Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Huzuni Inazidi Huku Trump Akiwapa Mgongo Wafuasi wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waislamu waliompigia kura Trump walichukizwa na wateule wake wa baraza la mawaziri wanaomuunga mkono ‘Israel’.

WASHINGTON, Nov 14 (Reuters) - Viongozi wa Waislamu wa Marekani waliomuunga mkono Donald Trump wa Republican kupinga uungaji mkono wa utawala wa Biden kwa vita vya ‘Israel’ dhidi ya Gaza na mashambulizi dhidi ya Lebanon wamevunjwa moyo sana na uteuzi wake wa Baraza la Mawaziri, waliambia shirika la habari la Reuters. (Reuters)

Maoni:

Viongozi wa Waislamu nchini Marekani waliomuunga mkono Donald Trump katika uchaguzi wa 2024 wanajikuta wakikabiliana tena na majuto. Wengi waliamini uungaji mkono wao ulikuwa aina ya kulaani dhidi ya jibu duni la utawala wa Biden kwa ukatili wa mauaji ya halaiki, wakitumai kubadilisha mizani ya kisiasa ili kupendelea hamu za Waislamu. Hata hivyo, matumaini yao yamekatishwa kwa uteuzi wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri la Trump, ambao umesababisha mshtuko mkubwa.

Kinachosumbua zaidi ni uteuzi wa Marco Rubio kama Waziri wa Mambo ya Nje, Pete Hegseth kama Waziri wa Ulinzi, Mike Huckabee kama balozi wa umbile la Kiyahudi, na Elise Stefanik kama balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. Kila mmoja wa wateule hao ana historia ya uungaji mkono mkubwa kwa ukaliaji kimabavu wa Kizayuni, msimamo ambao unapingana vikali na maadili na matarajio ya jamii za Kiislamu. Matarajio kwamba uungaji mkono wao kwa Trump ungeleta mabadiliko chanya katika sera ya Marekani kuelekea ulimwengu wa Kiislamu umethibitika kuwa haufai. Badala yake, uteuzi huu unaangazia utawala unaofungamana zaidi na ajenda ya Kizayuni ambayo wengi walikuwa wanaihofia.

Viongozi wa jamii hiyo wameelezea kusikitishwa kwao, wakimtuhumu Trump kwa kusaliti ahadi alizotoa wakati wa kampeni. Usaliti huu umechochea hisia za udhalilifu miongoni mwa wale walioamini kwamba ushiriki wao kwa namna fulani ungeathiri mabadiliko ya kisiasa.

Hali hiyo inatumika kama ukumbusho dhahiri kwamba Waislamu wanahitaji kurudi nyuma kwenye kufanya kazi halisi ili kuregesha mfumo wao wa maisha. Uharakati wa kisiasa wa Kiislamu lazima ubakie katika kuamrisha mema, kukataza maovu, na kushikamana na Aqida. Kushiriki katika mifumo inayotunga sheria kinyume na sheria za Mwenyezi Mungu sio tu hairuhusiwi (haram) bali pia haina ufanisi katika kufikia uadilifu kwa Umma wa Kiislamu. Waislamu wanakumbushwa kwamba mabadiliko ya kweli hayatokani na kukiuka kanuni kwa ajili ya manufaa ya muda mfupi bali kutokana na kujitolea kwa uthabiti kwa hukmu za Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya pale aliposema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma’ida:51]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu