- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ulimwenguni wa Kusini na Mfumo Mpya wa Ulimwengu – Tumaini au Sarabi?
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Aprili 2025, wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa BRICS nchini Brazil, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia Datuk Seri Mohamad Hasan alitoa ujumbe ulio wazi: ulimwengu hauwezi tena kutegemea utawala wa dola moja ili kuhakikisha utulivu wa kimataifa. Alihimiza mataifa ya Kusini mwa Ulimwengu – inayojumuisha nchi zinazoendelea kote Asia, Afrika, Amerika ya Kusini, na Oceania – kuinuka kwa pamoja na kuongoza uundaji wa mfumo mpya wa kilimwengu. Matamshi yake yanaangazia sauti za vibwagizo vinazokua zisizoridhika na utawala wa muda mrefu na kuanguka kwa uaminifu wa utawala wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.
Maoni:
Wito wa mfumo mpya wa ulimwengu wa Ulimwengu wa Kusini unatokana na kukatishwa tamaa kwa kweli na kufeli kwa uongozi wa nchini moja. Kwa miongo kadhaa, Marekani imetumia taasisi za kimataifa na uwezo wake wa kijeshi kuunda mfumo wa kimataifa unaozingatia uliberali, ubepari, usekula, na maslahi yake ya kimkakati. Hata hivyo, uingiliaji kati wa muda mrefu wa kijeshi, kukosekana kwa usawa wa kiuchumi, na deni la taifa linaloongezeka kila mara kumedhoofisha uhalali wake na hadhi ya kimataifa.
Nyufa za kimaadili na kimuundo katika uongozi wa Marekani sasa zinaonekana – kutoka kwa mateso ya binadamu ya vita nchini Iraq, Afghanistan, na kwengineko, hadi uungaji mkono wake usioyumba kwa umbile haramu la Kiyahudi huku kukiwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huko Palestina. Mambo haya yameharakisha utafutaji wa miundo badali ya uongozi wa kilimwengu, huku dola viongozi nyingi zikiibuka kama muundo unaowezekana wa siku zijazo.
Hata hivyo, ingawa Ulimwengu wa Kusini mara nyingi hutajwa kuwa injini inayowezekana ya mfumo huo mpya wa ulimwengu, vikwazo vikubwa vinaendelea kuwepo. Kambi hiyo inasalia kuwa jumuiko la mataifa yaliogawanyika bila ya:
- Msingi wa shirika wa kimfumo;
- Mkakati ulioratibiwa wa kisiasa au kijeshi;
- Miundo ya taasisi au utawala kwa ajili ya uongozi wa pamoja.
Wanachama wake hutofautiana sana katika mifumo ya kisiasa, maslahi ya kiuchumi, na upatanishi wa kisiasa wa kieneo – na wengi wanasalia kutegemea sana mamlaka ya nje kwa biashara, usalama na miundombinu ya kiteknolojia. Bila mtazamo imara wa ulimwengu au dhamira ya kuunganisha, Ulimwengu wa Kusini hauwezekani kuwasilisha njia badali ya kuaminika kwa mpangilio unaofifia wa uongozi wa nchi moja (unipolar).
Kinyume chake, Uislamu unatoa dira yenye msingi wa kihistoria na kamilifu kimfumo kwa uongozi wa kimataifa. Chini ya Khilafah, ulimwengu wa Kiislamu wakati fulani ulianzisha mtindo mpana wa hadhara – ambao ulitawala katika mabara yote kwa uadilifu, utulivu wa kiuchumi, na mafanikio ya kifikra. Tofauti na mifumo ya kisekula, mtazamo wa ulimwengu wa Uislamu umejikita katika Wahyi, ulio mtukufu, na unafungamana kimaumbile na utu na uadilifu wa mwanadamu.
Leo, ulimwengu wa Kiislamu una viungo muhimu vya uongozi: idadi kubwa ya watu, maliasili nyingi sana, jiografia ya kimkakati, na muhimu zaidi, aqidah inayounganisha. Kilichosalia ni utashi wa kisiasa wa kuondokana na mgawanyiko na kusimamisha tena utawala jumla unaokita mizizi katika Sharia.
Kuanguka kwa utawala wa Marekani kunaashiria mwanya nadra wa kisiasa za kieneo. Hata hivyo, isipokuwa Ummah wa Kiislamu ukamate fursa hii kwa uwazi wa kimfumo na umoja wa lengo, ruwaza ya mfumo mpya wa ulimwengu itabakia kuwa ni sarabi. Uongozi hauwezi kuchukuliwa kutoka nje – lazima uregeshwe. Uislamu sio tu kwamba una uwezo wa kuongoza mfumo adilifu wa ulimwengu – umekadiriwa kufanya hivyo.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad - Malaysia