siku chache baada ya Rais wa Maldives, Mohamed Muizzu, wakati wa ziara yake ya kwanza ya nchi mbili jijini New Delhi, aliita India kama “moja ya masoko makubwa ya chanzo cha utalii” kwa nchi yake na alitumai kuwa watalii zaidi wa India wangetembelea taifa hilo la visiwa.” [Deccan Herald]

Maoni:

Chama cha Muizzu cha ‘Peoples National Congress’ (PNC) na muungano wake walipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa bunge kutokana na kampeni ya ‘India Nje’. Muizzu alimshambulia mgombea wake mpinzani Solih kwa makubaliano na India ambayo yaliruhusu uwepo wa wanajeshi wenye silaha wa India kwa jina la mradi wa bandari ya kisiwa cha Uthuru Thila Falhu (UTF). Makubaliano hayo yaliongezwa muda hadi miaka sitini.

Serikali mtawalia nchini Maldives zimeyumba kati ya ‘India Kwanza’ na ‘India Nje.’ Serikali za 2009 na 2018 zilifuata ‘India Kwanza’ kama sera yao ya kigeni. Watawala waliruhusu uwepo wa jeshi la India na walikubali mikopo kwa riba kutoka India. Kinyume chake, serikali ya 2012 iliyumba kuelekea China na kupokea mikopo ya riba kutoka China. Tofauti na watangulizi wake, ziara ya kwanza ya nje ya Muizzu kama rais haikuwa India. Alitembelea China na serikali yake iliingia makubaliano kadhaa na China.

Muda mfupi kabla ya ziara ya Muizzu nchini China, Modi alipiga picha kwenye tovuti ya utalii ya India, Visiwa vya Lakshadweep, ambavyo vinashindana na Visiwa vya Maldives kwa utalii. Maldives inahitaji watalii wa India kwa uchumi wake unaotatizika. Uchumi wa Maldives una tasnia ndogo. Utalii na uvuvi ndio vyanzo viwili vikubwa vya mapato. Baadhi ya 90% ya mapato ya serikali yanazalishwa kupitia kodi kutoka kwa utalii.

Huku ikiyumba kati ya India na China, Maldives inazidi kutumbukia kwenye deni lenye riba. Deni la nje la Maldives lilizidi dolari bilioni 4 mwaka wa 2023, data rasmi inaonyesha, ikiwakilisha takriban 118% ya pato la taifa na hadi karibu dolari milioni 250 kutoka 2022. Kufikia Juni 2023, Benki ya Export-Import ya China ilimiliki 25.2% ya Deni la nje la Maldives na ndiyo mkopeshaji mkuu zaidi wa nchi hiyo, kulingana na Wizara ya Fedha ya Maldives.

Suluhisho la migogoro ya kiuchumi ya Maldives haliko katika kuyumba kati ya dola mbili zinazopiga vita Waislamu na Uislamu. Mfumo wa sasa wa ulimwengu unaleta madhara kwa Waislamu, kiuchumi na kijeshi. Unafanya dola za Waislamu kuwa uwanja wa kunyonywa na wakoloni, na washirika wao, India na umbile ya Kiyahudi. Suluhisho kwa Maldives ni kuwa sehemu ya Khilafah tukufu, kama ilivyokuwa huko nyuma. Maldives ni nchi ya Waislamu na 99% ya wakaazi wake ni Waislamu. Uislamu ulikuja kwenye mamlaka na utawala nchini Maldives mwaka 1153 (548 H). Baada ya mawasiliano imara na Khilafah ya Khalifa Al-Muqtafi (المقتفي لأمر الله), mtawala Dhovemi alisilimu na kuwa Sultan Muhammad al-Adil, huku watu wa Maldives wakisilimu kwa makundi. Kama sehemu ya Khilafah tukufu, Maldives walistawi hadi kuwasili kwa wakoloni wa Magharibi, na kuanzishwa kwa mfumo wa kikanda wa kikafiri.

Enyi Waislamu wa Asia ya Kusini! Hairuhusiwi kufanya miungano na dola zinazopigana nasi kwa sababu ya Dini yetu na kusaidia wengine katika kupigana nasi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah al-Mumtahina 60:9]. Khilafah Rashida itakata mafungamano yote na dola zinazopiga vita Uislamu na Waislamu. Itawaunganisha Waislamu wote kama dola yenye nguvu na tajiri zaidi duniani. Khilafah itaweza kufikia njia zote kuu za bahari duniani, na kuiruhusu kutawala biashara ya kimataifa, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi zilizopita. Khilafah itakuwa dola yenye nguvu zaidi baharini tena duniani, na kuruhusu jeshi lake la wanamaji kutekeleza dori yake katika kufungua ardhi mpya kwa Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Malik – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu