Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuchaguliwa tena kwa Trump: Mporomoko wa Demokrasia uso Kifani

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Novemba 6, 2024, ilithibitishwa kuwa Donald Trump, mhalifu aliyepatikana na hatia, alishinda tena uchaguzi wa rais nchini Marekani. Tukio hili sio tu suala la mtu wa kuchukiza, bali ni dalili ya uozo wa kina katika mfumo wa kidemokrasia wa Magharibi. Huku ulimwengu ukitazama, kuchaguliwa tena kwa Trump kunafichua udanganyifu mwingi ambao demokrasia ya Magharibi imeunadi kwa ulimwengu kwa miaka mingi.

Maoni:

Uozo wa Kidemokrasia

Trump daima amekuwa akuwa na sifa ya kiburi, ubaguzi na ubinafsi. Kuregea kwake madarakani nchini Marekani kunadhihirisha mgogoro mpana wa uongozi ambao sio tu unatishia Amerika lakini pia unahujumu fahamu nzima ya demokrasia ya Magharibi. Wakati mhalifu aliyepatikana na hatia na mtu mpotovu waziwazi anaweza kuwekwa kuongoza nchi yenye nguvu zaidi ulimwenguni, kwa mara nyingine tena inafichua jinsi demokrasia ilivyo tepetevu, fisadi, na yenye uwezo wa kutumiwa vibaya. Ule unaoitwa utawala wa watu unasimama wazi zaidi kuliko hapo awali kama jukwaa la watu wenye kiburi, maslahi makubwa, na kipote cha wabaguzi ambao hawajali mahitaji ya kweli ya watu. Kipote hicho hudhibiti simulizi na mtiririko wa pesa, huku watu wakipotoshwa kuamini kuwa wana ushawishi wa halisi. Yale yanayoitwa maadili ya kidemokrasia si chochote ila ni udanganyifu unaotumiwa kuendesha, kudhibiti, na kukoloni watu na mataifa. Hili si jambo la Marekani pekee—linaonyesha uozo jumla wa demokrasia na mgogoro mkubwa wa uongozi katika nchi za Magharibi.

Uhuru, haki, na utu kwa muda mrefu zimekuwa kauli mbiu za Magharibi, lakini ukweli umethibitishwa kuwa na kitu cheusi zaidi. Ulimwengu wa Magharibi haujawahi kuwa mdhamini wa haki au utu; kinyume chake, kihistoria umetumia vyombo vyake vya nguvu kukandamiza, kutawala, kukoloni na kuharibu mataifa mengine. Unaendelea kufanya hivyo leo. Si mfumo unaowalinda wanyonge au unaojali manufaa ya binadamu wote. Badala yake, ni mfumo uliobuniwa kulinda kipote cha mabepari waliobahatika na kudumisha hali halisi iliyopo ambayo inahifadhi utawala wa Magharibi juu ya sehemu zengine za ulimwengu.

Mfumo Mpya wa Kisiasa Unahitajika

Kwa Umma wa Kiislamu, tukio hili ni ukumbusho kwamba hatuwezi kuweka matumaini na mustakabali wetu katika mikono ya dola za Magharibi au viongozi wao, kama baadhi, kwa bahati mbaya, walivyoamini. Wakati Waislamu mjini Gaza wanakabiliwa na mauaji ya halaiki, mara kwa mara tunaona jumuiya ya kimataifa ikifumbia macho.

Ikiwa tunataka kuwasaidia Waislamu nchi Palestina, haitakuwa kupitia Ikulu ya White House! Ni wakati sasa wa kugeuka ndani na kuunda upya mifumo yetu wenyewe kwa misingi ya haki, huruma na umoja. Khilafah ya Kiislamu si ndoto—ni wajibu wa Mwenyezi Mungu na hitaji la kivitendo, ikiwa tunataka kuona uadilifu na utu wa mwanadamu vikipewa kipaumbele katika ulimwengu huu. Hatima yetu haiwezi kutegemea matokeo ya uchaguzi jijini Washington au Paris bali lazima ijengwe kwa nguvu na ukinaifu wetu wenyewe.

Huku Magharibi ikiyumba chini ya uzito wa migongano na migogoro yake, sisi, kama Waislamu, tunayo fursa ya pekee ya kufufua zama za dhahabu ambapo Khilafah ilikuwa ni mwenge wa uadilifu, utu na maendeleo kwa ulimwengu mzima. Ukombozi wa Palestina na ulinzi wa wanyonge mjini Gaza na kwengineko unaweza kutokea tu kupitia Umma wa Kiislamu ulioungana chini ya uongozi wa Khilafah. Ndilo suluhisho—sio kwa Waislamu tu bali kwa wanadamu wote, ambao wanazidi kuteseka chini ya utawala na dhulma ya mfumo wa Magharibi.

Umma wa Kiislamu ndani yake wenyewe una masharti yote ya kuchukua vazi la uongozi. Ni wakati sasa wa Waislamu kuinuka, kukataa mfumo wa sasa wa kisiasa, na kuwa nuru inayowaonyesha wanadamu njia ya kuelekea kwenye jamii adilifu, yenye msingi wa sheria za mungu na uadilifu wa kimaadili.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote.” (Surah An-Nur, 24:55)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ibrahim Atrach

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu